Mchumia Rungu
JF-Expert Member
- Apr 26, 2013
- 1,438
- 826
ndugu zangu wanazuoni
kutokana na hali tete ya kupata pesa za field na kwa ukimya wa marais wa
vyuo vikuu pamoja na TAHLISO napenda kutoa wazo ya kuwa mwezi wa kumi
tukifungua vyuo vyote Tanzania tunaomba marais wajipime na wajiuzulu
kabla ya nguvu ya umma haijaamua....Kweli hawa jamaa wameshindwa
kuitisha hata press conference na kutuma altumatum kwa
government.....NAOMBA WANAHARAKATI WA VYUO VYOTE TUSHIRIKIANE
KUHAKIKISHA TUNAWATOA WATU HAWA....KATIKA HILI SITARUDI NYUMA NA NIPO
TAYARI KUFA NIKISIMAMIA HILI....
Naomba mnipm ili tujue tunafanyeje na tunaorganize vp mapinduzi haya...
Wenu katika harakati za ujenzi wa taifa letu...
Nashukuru kwa kuniita mjinga...nazani ww ni mmoja wa viongozi ambao itabidi watolewe....
Hoja ni pesa za kufanya wazalendo hawa walioamua kwenda kutumikia taifa japo pesa haikutoka lakini wakaenda wakiamini viongozi wataishinikiza serikali itoe pesa lakini viongozi hao wamejifungia ndani wakifurahia pesa za wanafunzi na kupita kujivunia kuwa wao maraisi....tucta huwa hawakai kimya linapokuja swala la mishahara je,hao nao hawatangulizi uzalendo!? Wahadhiri chuo kikuu cha Dar es salaam wakati fulani walitishia kugoma wakidai haki,je hao nao hawakuwa wazalendo....UDOM wahadhiri walitishia kugoma je hao hawakuwa wazalendo?!..
Uzalendo kwako nini?
Hapa tunaongelea ukimya wa Tahliso na viongozi wa wanafunzi vyuo vikuu......nakuahidi nitaengeneer mapinduzi haya na nyinyi nyote mtapigwa chini...
Tunataka viongozi watakaoweza fanya maamuzi magumu......
Mkuki kwa nguruwe eeh!
Labda nikukumbushe kiongozi wangu.....mimi sina siku nying hapa JF, nimejiunga juzijuzi tu ...yaani 2008...... toka wakati huo mpaka leo sijawahi kumuita mtu awaye yote mjinga ama neno linalofanana na hilo!
Mungu wangu ninayemwamini amenikataza kutukana, bali nitumie busara kuwatendea wema wengine.....tazama mkuu, unaposema yaliyoujaza moyo wako siyo yaliyoujaza wangu..... wewe ulinijibu kuwa NAFIKIRI UJINGA, japo ndipo fikra zangu zilipogota.....KUKIRI UJINGA. kutokana na maandishi yako ya awali kiongozi wa kuwatoa viongozi nakwambia hivii hutofanikiwa....
Dahhh ni changamoto mwakweli maisha magumu sana mtaani
Unapolazimisha step two kabla ya step one hapo ndipo ninaposhangaa...... je nani kawaambia pesa ya field hakuna? Je vidonda vya uchaguzi uliopita haujapona tu? Unaposhindwa kwenye chaguzi ungana na aliyekushinda kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii, kuendeleza vijiharakati visivyo na procedure si njia muafaka.....
Tuone kwamba psa za field hakuna, tuone kwamba jitihada kadhaa zimefanyika na hakuna mafanikio....hapo hata jamii itatuelewa, sasa hakuna kilichofanyika sisi tukurupuke tu ....halafu sisi ndo wasomi, wapanga mikakati wa kesho kwenye jamii......:sleepy:
Kwanza wewe unaonekana huna hata elements za uana harakati. Katafute wanaharakati wakuambie aharakati zinafanywaje.
Pili unaonekana unasoma vyuo vya uswahilini kama Datastar au Global training.
Udsm, Udom, Saut, Ardhi haina watu kwama wewe.