March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

Sasa naanza kuelewa kwanini RAILA anapata wasiwasi na utangazaji huu! Kenyatta kamaliza anga zake sasa wanapata kigugumizi kutangaza kwa Odinga.
 
Lakini ukweli unabakia kuwa 42.40% ni ya waliojiandikisha.
 
hivi mnachosubiria sasa kwenye hili jukwaa ni nini kama sio umbea tu uliobaki,matokeo ya uchaguzi uliokithiri UKABILA (TRIBALISM) wa kupindukia yanaonesha wazi kwamba Uhuru Kenyatta amekuwa rais wa ukabila Kenya,tusubiri nasi Tanzania 2015 wengi wakihitaka rais awe mkristo,pumbavu kabisa unaenda kupiga kura wakati rais ameshaandaliwa IT'S BETTER TO HAVE DICTATORSHIP REGIME
 
Tulisema sana hii kitu tukaambiwa eti sisi ni 'Analogue' wao ni 'Digital'...leo punda kagoma mzigo!

Kwakweli matatizo yaliyojitokeza ni ya kishamba na kijinga. Tatizo kama mashine kuwa hazicharge battery haliwezi kueleweka. Vituo vingine clerks wanaingiza password mashine inasema password not accepted!!!
 
Tume iwe makini sasa ili kuinusuru kenya ili yasitokee yale ya 2007
 
Kikundi cha watu wenye silaha kimeteka nyara vituo viwili vya kupigia kura huko Garissa Kaskazini mwa Kenya karibu mwa mpaka wake na Somalia.

Vilevile imeelezwa kuwa watu wapatao 19 wameuawa katika matukio mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi.

Chanzo: Gazeti la Metro 5.3.13

View attachment 85678
 
Kwakweli matatizo yaliyojitokeza ni ya kishamba na kijinga. Tatizo kama mashine kuwa hazicharge battery haliwezi kueleweka. Vituo vingine clerks wanaingiza password mashine inasema password not accepted!!!

Sasa katika mazingira kama haya,naiona kabisa possibility ya kumanipulate matokeo especially watakapoamua kutally manually,kweli Africa bado sana maswala ya Tech basi tu kung'ang'ana na vitu ambavyo hatuna uwezo navyo!
 
Rudia kusoma maelezo ya tiba uelimike

Yawezekana anacholisema Tiba ni sahihi lakini ukweli ni kwamba kura hazijaisha kuhesabiwa kwa hiyo sio rahisi kujua idadi ya watu waliopiga na kama wameshajua idadi ya waliopiga toka jana kazi ingekuwa imeshaisha maana hizo percentage toka jana zinatolewa kwa maana hiyo kama unakubali maelezo ya Tiba kwamba idadi ya waliopiga inajulikana obvious kwa muda wote huo hata kura za mmoja mmoja zingekuwa zishajulikana na kazi ingekuwa imeshaisha.
 
Huu ndio mchezo wa nchi zetu za Afrika hata hivyo tusubiri tuone matunda ya tume jhuru ya uchaguzi Kenya
 
Matokeo yalivyo kwa sasa saa 4 kamili usiku leo tarehe 5/3/2013

Uhuru - 2,778,403 - 53.38%
Raila - 2,188,301 - 42.04%

Tiba
 
Hawa sasa wanatafuta watu wauane. Wafuasi wataanza kujitangazia matokeo yao na matokeo rasimi yakitangazwa na kuwa tofauti na ya kwao hapo ndo ngumi zinaanza.
 
Sasa katika mazingira kama haya,naiona kabisa possibility ya kumanipulate matokeo especially watakapoamua kutally manually,kweli Africa bado sana maswala ya Tech basi tu kung'ang'ana na vitu ambavyo hatuna uwezo navyo!

Ndio kilichofanyika. Baada ya IEBC kupewa report ya hizo failures ikatoa ruhusa kwa wasimamizi kutumia hard copies kuidentify voters. Wanasema walikuwa na hard copies ready just in case. Halafu mtandao ukaenda down for 6 hours kwa hiyo kukawa hakuna mawasiliano kati ya IEBC na vituo kwa muda huo kupitia mtandao uliowekwa. Mimi sio mtaalam wa IT lakini kwa kutumia common sense mojawapo ya sababu ya mitandao kuwa chini marekebisho kufanyika, sasa hapa tunaweza kujiuliza kuna marekebisho gani yalikuwa yanafanyika?
 
Watu tayari wana querries ila hawawezi kuziraise publicly at this moment kwa sababu wanajua likitokea la kutokea maneno yao yanaweza kuwa tiketi ya ICC...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…