Marafiki zangu nawapenda ila mke wangu nampenda na kumsikiliza

Ohoooo! LIMBWATA limeshakuteka. Hongera sana Mkuu msalimie shem Sabrina.
 
Weka msingi wa familia kwanza,marafiki wapo tu na wao wakioa wataelewa tu..Maana marafiki nao muhimu sana kweny harakati zetu
 
Mwanamke katimiza wajibu wake kukutenga na watu wako wa karibu sio kwa ubaya lakini ni kwa sababu anakupenda and she wants you all to herself. Tatizo ni siku mambo yakienda mrama jua utakua peke yako
 
Mkuu uko sahihi japo unakosea
 
Atakapopata mtoto wa kumkeep busy utaelewa 😂😂😂 sahizi mpo kwenye honeymoon phase kila saa mke anatamani uwepo around!
 

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeongea umama kweli siku ukizinguana na mkeo utawatafuta washkaji......
unachotakiwa ni kubalance tu sio kuwatosa jamaa......
usiwe limbukeni sana
Pamoja sana soma andiko mkuu inaonekana kwenu bado maleria mnaipima kwa kuangalia homa
 
Ndoa mpya na hapo unajiona utadumu hivohivo hutokuja kubadilika siyo? Uliza kwanza acha pupa
 
Sabrina mjibu mwenzio, nasi tutambue uwepo wako
 
Hongera Mtoa mada,
Mke au Mume ni zaidi ya rafiki, ndugu na jamaa.
Ni mtu wako wa karibu ambae unapaswa mthamini sana. Wengine wataendelea kuwa marafiki bila kuadhiri urafiki wa Mke/Mume.

Rafiki inaweza kuonana nae mara moja hata kwa wiki au mwezi ila ulienae ndani ni kila siku uko nae katika raha na shida, milima na mabonde, wengine wanaweza kuwa na wewe wakati wa raha tu.

Kila mtu anapaswa kumfanya mwenza wake rafiki yake mkuu namba moja baada ya Mungu.

Nawasilisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…