Marafiki wa kweli ni wa utotoni

Marafiki wa kweli ni wa utotoni

Usiumizwe sana na marafiki wa ukubwani
Usiwaamini sana marafiki wa ukubwani
Wachache sana huwa wakweli na wasio na agenda kificho
Marafiki wa kukutana high school
Marafiki wa kukutana vyuoni
Marafiki wa kukutana makazini
Marafiki wa kukutana ukubwani kwenye biashara, uchumba nknk.. Si marafiki halisi bali ni marafiki kwa sababu fulani

Hawa ni mpaka mkae muda mrefu sana pamoja kwenye hali zote shida na raha, kukosa na kupata, kuumia na kuumizwa! Wengi wao rangi zao halisi hujifunua huku!

Rafiki uliyekua naye mkasoma wote shule ya msingi, mkacheza pamoja, mkachunga pamoja,mkalima pamoja mkatembeleana, mkacheka pamoja mkalia pamoja, familia zenu zinafahamiana ndugu zenu wanafahamiana.. Hawa ndio huwa marafiki wa kweli kwakuwa bond wanayoijenga huwa na vyanzo vingi.. Hawadahauliani na ni vigumu mno kusalitiana!

Tunakutana na watu wapya kila siku, wema na wabaya! Na wabaya waliojificha kwenye joho la wema! Sio dhambi kuwa na marafiki wapya! Maisha ni watu bila watu hakuna maisha ama maisha yanakuwa hayana maana!

Rai tangu ni hii kuwa makini sana unapochagua marafiki wa ukubwani.. Wengi ni marafiki wa agenda.. Wengi ni marafiki kwa sababu . Agenda ikiisha/ikifa ama sababu ikikoma na urafiki nao hufika tamati

Ninao marafiki wengi na ninawaamini sana ila baadhi wameniachia makovu .. Siumii kwakuwa natambua marafiki wa kweli ni wale wa utotoni[emoji2827]View attachment 2519891
Nakubaliana na wewe mzee Mshana Jr, utotoni mtu anakuwa bado hajaingiwa na hila, ukubwani huku watu wameshapigwa na maisha ni mabalaa tu
 
Sahihi mkuu,hata huyu ismail azizi kader(azam fc)...jamaa wa home na hana dharau hata nkimpigia saa 6 usiku anapokea...
Ila kuna maboya nlisoma nao TUMAINI,wamebadirika ajabu na wamesahau nyakat tulizopita pamoja
Huo ndio urafiki mkuu ,kader bonge la player,,mm yupo kijna Mmoja meshak Abraham sjui sasa Yuko wap ila nshaacha kumfatilia mana aliona nikama tunalia shida kwake
 
Rafiki ndio ndugu unabidi kuhakikisha unapata wa kweli mmoja ,wawili au watatu na wanne ..

Mimi nilipata rafiki Chuoni niseme huyu Jamaa namkubali Sana kuzidi Hadi ndugu zangu wote wa ukoo mzima achilia mbali wazazi

Huyo Mwamba ni rafiki yangu wa ukubwani ukitoa JF anafata yeye.
Hongera! Ila kwa maisha ya sasa hivi kuwa na marafiki watat au wawili ni wengi sana aisee! Ukibahatika kumpata mmoja wa kweli nyakati hizi. Utakuwa ni mmojawapo wa wenye bahati kubwa!
 
Mimi sina bahati ya Marafiki [emoji24]
Sina Rafiki wa Utotoni wala wa Ukubwani,
Hua natamani sana nikiona Marafiki wameshibana, wanataniana, wanasaidiana, wanaambatana sehemu pamoja, hata nikiangalia movies inayoonesha marafiki fulani wamepambana pamoja hua nawish na mimi ningempata Mtu/Watu wa namna hiyo,

What is wrong with me [emoji24][emoji24][emoji24]
 
Rafiki yako wa ukweli kabisa ni mama yako mzazi...
9f935d9544816c58b2a73b4f6a1b71b2.jpg
 
Mimi sina bahati ya Marafiki [emoji24]
Sina Rafiki wa Utotoni wala wa Ukubwani,
Hua natamani sana nikiona Marafiki wameshibana, wanataniana, wanasaidiana, wanaambatana sehemu pamoja, hata nikiangalia movies inayoonesha marafiki fulani wamepambana pamoja hua nawish na mimi ningempata Mtu/Watu wa namna hiyo,

What is wrong with me [emoji24][emoji24][emoji24]
Nitakuwa rafiki yako.. Don't regret what you have! Mariposa
 
Mimi sina bahati ya Marafiki [emoji24]
Sina Rafiki wa Utotoni wala wa Ukubwani,
Hua natamani sana nikiona Marafiki wameshibana, wanataniana, wanasaidiana, wanaambatana sehemu pamoja, hata nikiangalia movies inayoonesha marafiki fulani wamepambana pamoja hua nawish na mimi ningempata Mtu/Watu wa namna hiyo,

What is wrong with me [emoji24][emoji24][emoji24]

Utapata labda Kama unatabia mbovu mbovu Kama ulevi ,umalaya ,kuongelea watu uchoyo n.k tofauti na hapo utapata tu.

Mimi rafiki yangu ni Mchamungu Sana
Hapendi pombe
Hardworking

So nimeshare naye Mambo Mengi.

Na wewe ishi umo.
 
Unataka kusema wenye tabia mbovu hawana marafiki?
Mimi nawaona Walevi na Wazinzi kila siku wameshibana na kusaidiana halafu wataka kusemaje,

Kila Mtu huambatana na wa kuendana nae.
 
Back
Top Bottom