Marais Wastaafu wa Tanzania, wajengewa nyumba na Serikali

Ukiwa na akili sana na mtu wa reasoning kwenye nchi za Africa utaumia tu na kupata msongo wa mawazo.
 
Masamaki mtumishi tu wa TRA alikuwa na kesi ya kumiliki nyumba 70+ huyu ni muajiriwa pata picha mwajiri wake.
Mkuu cheo cha Rais ni habari nyingine kisikie tu hivyo hivyo. Anaweza kusema wote mnaochimba Tanzanite muondoke ili nichimbe mimi na hakuna wa kuhoji.
 
Na mwinyi amestaafu 1995, nyumba anakabidhiwa leo !!!

..sasa jiulizeni tangu 1995 alikuwa anaishi wapi?

..je, serikali haikumsaidia kumpatia makaazi?

NB:

..Mzee Mwinyi ameoa wake wawili.

..Hivyo alipokuwa Raisi alipewa nyumba Ikulu, ni nyingine mtaa wa Laibon Oysterbay.

..kwa uelewa wangu alipostaafu mwaka 1995 alihama Ikulu, lakini aliendelea kutumia nyumba ya mtaa wa Laibon.
 





Rais JPM amemkabidhi Rais Mwinyi nyumba na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ya Rais Kikwete, hisani ya serikali ya Tanzania.

Ungetegemea kipindi cha uchaguzi ni muda wa kujikita na mambo ya wananchi. Lakini cha ajabu siku kumi kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi Rais pamoja na wastaafu Urais wanathubutu kuwa na ratiba za kukabidhiana nyumba walizojengewa na serikali.

Wanasiasa gani hawa wabovu hawaoni kuna picha mbaya, bad optics, katikati ya kampeni za kuongelea masuala ya wananchi wao wanakabidhiana nyumba za serikali? Mambo ya manufaa yao binafsi? Kwa nini Waafrika tumelaaniwa kupata viongozi wabovu wasiotujali?

Na kibaya zaidi, walivyo waroho wa mali na jasho la wananchi, hawa wote tayari walishapewa nyumba za serikali tayari. Mwinyi alipewa nyumba ya serikali mtaa wa Laibon, Oyterbay, D'salaam miaka 30 imepita yumo humo, na Kikwete nae hivyo hivyo ana nyumba iliyokuwa ya serikali Mikocheni, D'Salaam. There is no way eti Rais wa Afrika akawa hakupewa nyumba wakati akiwa Rais. Kwa hiyo hizi mpya ni za ziada tu. Kulikuwa na haja gani ya kuwapa nyumba nyingine, hawashibi? Hivi kwa nini wao ndio wanajiona binadamu muhimu kuliko raia wengine?

Kichefuchefu zaidi ni pale Kikwete anapojifanya anaweza kungojea kupokea ya kwake ikikamilika kwa sababu eti alipopanga sasa hivi hajafukuzwa. Eti kapanga!

Wanatufanya sisi wajingaaaaaaaaa! Wanajua vast majority ya wananchi sisi ni wauza masinia ya ndizi na mayai na wasukuma boda boda, kwa hiyo hatujasoma, hatuwezi kuchambua lolote, kwa hiyo wanaweza kufanya lolote. Hawana hata hekima za kula na kipofu bila kumshika mkono, wanafanya wazi wazi katikati ya uchaguzi. Uzalendo sifuri, binadamu dhalimu kupita maelezo.
 
Na kesho mama akampe JK marcedez yake nayeye maana tayari mijengo washajengewa...
 
Tatizo la nchi maskini ni kuwa na wanasiasa wanyonya damu,
Wanaona ufaharj,na wanataka wananchi washangilie pale wanapokuwa wanaishi vzr,na kupeana huduma za Daraja la kwanza,wanatuaminisha kwamba nchi ina deni nao lazima iwahudumie,kama vile mpaka hapo walipo walikuwa hawahudumiwi.
Basi ni bora wangejipa hizo mali kimya kimya,kuriko alivyofanya huyu mama,
Juzi katoka kuwaambia wafanyakazi nchi haina pesa ya kuwaongezea mishahara leo anachukua pesa na Malj ya umma anagawa kama njugu tu,kama vile ni msahafu kwamba hawa wastaafu lazima wapewe mahekalu,mahekalu ambayo hawatakaa,wataishia kuyapangisha na siku wakifa watoto wao,ambao wengine ni Maraisi,wabunge,watayatumia mpaka wafe
 
Tanzania nchi ya ajabu sana kila kiongozii akiingia anafanyaa anavyoona yeye itakavyokuwa sawa kwanini isiwe hivi kujenga mifumo imara kama tulianza na na gesi tungehakikasha mikoa yote kuna plant za kusindika kesi ndio tuhamie na miradi mingine tunahakikasha mradi unakalimilika siyo gesi mara sgr mara stiegers Mirandi haiishi tuhamie miradi mingine hatutafika kama ni barabara tujenge zote tuhamie miradi mingine lakini kila raisi anafanya kile anachoona yeye pia tungejenge specialized hospital kila mkoa wakitoka kwenye madaraka wanajutia hata siwaelewi wasomi tunao chukua mia wape mitaji wafanye kazi

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Sasa hivi nmeona unaunga mkono ili kumkomoa marehemu
Kuunga mkono siyo kwamba yote atakayofanya unayemuunga mkono yatakua sahihi hivyo kwamba uyaunge mkono. Hata waliomuunga mkono JPM (wanaojitambua) hawakuafikiana na yote aliyoyafanya. Hawa watu ni wanadamu kama mwanadamu yeyote, hawawezi wakafanya yote sahihi kama malaika. Mlimtukuza mno JPM kama vile hakuna makosa aliyofanya. Haya mapenzi anayopewa mama na watanzania wote bila kujali tofauti zao za itikadi, ni matokeo ya uongozi uliopita.
 
Huu ni wizi wa pesa za walipa kodi na lazima tuukemee kwa nguvu zote. Upuuzi kama huu huusikii katika Nchi zilizoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…