Marais waondolewe tu na tusiwe na vyama kwani vinatugawa...

Marais waondolewe tu na tusiwe na vyama kwani vinatugawa...

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,669
Reaction score
33,691
Habari wanajamvi,

Upinzani haupewi nafasi nchini. Kama awamu hii ya tano, bora hata zilizopita. KIla siku viongozi wa upinzani wamekua wakipelekwa police.

Hii ikafanya wasi concetrate na maendeleo ya majimbo yao. Yes, nitajie mbunge gani wa upinzani ambaye hajapata ghasia za police awamu hii ya tano?

Wengi wakaishia kuwa passive. Na wengine kuona bora wakimbilie CCM labda ndio wata feel secured.

Worse Mr President , anatamka wazi wazi ' msiwabomolee hawa ni wapiga kura wangu' na ' Msipomchagua fulani (CCM) hamtapata maendeleo'

Sasa hii itawapa 'motisha' kweli hawa viongozi wa upinzani? Halafu mnasema kuna fair election. Under such climate, how can we have fair representation?

Second ni selfish, amewanyima haki wananchi kufuatilia viongozi wao kwa kukataza Mihadhara na open dialogue/debate. Sasa which young political party will flourish under such environment?

I mean HOW?

Hivi na huko ulimwenguni mambo ni kama haya? CCM inashinda si kwa sababu ina sera nzuri bali ni kwa kukandamiza upinzani.

Mimi naona tuwatoe Marais kama viongozi wetu. Tubaki na Waziri Mkuu anayesimamia mawaziri na wabunge.

Huyo Waziri Mkuu asiwe wa chama chohote. Na wabunge na mawaziri wasiwe chama chochote. Namaanisha tusiwe na Chama!

Vyama vinatugawa, na sio fair.

Imagine hotuba za Rais ni nimetengeneza barabara hii, flyover hii. Halafu Lissu anakuwepo na sera ambazo hazijawa tried/ahadi.

Jamani hata kama Lissu angekua na sera zipi bado ingekua ngumu(Makamanda msinichukie).ila ni kweli wote hawaanzii level moja.

Sio fair kabisaaa! Tusipokua na vyama, itakua poa sana. Mawaziri na Wabunge wapatikane kama kazi nyingine zinavyotangazwa, na mtu competent ndio anapata kazi. Akiboronga anatolewa.

Hatusubiri mpaka miaka mitano au kumi ili tumtoe mtu ofisini.

Kama sasa hivi unaona kabisa kuna upendeleo. Pesa zinatolewa bila idhini ya bunge and the person will be in the office for ten years.

Pathetic
 
Kuna mtu namsubiri mzee wa kuropoka bila kutumia ubongo..... Ndio ni comment kwenye huu uzi.....
 
Popote kwenye ulaji hakuna haki. Cha muhimu ni kukata mishahara na posho zisizo na kichwa wala miguu wanazomwagiwa kwa kupitia madaraka yao.
 
Marais wasiwepo tu kwa kweli, uonevu ni wa waziwazi
 
Back
Top Bottom