secretarybird
JF-Expert Member
- Aug 22, 2024
- 23,984
- 51,055
SawaMarafiki wanutotoni Wana sifa zifuatazo:-
1. Wenye wivu mkali japokuwa hawana unafiki, ukifaulu masomo watakuambia unaringa.
2. Ni wachomaji wakubwa, yaani rafiki yako anaweza kumfikishia taarifa zako mwalimu ili tu uchapwe wafurahi.
3. Wanafurihia matatizo ya wengine kwa mfano ukichapwa basi wanafurahi kinoma.
4. Hawawezi kukutunzia Siri wala madhaifu kwa mfano kama āhujatahiriwa watakutangaza mbele ya darasa na kukupa majina mbalimbali mfano 'govinda'.
5. Ni machawa wa wanafunzi wanatoka kwenye familia za kitajiri au kwa wanafunzi wanye vipaji mbalimbali kama kucheza Mpira wa chandimu nadhani Tlaatlaah Lucas Mwashambwa na ChoiceVariable karia waliianza huku.
STORY.
Kuna siku pale shuleni nilipanda kwenye mwembe halafu chini ya mwembe kulikuwa na rafiki yangu zephania, sasa isivyobahati mwalimu wa Hisabati akawa anapita, nilipomwana mwalimu anakuja nilimwonesha ishara zephania kuwa atulie ili mwalimu asinishtukie.
Kumbe zepha alikuwa anatamani mwalimu anione anaichape ili tu yeye afurahi.
Zepha akatulia lakini mwalimu alipokaribia Zephania akaanza kuniambia "oya secretarybird jifiche vizuri mwalimu atakuona, jifiche mwalimu atakuona..." aliendelea kutamka maneno haya ili mwalimu anione na hatimaye alifanikisha jambo lake.
Mwalimu alipofika chini ya mti akamwuliza Zephania kwanini anaongea peke yake lakini zepha aliendelea kutamka yale maneno huku akikodoa juu ya mti nilikokuwa Mimi.
Aise mwalimu aliniona na alinishushia kipigo cha mbwa mwizi, nilipotoka hapo nikamwende Zepha na kumwuliza kwa nini alimfanya vile lakini jibu lake akiniambia kuwa alikuwa ananisidia ili mwalimu asinine.
Tangu siku hiyo niliacha kuwa na urafiki mazima, kimoyo Moyo nikajisemea "utafikiri ni kumanyoko"
Al-mukheef mzabzab Monetary doctor unawzungumziaje marafiki wa utotoni.
Nimeshasema marafiki ni kumanyoko ndo maana sina rafiki wa ukubwani.hao wa ukibwani wamekusaidia nini
Hakika huyo rafiki yako alikuwa wa tofauti sana, marafiki wengi huwa ni vichomi yaani furaha yao ni kuona wewe ukidhalilika ili wakutangaze kwa wengine.Kuna baadhi walikuwa masnitch sana ila haimanishi hakuna marafiki Bora waliokuwa tayari kuumia kwa ajili yetu
Kuna rafiki yangu alikuwa tayari kuumia peke yake hata kama kesi ya kwenu wote,sometimes walimu wanoko wakimdaka yeye wanamlazimisha akutaje na wewe maana wanakutamani sana ila jamaa anakataa kuwa hujashiriki kwenye hiyo kesi na msalaba wako anaubeba
Japo sasahivi wengi wao hatupo na ukaribu sana ila jah awabless sanaššš
Masnitch wapo tena wengi sana kuanzia mtaani tulipozaliwa shuleni mpaka maeneo yetu ya kaziHakika huyo rafiki yako alikuwa wa tofauti sana, marafiki wengi huwa ni vichomi yaani furaha yao ni kuona wewe ukidhalilika ili wakutangaze kwa wengine.
usiruhusu rafiki wakutumie, wewe ndio uwatumieNimeshasema marafiki ni kumanyoko ndo maana sina rafiki wa ukubwani.
Umenenausiruhusu rafiki wakutumie, wewe ndio uwatumie
Saa name usiku ukilala wanaenda kusoma kimya kimya bila wewe kuwa na taarifa.Masnitch wapo tena wengi sana kuanzia mtaani tulipozaliwa shuleni mpaka maeneo yetu ya kazi
Mfano shuleni Kuna wale ambao wanakushawishi kwa nguvu zote msiende kusoma na wewe unajaa kwenye mifumo yake ila yeye ikifika mida yake kimya kimya anaenda kupiga pindi
Matokeo ya paper yakija unabaki kushangaa tu kivipi kafaulu wakati hatujasoma wote
Mamodinyo wengi walikuwa wale watoto wanaojua kusuka Mipira ya chandimu halafu hawajui kucheza Mpira so kwa sababu wao ndio wamiliki wa Mpira lazima wacheza halafu ukiwa unajua kucheza basi lazima uwe upande wao.Ndugu zako mamodinyo unahisi walikuwa marafiki wanamna Gani???
Na SI ndiyo wale darasa zima mnaomba mwalimu asikumbuke kama aliacha test yake ya math ila yeye akimuona anaondoka bila kukagua test linanyoosha mikono "teacher umesahau kukagua test yako"Mamodinyo wengi walikuwa wale watoto wanaojua kusuka Mipira ya chandimu halafu hawajui kucheza Mpira so kwa sababu wao ndio wamiliki wa Mpira lazima wacheza halafu ukiwa unajua kucheza basi lazima uwe upande wao.
Timu yake ikifungwa/akiumizwa mguu anachukua Mpira wake anauweka kwapani huyoooo! Anachechemea na miguu yake iliyopinda kulielekea darasa na darasani akifika anaanza kuandika majina ya wapiga kelele na kumpa class monitor.
Ni marafiki wakubwa wa mamonitor na time keepers.
Siku akipewa nafasi ya kugonga kengele ya chakula analielekea kengele kwa kunesa nesa ili wanafunzi wote wamwone.
Hatimaye jioni anawahadithia wazazi na wadogo zake jinsi alivyopewa fursa asiyoitegemea ya kuhonga kengele.
Al-mukheef mamodinyo utawaweza?
Akishafanya yeye anamkumbusha tichaš¤£.Na SI ndiyo wale darasa zima mnaomba mwalimu asikumbuke kama aliacha test yake ya math ila yeye akimuona anaondoka bila kukagua test linanyoosha mikono "teacher umesahau kukagua test yako"
Marafiki wa ukubwani pia ni wabaya ila hawajioneshi directly ndiyo maana ili kuwajua unatakiwa utilize akili.Utotoni hakuna pesa ndio maana una marafiki wengi.
Ila ukubwani pesa,mafanikio,ufukara,matatizo,mahusiano ndio itakupa rafiki ambaye muhimu kabisa.
Akishafanya yeye anamkumbusha tichaš¤£.
Pia anatengeneza ukaribu na watoto wa Waalimu, anaiba hela ya vikoba ya mama yake au anaiba mayai ya kuku ili anunue karanga, puto au pipi na kuwagawia watoto wa Waalimu kwa minajili ya kuimarisha urafiki.
Matapeli wakubwa.