KUTATABHETAKULE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 5,159
- 5,070
Maana yake ni kwamba aliye nacho ataongezewa, asiye nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alichonacho. Wote tuseme Amina.Maana yake nini
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Maana yake ni kwamba aliye nacho ataongezewa, asiye nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alichonacho. Wote tuseme Amina.Maana yake nini
Ukiwa na akili sana na mtu wa reasoning kwenye nchi za Africa utaumia tu na kupata msongo wa mawazo.Kweli aliyeshiba hamjari mwenye njaa,
Kulikuwa na umuhimu gani Tena kipindi hiki,kuwajengea Hawa nyumba,Hawa watu wanaukwasi mkubwa sana,ukiacha mali walizonazo,na walizoiba.
Ktk nchi maskini unatumia pesa kuwajengea nyumba maraisi,ambao kwa viwango tu vya kimataifa ni matajiri sana.
Hizi pesa zingetumika kulipia mikopo ya vijana waliomaliza Elimu ya juu,ingekuwa poa sana.
Timing imekuwa mbaya sana,wananchi wameuliwa na magaidi mtwara,Dar viongozi wanaongezeana ukwasi.
Kwanza hizi pesa zimetoka wapi,zimeidhinishwa n
Kuna kitu huwa najiuliza sana lakini sipati jibu! Je hivi ni kweli marais wetu na mawaziri wetu wakuu kwa mishahara mikubwa na posho nono za mfululizo wanazolipwa wawapo madarakani, ikiwemo kununuliwa na serikali mahtaji ya kila siku mpaka nguo za mwilini na mashuka ya kulalia, Pia kiinua mngongo cha kutosha na bado anaendelea kuvuta pesheni ya 80% ya mshahara wa yule aliyeko madarakani, Hivi kweli ni mtu wa kushindwa kujenga nyumba kama hiyo???? Hizi nyumba si bora wangekuwa wanajengewa wastafu wa kada za kawaida kama walimu au manesi??? Maana hawa hata mshahara wao na mafao yao ni mgogoro wa mgogoro! Pensheni wanazolipwa kila mwisho wa mwezi utaona huruma!
Naombea Mungu tufike mahala tupate kiongozi mwenye maono tofauti, atakayeweza kuona kundi halisi lenye uhitaji wa mafao hayo!
Sina kumbukumbuAlivyopelekwa St Thomas Hospital Uingereza aliondokea Butiama au Mikocheni?
Na mwinyi amestaafu 1995, nyumba anakabidhiwa leo !!!
Akapewe tu kila kitu, maana anaonekana ni zaidi ya Mtanzaniamnalalamika leo MWNYI kupewa Benz?
Wapuz kweli...wanalalamika garimnalalamika leo MWNYI kupewa Benz?
Tatizo la nchi maskini ni kuwa na wanasiasa wanyonya damu,
Rais JPM amemkabidhi Rais Mwinyi nyumba na kukagua maendeleo ya ujenzi wa ya Rais Kikwete, hisani ya serikali ya Tanzania.
Ungetegemea kipindi cha uchaguzi ni muda wa kujikita na mambo ya wananchi. Lakini cha ajabu siku kumi kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi Rais pamoja na wastaafu Urais wanathubutu kuwa na ratiba za kukabidhiana nyumba walizojengewa na serikali.
Wanasiasa gani hawa wabovu hawaoni kuna picha mbaya, bad optics, katikati ya kampeni za kuongelea masuala ya wananchi wao wanakabidhiana nyumba za serikali? Mambo ya manufaa yao binafsi? Kwa nini Waafrika tumelaaniwa kupata viongozi wabovu wasiotujali?
Na kibaya zaidi, walivyo waroho wa mali na jasho la wananchi, hawa wote tayari walishapewa nyumba za serikali tayari. Mwinyi alipewa nyumba ya serikali mtaa wa Laibon, Oyterbay, D'salaam miaka 30 imepita yumo humo, na Kikwete nae hivyo hivyo ana nyumba iliyokuwa ya serikali Mikocheni, D'Salaam. There is no way eti Rais wa Afrika akawa hakupewa nyumba wakati akiwa Rais. Kwa hiyo hizi mpya ni za ziada tu. Kulikuwa na haja gani ya kuwapa nyumba nyingine, hawashibi? Hivi kwa nini wao ndio wanajiona binadamu muhimu kuliko raia wengine?
Kichefuchefu zaidi ni pale Kikwete anapojifanya anaweza kungojea kupokea ya kwake ikikamilika kwa sababu eti alipopanga sasa hivi hajafukuzwa. Eti kapanga!
Wanatufanya sisi wajingaaaaaaaaa! Wanajua vast majority ya wananchi sisi ni wauza masinia ya ndizi na mayai na wasukuma boda boda, kwa hiyo hatujasoma, hatuwezi kuchambua lolote, kwa hiyo wanaweza kufanya lolote. Hawana hata hekima za kula na kipofu bila kumshika mkono, wanafanya wazi wazi katikati ya uchaguzi. Uzalendo sifuri, binadamu dhalimu kupita maelezo.
Mkuu tunaangalia "kagari" hayo majumba haikuwa issue kubwa maana tulizibwa midomo!!! 😀 😀View attachment 1603958
Raisi mstaafu awamu ya pili akikabidhiwa nyumba aliyojengewa na serikali Masaki Dar Es Salaam
View attachment 1603960
Muheshimiwa Magufuli akikagua ujenzi wa nyumba ya raisi mstaafu awamu ya nne anayojengewa na serikali Kawe beach Dar Es Salaam
Hili wengi wanalikalia kimya kana kwamba halipo!!Ipo kisheria kama wengine wanavyopewa magari baada ya kustaafu
Mkuu mbona walishajenga kitambo au ulikuwa ughaibuni wakati huo?Wangejenga butiama
Sasa hivi nmeona unaunga mkono ili kumkomoa marehemuBora wangejenga zahanati ikasaidia wananchi. Mzee Mwinyi tayari ana nyumba yake binafsi.
Kuunga mkono siyo kwamba yote atakayofanya unayemuunga mkono yatakua sahihi hivyo kwamba uyaunge mkono. Hata waliomuunga mkono JPM (wanaojitambua) hawakuafikiana na yote aliyoyafanya. Hawa watu ni wanadamu kama mwanadamu yeyote, hawawezi wakafanya yote sahihi kama malaika. Mlimtukuza mno JPM kama vile hakuna makosa aliyofanya. Haya mapenzi anayopewa mama na watanzania wote bila kujali tofauti zao za itikadi, ni matokeo ya uongozi uliopita.Sasa hivi nmeona unaunga mkono ili kumkomoa marehemu
Sasa hivi nmeona unaunga mkono ili kumkomoa marehemu
Ungekuwa wewe ni Rais mstaafu,ukajengewa hiyo nyumba na kupewa..je,ungekataa?Huu ni wixzi wa pesa za walipa kodi na lazima tuukemee kwa nguvu zote. Upuuzi kama huu huusikii katika Nchi zilizoendelea.