Marais Wa Africa na Ushirikina. Chanzo cha kutoendelea nchi nyingi za Afrika

Marais Wa Africa na Ushirikina. Chanzo cha kutoendelea nchi nyingi za Afrika

Guru Master

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2017
Posts
226
Reaction score
594
Moja ya mambo mengi yanayosababisha nchi za Kiafrika zisiendelee ni pamoja na asilimia kubwa ya viongozi wake kuingia katika uongozi kwa njia za kishirikina au kuamini ushirikina. hili limekuwa tatizo kubwa sana na kuna ushahidi namna ambavyo washirikina wamekuwa wakitumika hasa nyakati za uchaguzi. kuna shuhuda nyingi za viongozi kujihusisha na ushirikina katika nchi zetu za afrika.

1.Gambia . Rais wa nchi hii Bwana Yahya Jammeh yeye ameshahusika mara nyingi kwenye shughuli hizi za kishirikina kwa kuagiza kukamatwa wale ambao anaamini ni wachawi na walikuwa wakimsumbua katika utawala wake. hawa walikamatwa na kunyweshwa kwa nguvu dawa maalum ambayo alikuwa ametengenezewa na waganga wake ambao walikuwa wanatembea naye kila aendapo na ndiyo washauri wake wakuu. walikamatwa wachawi wapatao 1000 na wakawa wakiteswa na kunyweshwa hiyo dawa na katika tukio hilo wanaosemekana wachawi sita walifariki dunia kwa mateso waliyokuwa wakiyapata. Rais huyu amekuwa kila anapoenda anakuwa na kundi lake la waganga ambao humtengenezea mazingira ya eneo husika. amekuwa kila mwezi akihudhuria sehemu flan ambayo huenda kufanyiwa mambo ya kishirikina ili adumu kwenye uongozi.

2. mwaka flan katika nchi moja ya afrika mganga mmoja mkubwa alikuwa ndiye mpiga debe na mshauri mkuu wa mgombea urais mmoja na team yake. akimshauri mavazi gani avae na aina ya pete za kuvaa apendwe na katika hili inaonekana wengi hasa vijana na akina mama walionekana kurogeka na kujikuta wanamchagua mgombea huyo pasipo kujua kwa nini wanamchagua. na ushawah kutolewa utabiri wa kutishiwa kuwa mtu ambaye atampinga mgombea huyo kwenye uchaguzi flan atakufa. ukichukulia na mara kadhaa mgombea huyo kuanguka akiwa kwenye mikutano kwa kile kinachosemekana nguvu zake kuzidiwa na wachawi wengine. katika nchi za afrika kwa marais kuamini ushirikina ni jambo la kawaida kabisa. ashawah sikika rais mmoja akimwambia mgombea kuwa asiwe na waswas eneo ambalo anahutubia linashikiriwa naye kwa nguvu za giza.

3. Idd amin dada alikuwa rais wa uganda ambaye aliamini sana kwenye ushirikina. kila safari ambayo alikuwa akiifanya alihakikisha kuwa waganga wake wanamshauri kwanza na pengine kutangulia kutengeneza mazingira kabla hajaenda. na mara kadhaa ilikuwa inasemekana usiku alikuwa akiamka na kwenda kuonana na mganga wake chumba maalum ili aweze saidiwa mambo kadhaa ya kimila na hivyo kuzidi kuogopwa na wabaya wake kupatwa mabaya. idd amin alikuwa akiua watu na kuwaweka ndani na kula nyama zao haya ni kwa mujib wa aliyekuwa mfanyakazi wake miaka hiyo.

4. katika nchi moja afrika mashariki rais aliyeingia madarakani alikuwa akipata shida kulala ikulu kutokana na madudu yaliyokuwa yameachwa na aliyekuwa mtangulizi wake. rais huyo aliteseka kwa muda mpaka naye alipoletewa mganga na mmoja ya viongoz aliokuwa amewateua ili waweze sasa kurekebisha hali ya mule ndani ikulu na baadaye sasa kukalike.inasemekana hili jambo katika nchi hiyo lilisababisha impact kubwa sana na matokeo yake yakawa na athari kubwa katika nchi husika. marais, mawaziri na wabunge wamekuwa wakiamini sana kwenye ushirikina ili kupata vyeo au kudumu kwneye vyeo vyao.

