Marafiki hawadumu wanakuja na kuondoka, tuliowahi kuwa mabesti nao leo tunaishia kuchunguliana status hata "hi" hakuna

Nyakati zinabadilika jifunze kubadilika nazo😄
 
Nimepoteza marafiki zangu wengi nilipoolewa aisee...wengine naumia maana nikikumbuka moments zetu pindi tupo chuoni daah...sema ndo hivyo no way out...unakuta unamtafuta mtu ww tuu...yani inakua one side communication..unaamua kuacha tuu..
Kuna best angu urafiki umekoma juzi juzi kisa tuu sijamchangia mdogo wake alikua anaoa kiasi cha hela alonichangia kwny harusi yangu jamani tena alikua anakumbushia mimi nilikutolea hii...so mm nimetoa hela ya kadi..as long as harusi iko mbali na nisingeweza kuhudhuria nikamwabia ukiolewaga ww ndo ulalamike akanchunia nahisi kaniblock...
Niliumia basi nimeachana nae...any way maisha nadhani ndivyo yalivyo..
Uzi umenigusa...
 
Umeongea ukweli halisi.
 
Poleee Dear!!
 
Marafiki wengi uwa wako kimaslahi zaidi, ndio maana ukiwa na pesa na marafiki wanakua wengi na zikiisha wanakukimbia unabaki mwenyewe. Marafiki wengine unaweza ukawa huna kitu ila wamekuotea kuna siku utakua vizuri kwa hio wanakua na wewe tu, lakini ukweli ni kua URAFIKI NI UNAFIKI. Urafiki wa kweli ni familia yako.
 
Pole dear mi nipo kwa ajili yako mtani wangu 🤗😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…