Viongozi wa kizungu wanawazidi hawa wa kwetu mara 110, amini msiamini, nimeshuhudia kwa macho yangu!
Wawo kiboko na wakaniteka akili kabisa kabisa, nimewakubali, sio huu wa kiafrika bana! Viongozi wa kizungu uchawi wao wa kwanza, miundo mbinu matata kabisa, pili na kuendelea, maji, umeme, afya bora, ustawi wa jamii, maendeleo ya kufa mtu, wamewamaliza kabisa wananchi wao, hawasikii wala hawaoni, hata mie nilipoenda soma kule, hilo limbwata lilinipata, nikawehuka, mpaka niliporudi na kukutana na ule uchafu JK Nyerere fahamu zote zikanirudia! Aacha kabisa na wazungu, wale kiboko aise, wana mandege, matreni kama basi, treni yaenda kasi kama ndege! Kuna mpaka treni inapita chini ya ardhi, nyie juu wala hamsikii! Shenzi kabisa wale, ukienda hata benki sio lazima foleni, mashine kutumbukiza hela, kutoa hela, kutumbukiza cheki! Hospitali napo, huna haja ya kuona receptionist, wewe wagonga tu kwenye kama kakompyuta ukutani jina na tarehe ya kuzaliwa wakaa, muda si muda jina lako latokea kwenye mkanda uko juu kama airport uende chumba gani kwa daktari! Na dawa zozote ukitaka zipo, hamwezi kuamini wala huna haja ya kutoa rushwa upate! Acha hivyo, waweza kaa nyumbani na ka laptop ukaagiza ngosha kuanzia mazagazaga yote mpaka nyama! Teksi na daladala zina barabara zake, daladala hazina konda, ni yule yule dereva, teksi napo hakuna kubishana na dereva, unaangalia mita tu walipa waenda zako, Bar hakuna kuletewa bia, waenda kaunta, ukimaliza tena, hakuna cha bill wala barmaid wa kukupandishia bill au bei za ajabu za vinywaji! Upuuzi kabisa, washirikina sana wale! Shule watoto bure mpaka chuo, huko wanapewa mikopo watakayolipa wakipata kazi, kura sio lazima eti foleni kama sisi, waweza piga home tu, waletewa kura yako wapiga unapost, shenzi kabisa wale jama kama Gambushi! Ukichelewa peleka mtoto shule pale reception wakutana tena na kama kakompyuta kako kamesimama pale kana kila sababu wajaza sababu zako unasepa mtoto anaingia darasani! Wale mafirauni eti hata nyanya za kupitisha umeme kama za kwetu juu ya ardhi hawana! Wamezichimbia chini! Hata mabomba ya maji huoni achana na ya gesi kila nyumba! Ile mizeruzeru ina Broadband karibu kila nyumba! Kama si kuwaroga wananchi ni nini?! Jamaa mvua inanyesha aise! Kama kule kwetu Shinyanga! Ila kwao yaweza piga hata masaa 12! Lakini ikikatika washangaa maji barabarani hamna! Ndorobo wale si wameweka ile mitaro yao ya kichawi ya kunyonya maji yote! Hakuna cha kukwepa mahandaki kama kwetu wala nini wana barabara nyeusi za lami kama zetu kila sehemu! Washenzi wale wanga sana, eti hata usiku wanafanya kazi, hawalali, viwandani wana shift 6-2, 2-10, 10-6! Kama sio kuwanga usiku ni nini ngosha?! Binadamu gani asiyelala kama kwetu?! Nakuapia hata fundi kabambe wa Sumbawanga hatawaweza wale! Yaani yapo mengi mpaka nimesahau ngosha, ntakuhadithia siku nyingine, sina hamu nawo, nyambafu kabisa wale...
Na sirudi tena ng'o, uchawi gani ule?! Nina bahati kweli ngosha, kidogo niwe MSUKULE WAO!