5. muammar ghadaf aliyekuwa rais wa libya. huyu ni mmoja kati ya viongoz waliokuwa washirikina sana.na aliweza tengeneza hata urafiki na viongoz wengine wa nchi mbalimbali akiwapa pesa nyingi wamsaidie kupata waganga wakali zaidi aweze kuwa rais mwenye nguvu,anayesikilizwa na kupendwa na watu wengi.

6. viongozi kama Houphouet, Mobutu seseseko , Eyadema, Ahidjo, Bokassa, Sekou Toure hawa walikuwa wkaishiriki mara nyingi sana katika shughuli mbalimbali za kishiriina katika ikulu zao kwa kufukia wanyama wakiwa hai, kuwa consult waganga wa kienyeji maalum ambao ndiyo waliokuwa wakiwapa maelekezo mbalimbali na hata katika maamuzi makubwa hawa ndiyo walikuwa wakitoa ushauri. miaka ya 1990 ikulu ya zaire ilijawa na waganga kutoka Senegal, Mauritania and Mali ambao walikuja kumfanyia matambiko mobutu seseseko pamoja na familia yake. waganga walikuwa wengi sana toka nchi hizo na nyingine wakimfanyia dawa na matambiko. waganga hawa walifikia floor nzima ya Intercontinental Hotel huko Kinshasa wakiwa wameletwa na rais.

7. jonas savinmbi akiwa kiongozi wa UNITA alikuwa mmoja ya watu waliokuwa wakiamini sana wkenye ushirikina ili aweze jificha na pia hata kuroga waliokuwa wakimpinga na katika hili alifanikiwa kuwoandoa katika mazingira ya kutatanisha watu waliokuwa wakionekana kuwa na nguvu na hivyo kutishia uongozi wake.

8. laurent gbagbo huyu alikuwa akikataa kuingia moja ya ofisi moja katika jengo la ikulu kwa imani sababu ya iman za kishirikina huko cocody.

9. katika nchi flan afrika kuna rais ambaye ilikuwa kwa mwezi mara moja usiku anaondoka kwenda kwenye mto flan ambako huko hupotea ndani ya maji kwa kubebwa na mamba na kwenda katika ulimwengu usiojulikana kwa muda flan na baadaye kurudi akiwa mkavu kabisa bila hata kuloa. huyu ni mmoja ya viongozi katika afrika ambaye alikuwa na amekuwa akiamini sana uchawi na ushirikina hasa katika suala la yeye kupendwa na kuwa kiongozi. inasemekena alishawah kumroga na kumwozesha mguu mwananchi mmoja ambaye alionekana kuwa na mvuto katika jimbo lake na hivyo kumuondoa katika nafasi ya kushindana naye katika ubunge miaka hiyo akiwa mbunge na waziri.

katika nchi ya tanzania kumekuwa na matambiko mbalimbali kila mwaka wa uchaguzi ambayo hutumika kwa msimu huo mzima ili kumfanikisha mhusika kuwa na cheo alicho nacho. tulishashuhudia miaka flan kulikuwa na mauaji kwa ajili ya kuchuna ngozi zitumike kwenye shughuli za kishirikina zinazohusishwa na uchumi na siasa. baadaye likaja tambiko au kafara ya albino nayo ilikaa katika masikio ya watanzania kwa miaka 10 ikihusishwa na ushirikina katika shughuli za kisiasa na kiuchumi.

kuna shuhuda nyingi za wagombea ubunge kurogana ikiwepo moja mwaka flan mkoani tabora mgombea urais mmoja ilibidi apakizwe kwenye mkokoteni apitishwe njia ya nyingine baada ya kuwa ilibainika kuwa angepata ajali kama angetumia gari kutokana na utabiri wa mganga wake.

mkoani tabora pia imeshawah tokea mgombea mmoja kuhutubia ng'ombe waliokuwa wakila nyasi pasipo yeye kujua kuwa anahutubia wanyama kutokana na kuwa alikuwa ameshachezewa shere kwenye tukio hilo la kufanya kampeni. kuna kiongoz mmoja wa chama ambaye alikuwa mwalimu huko singida na baadaye akapanda vyeo hatimaye kufika ngazi za juu katika chama hicho huko mkoani mwanza ambako amejenga chumba maalum kwa ajili ya kumfikishia mganga wake toka mkoa flan anapokuja kumtembelea na kumfanyia matambiko.

