baby zu
JF-Expert Member
- Nov 9, 2015
- 1,816
- 4,770
Daaa nami nina rafiki alikua mwema sana kwangu, ni mtu ambae sikuwahi kufikiria kama nitamtoa kwenye maisha japo mpaka sasa namkumbuka kwa wema wake kwangu,,Hii ilinitokea kwa rafiki yangu mmoja ambaye tulikua tumeshibana haswa kwa miaka mingi, niliamini tutakua close mpaka tukiwa vibibi. Huu urafiki ulivyoisha (kwa sababu ya mgogoro wa kifedha, tulianzisha biashara pamoja) iliniuma kuliko breakup ya mwanaume yoyote. Alihama nchi na hivi karibuni niliona ameview status yangu whatsapp, sijui ilikua kimakosa au alidhamiria. Huwa namkumbuka sana, na kila nikipiga hatua mpya kwenye kazi au maisha nafikiria angekuwepo tungefurahiaje pamoja hilo tukio, nabaki kuumia tu!
Tatizo letu nilimshauri kuhusu mwenendo wake wa matumizi ya pesa ila akachukulia tofauti alinitumia msg ambayo imegoma kufutika kwenye moyo "futa namba zangu na za mama yangu hatukuhitaji kwenye maisha yetu" daaa nilizifuta kweli na mpaka sasa ni miaka miwili bila mawasilianilo japo namwombea Mungu ambariki sana ktk maisha yake