March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

2007 machafuko yale ya Kenya yana mkono wa CCM, nashangaa kwanini mahakama ya ICC hawakuliona hilo, ya mwaka huu pia yana mkono wa hawa majangili.

wazungu wenyewe ndiyo hawa wanaobeba madini bwelele watawafungulia kesi kweli? mpaka siku tuwaondoe madarakani ndiyo watawageuka..
 
jamani mnaofatilia inamaana hakuna update tena au nianze kusherekea...
 
Kwa vipi zitaitumbukiza Kenya matatani kama member amepost hapa ili tupate picha ya kinachoenda kutokea? Au uko tayari kuangusha varangati kwa sababu ya uchaguzi wa Kenya?
LATEST NEWSKenyatta 2,978,119Raila 2,756,551WAPENZI WATAZAMAJI MCHUANO NI MKALI KABISA
 

Kama ni kweli, je huyo engineer akishitakiwa kwa uhaini litakuwa ni kumuonea au vipi?? Mimi ninaunga moono akamatwe ashitakiwe kwani alikuwa anataka kuleta maafa makubwa Kenya!!!
 
Msomali A.K amemdanganya huyo Engineer kuchakachua matokeo, imekula kwake-atajuta kufanyiakazi ushauri wa Jangiri la Meno ya Tembo!

Taratibu mkuu maana hata Boss wa tume ya uchaguzi na mipaka umemwangaia vizuri na kuweza kutambua asili yake? HAINA ROLE katika yanayotokea jamani! Wacha tusiwe na mawazo hasi; kama mfumo mpya katika Katiba mpya wanaufuata yote yatakuwa sawa
 
Nawapongeza sana tume ya uchaguzi hapo Kenya!

Wahakikishe haki inatendeka!
 
Nadhani bila ya kuwa makini na tume ya uchaguzi, vyama pekee havitaweza kusimamia matokeo yao. Cha msingi na sisi (TZ) kuunda tume huru na yenye lengo la kulinda maslahi ya nchi. La sivyo maana halisi ya kupiga kura itapotea..

Hiki ni kichekesho Tanzania kuunda tume huru? tangu lini. Tuna rundo la kesi tumeshindwa kufanya hizo tume. Tuliangalie suala hili upesi na lifanyiwe kazi. 2015 si mbali
 
Digitali inaposuasua kuliko analogia hapo ndipo mambo yanapoharibikia.

Hivi inawezekana ujio wa Uhuru na Kibaki nchini mwetu wakati wanaelekea katika uchaguzi walikuwa wanakuja kukamilisha mafunzo ya uchakachuaji wa kura!

Hii mamual work inauwezekano mkubwa ikapeleka maangamizi katika kambi ya jubilee!
 
mary mary nakwambia tukipata tume huru kama hii hakika itapendeza sana kwa nchi yetu! 2015 mi natamani iwe tarehe ya kesho.


Hiki ni kichekesho Tanzania kuunda tume huru? tangu lini. Tuna rundo la kesi tumeshindwa kufanya hizo tume, ghalfa tukawaundie wengine?
 
Last edited by a moderator:
Kamanda nadhani uko nyuma na matangazo. Yale matokeo tulokua tukipata awali yalikua manipulated.
Somebody hacked into the IEBC system wakawa wanacheza na figures. Hii nd'o sababu ilofanya kura
zihesabiwe upya.

Mkuu hakuna kura zinazohesabiwa upya, bali official results zinahakikiwa physical ili kupata matokeo rasmi, ata kama system ingefanya kazi vizuri ili bado hili zoezi la kudhibitisha lingefanyika tu, so kwa kuwa system imefeli sasa matokeo yale ya jumla yaliyotoka majimboni yanaingiziwa pale Bomas, hakuna cha kushangilia hapa mkuu,na hakuna wizi wowote wa kumanipulate data uliojdhibishwa mpaka sasa, jiandae tu kisaikolojia kwani kabla usiku huu haujaisha Kenyatta anarudi sehemu yake.
 
ZeMarcopolo tusikimbiane,am still on team Raila.

Mku, sasa hivi ni kitu tofauti kabisa na awali. Ni sawa na mechi ya home and away. Predictions zote zilizokuwa zinafanywa awali zilikuwa derived kutoka kwenye matokeo yaliyokuwa yanaonyeshwa awali. Kwahiyo hapa pia ikifika stage fulani pia tutaanza tena upya kufanya prediction.
 
kuna sehemu nimesoma ,aliyegundua huu unyama wa safaricom na jubilee ni nguli mmoja wa maswala ya IT ambae pia ni mbunge wa cord.tayari watu wawili wamekamatwa na huyo jamaa kakimbia.
 

Sasa kama lazima zingehakikiwa tena kulikuwa na umuhimu gani wa kutumia system hii?
Kubali ukweli kwamba IEBC Imestukia mchezo otherwise wasingehangaika na manual period!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…