Marais wa nchi wazuiwe kisheria kuropoka kwenye mitandao ya kijamii

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
10,509
Reaction score
16,734
Dunia inakwenda kwa kasi sana kuelekea inakoelekea dalili zikiwa ni wepesi wa mawasiliano baina ya mtu na mtu na kwa jamii kwa ujumla.

Katika miaka ya karibuni tumeshuhudia viongozi wakuu wa nchi wakizungumza mambo mazito ya nchi kwa umma bila kizuizi chochote kile.Kuna mambo mazito ya nchi yangehitaji kupitia washauri wao maalum au kupata kibali cha mabunge na mabaraza yao ya utawala.

Mambo hayo yamekuwa yakifanywa na viongozi wa mataifa madogo na makubwa.Raisi Trump ni mmoja wa mfano wa matumizi mabaya ya mitandao kuzungumzia mambo nyeti ya nchi.

Mara nyingi Trump amekuwa akitumia mtandao wake wa kijamii kujibishana na watu wadogo na viongozi wengine wa nchi. Ni kawaida kumsikia akipeana mipasho na Medvdev wa Urusi au na hata wale viruka njia aliokuwa nao miaka ya nyuma.

Hali hiyo kwa upande mmoja inatoa siri muhimu za nchi na kuhatarisha usalama wa nchi na hata kupelekea taifa kubwa kushuka kwa heshima yake pakubwa. Harakati na matamko ya Trump inawezekana ilichangia pakubwa kushindwa kwa jaribio lake la kuvunja vinu vya nyuklia vya Iran.

Pamoja na ukweli kuwa vinu hivyo havifikiwa na makombora iliyonayo Marekani lakini pia kwa umakini mkubwa wairan walishajua kuwa Trump anakuja na ndipo wakahamisha mitambo muhimu iliyokwisharutubishwa Uranium ikapelekea Doomsday aircraft kutifua vumbi tu kwenye malango ya vinu hivyo na njia zinazovizunguka.

Trump alipokanusha kupitia mtandao wake wa kijamii maneno ya mkurugenzi wa Pentagon kwamba Iran haikuwa na bomu la nyuklia na kwamba mradi wake ni wa kiraia hiyo ilitosha kuonesha anakusudia kupiga tu ili kupata sifa.

Siku 12 alizozitoa Trump kwa nafsi yake kwa Putin kwamba akubali kusitisha vita au atapokea kipigo zitapuuzwa na zitapita bila kufanya chochote.Itaonesha udhaifu tu wa Marekani na wala haitaisaidia kuwa kubwa kwa mara nyengine.

Kama raisi Samia angejibishana na Paul Kagame kuhusiana na mzozo wa DRC basi vita vingekwishazuka baina ya Rwanda na Tanzania.

Mwisho wa indari yangu kwa matumizi ya mitandao ya kijamii ni kuwa maraisi waruhusiwe kutoa salamu za pole basi kwa wafiwa na si zaidi ya hapo.
 
Medvdev tu ndiye mwenye uwezo mkubwa wa kumpasha /kumbumbusha Trump kwamba Trump na Amerika wasijichukulie/kujiona kwamba wao ndiyo Miungu ya Dunia, Medvedev akamkubusha tena Trump kuhusu deadman's hand kwamba hiko still alive and kicking, sijui hata kama Trump alishawahi kusikia term kama hiyo - yupo yupo tu kazi kukwaruzana kwaruzana na
watu au Nchi ambazo hazikubaliani na matakwa yake ya kuwa wabulldoze watu/mataifa - MAGA hisiwe mantra ya kulazimisha Dunia ifuate matakwa ya aidha Amerika au Trump mwenyewe au kutumia hila za kupora mali asili ya Mataifa maskini.
 
Back
Top Bottom