Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
MARAFIKI ZETU MTUSAMEHE SANA
Siku zote ukimya wa marafiki unaumiza kuliko kelele za maadui. Lakini marafiki zetu mtuelewe kwamba ukimya wetu haumaanishi kujitenga, kuringa wala kuvimbiana.
Haimaanishi urafiki wetu umekufa au Kuna chuki na uadui ndani yetu umezaliwa. Hapana!! Sio hivyo!!
Nikiwa naandika haya napenda niwaambie marafiki zetu kuwa
"SISI BADO NI MARAFIKI ZENU."
Ni muda sasa wa marafiki zetu kutambua kuwa sasa tumekuwa na vitu havipo tena kama zamani. Ule muda tuliokuwa tunautumia kupiga story kwenye vigenge sasa tunautumia kwenye mapambano ya kusaka tonge.
Lakini pia marafiki zetu mtambue kuwa tunapitia changamoto nyingi ambazo hatuwezi kuzieleleza mitandaoni.
Kwasasa tuna wapenzi ambao tunahitaji muda wa kuwasoma ili kuona kama wanafaha kuanza nao maisha ya ndoa. Kuna wengine tayari tupo kwenye ndoa na tunategemewa na pande zote mbili za muungano, tunahitaji muda wa kutimiza majukumu yetu sawasawa.
Kuna wengine tunapitia msoto mkali sana wa kiuchumi, vichwa vinawaka moto yaani sio tu kesho bali hata leo hatujui tutakula nini.
Tusameheni sana kwa kutoonekana kwenye matukio yenu na kushindwa kuwachangia sherehe zenu kama hizo za birthday na harusi. Mambo bado magumu kwetu hadi sherehe tunaona kama anasa tu.
Tusameheni kwa sometimes kutoona comments zetu za hongera kwenye mafanikio yenu, haimaanishi hatujapendezwa na hatua zenu.
Tusameheni kwa kila simu tunazopishana nazo kwa kutokuwa karibu na simu kwasababu ya harakati za kimaisha. Haimaanishi kama tuna Kiburi, kujidai au kuwakataa.
Tusameheni kwa changamoto zenu tunazoshindwa kuzitatua ilihali kwa macho ya nje mnatuona kama uwezo huo tunao.
Binafsi naumia sana rafiki yangu unaponiomba buku tano tu wakati huo na mimi mfukoni sina kitu. Naumia zaidi pale mwana anapodhani kuwa namfanyia kusudi. Nyie hamjui tu.
Msichukulie ukimya wetu personal. Sisi sio maadui bali tuko bize kupigana na hizi haso ambazo hazijatulipa hadi hivi sasa. Dah! Inaumiza sana.
Kwenye harakati zetu, wengine tumeshadhurumiwa sana ila hatusemi tu.
Nimalize kwa kusema kwamba katika umri wetu huu tunatakiwa kuwa ngangari sana kwani tukilala sasa huenda tusiamke milele na tukicheza leo huenda kesho yetu ikaja kuwa mbaya sana kuliko leo.
Hakuna nafasi ya kuweka uadui na watu, hata ma X zetu ni marafiki zetu pia, ukimya wetu kwenu usiwe na tafsiri mbaya kwamba tunawachukia, hapana!!
AMANI na UPENDO kwa marafiki zetu wote.
LIKE , COMMENT & SHARE post hii kwa marafiki zako wengine.
Ahsanteni.