Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Katika awamu ya kwanza ya marathon ya roboto ya mwaka jana, roboti ziliendeshwa na watu kutokea mbali, na robot bingwa ilimaliza kwa saa 2 na dakika 40, zaidi ya mara mbili ya muda wa binadamu.
Lakini mwaka huu, hali imebadilika. Roboti yenye urefu wa mita 1.69 inayoitwa “Mwali wa Radi” ilimalizia kwa dakika 50 na sekunde 26. Hiyo ina maana gani? Katika Mbio za Lisbon za Nusu Marathon zilizofanyika mwezi Machi, mwaka huu, mkimbiaji wa Uganda Jacob Kiplimo alitumia muda wa dakika 57 na sekunde 20, akiweka rekodi mpya ya dunia. Hii ina maana kwamba roboti zimewashinda binadamu katika mbio za marathon.
Hili sio jambo pekee la kushangaza. Mbio za mwaka jana zilikuwa na timu 20 tu zilizoshiriki, mwaka huu, idadi hiyo iliongezeka hadi zaidi ya timu 100 kutoka mikoa 11 nchini China, na hata kampuni za teknolojia za kigeni zilituma timu 5. Muhimu zaidi, karibu asilimia 40 ya roboti hazihitaji tena udhibiti wa mbali wa binadamu. Zimekimbia kwa kujitegemea na kuamua njia yao zenyewe, yaani zimeanza kuwa na “akili”.
Bila shaka hatuwezi kuangalia tu mambo mazuri. Bado zaidi ya nusu ya roboti zilishindwa kumaliza mbio. Baadhi yao “ziliharibika” katikati, nyingine zilipotea njia, na nyingine “zilianguka tu” na kushinda kusimama tena. Hii inaonesha kwamba teknolojia hiyo haijakamilika.
Watazamaji wengi wa mbio hizo wana shaka kuhusu madhumuni ya kufunza roboti kukimbia.
Ukweli ni kwamba, madhumuni ya kufunza roboti kukimbia mbio za marathon si kwa ajili ya kujua ipi inaweza kukimbia kasi zaidi, ni kufahamu dosari za roboti ili kuzirekebisha na kuzikamilisha. Mchezaji akishiriki kwenye mchezo lazima afanye maandalizi kwanza, na mbio hizi ndiyo maandalizi kwa ajili ya siku za baadaye.
Wakati siku moja “wakimbiaji wa chuma” wanaonekana katika mitaa wakipeleka vifurushi, wakiandamana na wazee katika korido za hospitali, na kutafuta manusura katika magofu ya moto, tukiangalia nyuma mbio hizo za marathon, unaweza kusema, “Kumbe, yote yameanza zilipojifunza kukimbia na kutoanguka.”