Marais Wastaafu wa Tanzania, wajengewa nyumba na Serikali

Dah, jamaa anatafuta justification ya mambo fulani fulani kwa kila njia.

Ndio maana kwa jeuri alimtuma JK kwenye kampeni yake Mbagala jana.

Eti ni Rais wa wanyonge, Hivi marais wastaafu wenye ukwasi na marupurupu kibao ni wa kujengewa nyumba na serikali wakati kuna watu wanateseka kwa njaa mitaani, watu hawana maji ya kunywa mijini na vijijini? JK na Mwinyi wana shida hiyo kweli?
 
Kumbe umekumbuka hongera Magufuli. Ndio dunia hiyo Mzee wangu. Hongera
 
Huu ni ubadhirifu na matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Hawa marais wakiwa madarakani wanakuwa wameisha kukusanyia pesa za kutosha na kujijengea mahekalu mengi. Maana mwinyi na Kikwete wanamiliki vijiji vyao.
Hii nyumba aliyokabidhiwa mwinyi ina thamani ya zaidi ya shilingi bilion saba kwa makisio ya awali.
Sasa fikiria mzee wa miaka 95 anajengewa nyumba yenye thamani hiyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…