“Marafiki wanaotegemewa na wenzi wa dhati” miaka hii ya uhusiano kati ya China na Tanzania

“Marafiki wanaotegemewa na wenzi wa dhati” miaka hii ya uhusiano kati ya China na Tanzania

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
4719351211760023601.jpg


Pili Mwinyi

Tarehe 24 Machi mwaka 2013, rais Xi Jinping alikanyaga kwa mara ya kwanza ardhi ya Tanzania tangu awe rais wa Jamhuri ya Watu wa China. Katika kipindi chote hicho cha miaka tisa yameshuhudiwa mabadiliko makubwa ndani ya nchi pamoja na mchango mkubwa alioutoa katika nchi za nje hasa nchi za Afrika. Rais Xi alikalia kiti cha urais huku akiwa na malengo mengi mazuri kuhusu Afrika. Na kuonesha umuhimu wa uongozi wa marais na kazi zao katika kukuza uhusiano na Afrika.

Katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Xi, akiwa anaizingatia zaidi Afrika, sera ya China kwa Afrika ikaanza kuonesha mwelekeo mpya, ambapo tulishuhudia vipaumbele na mikakati ya Beijing ikibadilika kwa bara la Afrika. Mwelekeo huu hadi sasa umekuwa na faida na tija kubwa kwa mustakabali wa uhusiano wa China na Afrika.

Ziara hii ya aina yake barani Afrika aliyoifanya mwaka 2013, ikiwa ni safari yake ya kwanza nje ya nchi kama mkuu wa nchi, ilimfikisha katika nchi za Tanzania, Jamhuri ya Kongo na Afrika Kusini. Baada ya kuondoka Russia, kituo chake cha kwanza katika Afrika kilikuwa Tanzania. Wakati yupo nchi Tanzania alisaini mikataba 19 na serikali ya Tanzania kwa ajili ya miradi iliyopangwa kutekelezwa kwa pamoja na nchi hizo mbili.

Kabla ya rais wa China Xi Jinping kufika Tanzania, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania wa wakati huo Bernard Membe, alisema ziara hiyo ya kiongozi mwenye ushawishi mkubwa duniani itakuwa ya kihistoria, na kuielezea kama ni heshima kubwa na ya aina yake ambayo italeta fursa nyingi kwa Tanzania na pia itadumisha urafiki wa jadi uliopo kati ya pande hizo mbili.

“Reli ya TAZARA iliyojengwa na China nchini Tanzania katika miaka ya 70 imetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi ya bara la Afrika na ni ushahidi wa urafiki kati ya Tanzania na China na kati ya China na Afrika.” alisema Membe.

Ziara hii ilitoa funzo kubwa kwa wadau wa nchi mbalimbali za Afrika. Kwani angeweza kuanza kutembelea mabara mengine kama vile Ulaya au hata kwenda Marekani. Lakini alithamini uhusiano na urafiki wa jadi, na kuamua kwanza kuwapa heshima marafiki zake wa Afrika hasa Tanzania kwa kwenda kuwatembelea akiwa kama rais mpya.

Baada ya kuwasili Tanzania tarehe 24 Machi 2013 rais Kikwete na Watanzania wengine walimpa makaribisho makubwa rais Xi na mke wake mama Peng Liyuan. Katika hotuba yake rais Kikwete alisema haamini kwamba rais Xi ameichagua Tanzania kuwa kituo chake cha kwanza kutembelea katika Afrika. Hivyo alipata hamasa ya kujifunza sentesi moja ya Kichina isemayo “Ndoto ya China, kweli imetimia", akiwa na lengo la kuitumia na kuisema mbele ya rais Xi.

China, chini ya rais Xi imeshuhudiwa ikiongeza kwa kiasi kikubwa ushiriki wake wa moja kwa moja katika masuala mbalimbali ya Afrika. Katika mwaka huohuo baada ya kuwa rais, Xi alitoa pendekezo la kuanzishwa kwa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”. Pendekezo hili lenye lengo la kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na mafungamano baina ya kanda, lilipokelewa kwa mikono miwili na kwa moyo mkunjufu na Afrika.

Tanzania ambayo ipo kwenye pendekezo hili, imezidisha ushirikiano wake na China chini ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, katika nyanja za kilimo, umeme, biashara, uwekezaji, miundombinu, nishati na nyinginezo. Kuanzia hapo China, chini ya rais Xi ikapanua ufadhili wake kwa Tanzania.

Hivi sasa, China imekuwa mshirika mkubwa wa biashara wa Tanzania na mwekezaji mkubwa wa pili kutoka nje. Uwekezaji wa China nchini Tanzania umeendelea kuongezeka, ukiwa ni zaidi ya dola bilioni 1 za Kimarekani. Uhusiano huu wa China na Tanzania umeshuhudia uwekezaji wa China ukileta maendeleo ya uchumi na kutoa fursa za ajira zaidi ya elfu 80 kwa wenyeji.

W020220320714858240711.jpg

Ni hivi majuzi tu waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi alimkaribisha mwenzake wa Tanzania Liberata Mulamula aliyekuwa ziarani hapa nchini kwa njia ya video. Wakati wa mazungumzo yao Wang Yi alisema China iko tayari kuangalia uhusiano kati ya China na Tanzania kwa mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, na chini ya makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizi mbili, wataendelea kuimarisha ushirikiano na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo huru ya bara la Afrika.

Tangu rais Xi aweke msisitizo wake kwa Afrika naweza kusema ushirikiano kati ya China na Tanzania sasa umekuwa imara zaidi na upo kwenye kipindi kizuri cha historia. Kuna msemo maarufu kwamba “Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli” China imejitahidi sana kusaidia kupandisha hadhi ya Tanzania na Afrika kimataifa, na kuihimiza jamii ya kimataifa kuitilia maanani zaidi na kuwekeza katika Afrika.

Kwa ujumla ile dhana ya China ya “viongozi ni lazima wawatumikie wananchi”, na “wananchi ndio mabwana wa nchi”, inaonekana waziwazi kwa rais Xi, na dhana hii sio kwamba anaitumia China tu, bali pia anaitumia hata kwa marafiki zake wa Afrika. Waswahili wanasema “Chanda chema huvikwa pete” Kwa juhudi za rais Xi alizozifanya katika miaka yote hii tisa za kuhakikisha anapandisha hadhi ya ushirikiano na uhusiano baina ya China na Tanzania na baina ya China na Afrika kwa kuzihimiza na kuzivuta nchi za Afrika ili nazo zifikie hatua ile ambayo imeifikia, kweli zinastahili pongezi kubwa.
 
Back
Top Bottom