March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

uchaguzi umeisha.. turudi... kwenye.forum zingine tukachangie hoja ... ntarudi humu odinga akikubaliwa pingamizi lake mahakamani so far nimesurrender.. ila bila kupindisha maneno hawa jamaa wakabila aisee ..demokrasia bana..
 

mmmh! mi nasubiri mpaka tume itangaze, sasa hivi story kutoka citizen tv ni kwamba kuna matokeo kutoka sehemu 11 ambayo hayakujumuishwa kwenye yale matokeo yaliyotangazwa kwa luninga....hao tume wanaweza wakapanda hapo jukwaani na suprising news, time will tell....SIASA NI MCHEZO MCHAFU
 

Mkuu hiyo hakuna nusu mtu. Hiyo nukta tano ondoa kwenye conclusion. Wenye fani wakiiona wanaweza kuzimia
 
Tatizo hawa watu hawajui tofauti ya absolute value na relative value, usiwalaumu hesabu zilikuwa zinakimbiza watu wengi sana madarasani, kwa nini hawajiulizi kama hiyo 1 ni %age kwa nini zisiandikwe pamoja yaani 51% badala ya 50%+1.

uzuri zaidi citizen walikuwa wanaandika Uhuru surpasses 50% plus one mark
 
Siwezi kabisa kuondoka katika uzi huu bila kuwaa na kupeleka SHUKRANI zangu na pole nyingi kwa Kenyan kwa kazi kubwa japo muda wote niliokuwa kwenye uzi huu pia nilikuwa napata matangazo ya moja kwa moja kupitie the Citizen na NTV.
Pia pongezi kwa Tiba kwa ufafanuzi na uchambuzi murua wa mara kwa mara aliokuwa akiutoa ambao kwa wengi uligeuka shule.
Waliochangia kunogesha uzi huu ni wengi lakini naomba niwataje wawili hao.
Nitarudi tena na tena kwenye uzi huu, kwa sasa najiandaa kwenda Nairobi kuhudhuria kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta.
Ahsanteni.
 
Last edited by a moderator:


Hii Kwa upande wangu naona ni sawa kabisa maana Odm wametoka kiupya na madai kuwa kura za majimbo 11 hazijajumuishwa kwenye jumla ya kura zao hivyo imemlazimu kuanza kupitia upya pamoja na mawakala ili kumaliza ile utata unaoweza kujitokeza maana jamaa ndio hapohapo atapata sababu ya kwenye mahakani kwamba alikuwa nahoja na tume hawakumsikiliza
 

Mkuu, naungana na wewe kumshukuru mwana JF Kenyan kwanza kwa kuanzisha uzi huu, pili kwa kuendelea kutupa update kila zilipokuwa zinapatikana. Mkuu Consigliere naomba nikushukuru kwa kuutambua mchango wangu kwenye huu uzi. Nitakuwa njiani kurudi Dar kesho alfajiri baada ya kumaliza kazi hapa.

Tiba
 
Kuanzia sasa Uhuru Kenyatta ni kiumbe tofauti kabisa kwani hata hapa BOMAs ameingia kwa ulinzi mkali kupita kiasi. The man in Power soon!!!

Tiba
 
Amepata kura ngapi jumla???

nani maana kama ni UHURU angalia hapo juu utaona

Uhuru Kenyatta - TNA: 6,173,433 [50.03%]
Raila Odinga - ODM: 5,340,546 [43.28%]

Total Vote cast - 12,338,667

291 out of 291 Constituencies results
 
Mkamap BBC wanasema amepata 50.07% ina maana kuna kura za ziada zimeongezeka!

Ni kweli nafikiri ni calculation tu, hiyo % hapo juu ilikuwa estimated, lakini ya uhakika ni 50.07% baada ya kuzihesabu zilizo harabika.
 
Halafa nashangaa watu wanapiga kelele eti siasa za Kenya zimejaa ukabila,waulize kina Dr. Salim,Malecela,Zitto,Dr Slaa
SIASA NI MCHEZO MCHAFU UKIINGIA HUKO JIANDAE KWA LOLOTE LITAKALOKUTOKEA
Haijalishi ni China,Urussi,France,US,Brazil,South Africa
tatizo jf na watz hawajui lolote nikiwaita jina size yao hawapendi
 


Mkuu shukran zikufikie popote pote ulipo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…