kuna ajali ilitokea mwaka flan ikimhusisha pia waziri flan ziwa victoria ambako yeye na huyo aliyekuwa mwalimu walikuwa wametoka kisiwa flan kinachosifika sana kwa ushirikina katika ziwa victoria kwa ajili ya kwenda kuonana na mganga.

katika hali kama hii ya uongozi kwa nchi zetu za kiafrika ni ngumu sana kuendelea. na haitatokea nchi ikaendelea ikiwa katika nafasi ya juu kabisa ambayo ni chanzo cha maendeleo ya nchi imeshikiliwa na mtu anayeamini uchawi na ushirikina.

angalizo: hatusemi wazungu si washirikina.
 
Namba 2 inanipa shaka kidogo

Sent from my TECNO-L8 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu unayosema ni kweli kabisa.... Kabisa. Hiyo namba mbili naifaham story ilivyo. Inasikitisha san. Watu wameshawah kurogwa kwa mamilioni n wanaojiita masheikh na wachungaji kumsaidia mgombea urais mmoja mshirikina. Hata mobutu,huyo wa gambia,gadaf alikuwa mshirikina sana na arap moi pia.
 
Umeacha yule wa nchi moja ya pembe ya afrika wakati anapindua nchi haraka aliichukua pete ya kiongozi aliyempindua
 
ivi kwanin hatuna utamaduni wa kuwapa uraisi matajiri

sent from my iphone 7 nimeinunua SAPNA pale POSTA
 
ushirikina haupo kwa waafrika tu hata wachina, wahindi na wazungu pia tatizo ushirikina wa waafrika ni wakurogana wenyewe kwa wenyewe wakati wenzetu ni ushirikina wa biashara na teknolojia
 
Nasikia pia ktk nchi moja ya East, huwa wanawasha kibatari na kuzunguka nacho nchi mzima, wakiwa na msururu wa magari, eti wanamulika maadui, cha ajabu hata mchana huwashwa. Wakati huo uo wana sera ya kubana matumizi ili kufikia malengo ya nchi ya vinu.
 
Afrika kuna mizuka na mizimu kuwa ndiyo viongozi.

Ila hata wazungu koko nao ni wachawi tena wao wanasomea kabisa school.
Ndiyo nimeona South Africa kwa Madiba wameamua kuanzisha school of witches ambapo mtu au aliyehitimu grade 12 kujiunga ni lazima awe amefaulu physics, na mathematics.

Kwa hiyo, ni kawaida sana kwa Africa.
 
Hakuna cha holy book wala sacred books huu upuuzi wa wazungu koko na warabu pori kuwa ni dini ni ujinga na uchwara.

Leo hii tunaona maajabu Kwa hawa mitume na manabii Kwa kuzibeba hizo holy book ila wanatenda maovu kuliko hata mie nisiyevigusa hivyo vitabu.
Hahahah
 


Mkuu , [HASHTAG]#Kirikou[/HASHTAG] ,
Kweli mfano nikijiweka kwenye wabeba vitabu Mimi naweza nikawa Papa au Mtume S. A. W ama Yesu Kristu kabisa japo sitaweza kutundikwa msalabani na kufufuka kisha kusepa kwenda mbinguni.

Ila maovu ya wabeba vitabu na sijui shanga za kuhesabu Kwa vidole ni za kutisha.
 
Mkuu , [HASHTAG]#Kirikou[/HASHTAG] ,
Kweli mfano nikijiweka kwenye wabeba vitabu Mimi naweza nikawa Papa au Mtume S. A. W ama Yesu Kristu kabisa japo sitaweza kutundikwa msalabani na kufufuka kisha kusepa kwenda mbinguni.

Ila maovu ya wabeba vitabu na sijui shanga za kuhesabu Kwa vidole ni za kutisha.
Nakubali hoja yako,
Hawa watu wanacheza na akili zetu, kwenye mwanga wanaabudu na kusifu ila gizani wana mambo mengine
 
Ushirikina ni janga letu waafrika.

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Nakubali hoja yako,
Hawa watu wanacheza na akili zetu, kwenye mwanga wanaabudu na kusifu ila gizani wana mambo mengine

Ndiyo hivyo mkuu.

Ila ukiwaangalia Kwa haraka haraka unaona utukufu lakini ukichunguza Kwa umakini inakuwa majanga.
 
Back
Top Bottom