March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

Hata kama Odinga akishinda itabidi atumie busara za hali ya juu kuhakikisha amani inatulia nchini mwake. Pamoja na kwamba sina kuolifikisheni za kuwa adivaiza wa prezidaa, naamini itakuwa vyema kumvuta Uhuru Kenyatta kwenye ka-nafasi ka juu ili kuondoa imani kwa wakikuyu kuwa wameonewa. That's in Kenyans' Best interest unless ICC iamue kuweka mitego mingine ya kumkamata Uhuru. Whoever wins anahitaji kutengeneza mamlaka itakayoaminika kwa pande zote.
 
..
Mkuu hata mimi nilishangaa sana. Huwezi kuona eti kuna constant number difference kati ya Kenyata na Odinga at either 6xxx or 5xxx. Jana tangu asubuhi nilikuwa na-compute tu differences and I was wondering why. Huo engineer anyongwe hadharani kabisa maana anachezea demokrasia za watu. Sasa basi chopa zimeduata matokeo yafanyike mannually ni bora wahesabu siku kumi iwe halali kulika kubaka demokrasia. Long live independent electoral commission of Kenya. Hope things will work better in Tz 2015 havind independent commission in place!! Mwisho wa wizi.

Huyo ni injinia uchwara tu, hata kama mtu unadonoa hutakiwi kudonoa kwa kiasi kikubwa hivyo. Nafikiri lengo kuu lilikuwa kuzuia RUN OFF. Kama hiyo ndiyo ilikuwa ni sababu basi utajua kulikuwa kuna mkono wa chama fulani.

Hapo kwenye nyekundu, hilo litawezekana pale mamlaka ya Kenya itakapomng'ang'ania yule JANGILI wa tembo wa Tanzania. Nashindwa kuelewa ni vipi ameruhusiwa kuingia Kenya......unganisha dots na ujio wa Uhuru pamoja na Kibaki nchini Tanzania b4 uchaguzi.Pamoja na hayo ni wananchi wa Tanzania kukomalia TUME HURU YA UCHAGUZI
 
Duh huu ubize bhana...nilikuwa sijajua chochote kuhusu hii analogie ya huko kenya
 
Who is James Rege?
James Rege expert wa IT na nguli wa masuala ya Mawasiliano Africa. Alikuwa na ni mmoja wa waanzilishi na Mkurugenzi wa kwanza wa Vodacom Tanzania mwaka 2000. Pia alikuwa ni mmoja wa wanahisa wa Vodacom kabla ya kuuza hisa zake na kurudi Kenya na kuwa Super dealer wa Safaricom na biashara za Courier.

Baada ya kuondoka Tanzania alipata pia kuwa Permanent Secretary. Mwaka huu amegombea ubunge jimbo la Karachuonyo kwa tiketi ya ODM na kushinda.

Huyu ndiye aliyestukia mchezo wote uliofanywa na Safaricom of course kuna insiders wamempa hint na si suala la bahati mbaya.
 
Ebu update hapo juu; taratibu mtakubali kuwa ni matokeo yaleyale...

Kenyatta 361, 849

Odinga 205, 000
 
Ni kweli kabisa kama wameanza upya....ni kweli sasa Raila anaongoza mbali sana 69% kwa 27% za Uhuru!
saa 3.30 usiku 6.03.2013 Kenyatta 2,978,119 49.55% Raila 2,834,284 47.2%mchuano wa namna hii haumpi Uhuru wa moja kwa moja. round ya pili must. i think this time around rigging has failed
 
Sasa kama lazima zingehakikiwa tena kulikuwa na umuhimu gani wa kutumia system hii?
Kubali ukweli kwamba IEBC Imestukia mchezo otherwise wasingehangaika na manual period!

Update: Uhuru Ameshashika tena nafasi ya kwanza, tunarudi kulee...
 
NAONA UKABILA AT WORK... UK KESHAMPIGA Gap RAILA kitu cha 156,849...Naona mchezo unaanza kama mwanzo
 
Sasa kama lazima zingehakikiwa tena kulikuwa na umuhimu gani wa kutumia system hii?
Kubali ukweli kwamba IEBC Imestukia mchezo otherwise wasingehangaika na manual period!

Walikuwa wanatumia matokeo ya awali ili kupunguza pressure ya wananchi ukizingatia manual system hutumia muda mwingi zaidi, kuepuka yaliyotokea 2007 walitaka safari iwe faster zaidi, bahati mbaya system imefeli..
 
saa 3.30 usiku 6.03.2013 Kenyatta 2,978,119 (49.55%) Raila 2,834,284 (47.2%) mchuano wa namna hii haumpi Uhuru wa moja kwa moja. round ya pili must. i think this time around rigging has failed
 
Ingawa Sipendi lakini kwa Majonzi Makubwa Nakubalai kwamba Raila anakwenda Kupoteza Pambano. Inauma sana lakini Wakenya wameamua

...haa ha ha, naona mlikuwa mnajipa moyo, huu mchezo ulishaisha longtime, kilichobaki hapa ni kama tu kura zilizoharibika zitawekwa kwenye jumla ya kura au la....
 
NAONA UKABILA AT WORK... UK KESHAMPIGA Gap RAILA kitu cha 156,849...Naona mchezo unaanza kama mwanzo

Sio unaanza Mwakalinga, mchezo tulishauona toka jtatu, ila watu hapa wakawa wanajifariji na eti kuchakachuliwa...
 
Nashangaa za Kisumu,Kisii hazijawekwa hadi sasa
 
Mkuu hakuna kura zinazohesabiwa upya, bali official results zinahakikiwa physical ili kupata matokeo rasmi, ata kama system ingefanya kazi vizuri ili bado hili zoezi la kudhibitisha lingefanyika tu, so kwa kuwa system imefeli sasa matokeo yale ya jumla yaliyotoka majimboni yanaingiziwa pale Bomas, hakuna cha kushangilia hapa mkuu,na hakuna wizi wowote wa kumanipulate data uliojdhibishwa mpaka sasa, jiandae tu kisaikolojia kwani kabla usiku huu haujaisha Kenyatta anarudi sehemu yake.
Butola,

Kwanza labda hatuelewani maana kwa sababu ya kiinglishi na kiswahili. basi kwa ufupi nasema kwamba,
'the votes are being tallied again manually"...sasa tafuta tafsiri ya hio kwa Kiswahili. Sijasema wanahesabu
kura tena from the polling stations. If I insunuated that in any way, samahani.

Pili sishangilii chochote hapo bali ombi langu ni kwamba haki itendeke pande zote ndiposa watu wasiwe na ishu
za kulalamika. Lakini as the way things stand, there will be complaints from whichever side that loses. Hio
ukae ukijua.

Tuzudi kufahamishana kamanda.
 
Back
Top Bottom