March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

Hawa wakenya nao vipi inakuwaje hadi sasa matokeo ya Nairobi bado?

Hata mimi nimeshangaa sana ila ndiyo Citizen TV wanasema wanaanza kutoa ya Nairobi! Ila mkuu Raila hali si njema hata kama babo nyingi hazijahesabiwa! almost Uhur anampita kwa karibia kura laki sita (600,000). Du kazi ipo.,
 
Usiwalaumu voters. Kilichopo katika nchi yetu ni kwamba wapiga kura wana uzoefu wa kuona viongozi hawatekelezi ahadi zao. Kwa hiyo zile sera wanazozihubiri huwa ni sound tu za kuingia madarakani. Hata ukichagua kwa sera haisaidii kitu kwa sababu in the end yatakayofanywa ni mengine.

Ili watu wachague kwa kupima sera ni LAZIMA waamini kuwa sera zinazohubiriwa kwenye majukwaa ndizo zitakazotekelezwa.

Ukitaka kuthibitisha hili anzisha thread ya kuuliza Mnyika ametekeleza vipi ahadi zake? Utashambuliwa na watakaokushambulia watakwambia yale aliyoahidi sio jukumu lake kutekeleza!!!

Ndio maana watu wanachagua kwa preferences za jinsi wanavyojisikia karibu na mgombea either kwa urafiki, ujirani au sababu nyingine.
Ni kweli mkuu, Abas Mtemvu mbunge wangu sioni alilotekeleza, na tutamtosa.
 
Raila is going to close the gap. Just wait and see. Kutakuwa na raundi ya pili hapa for sure. Hakuna atakaefikisha hizo 51%. Kura kutoka maeneo mengi yanayom-support Uhuru Kenyata zimejumulishwa, sasa ni zamu ya Raila nae za kwake kujumulishwa
 
Nitolee mfano wa mbunge wa Tanzania aliyetekeleza ahadi zake na akarudi bungeni kwa sababu hiyo, na uniambie ni nani na ni ahadi gani hizo.

Nitolee pia mifano ya wabunge ambao wamekataliwa kwa kutotimiza ahadi zao.

Hivi Juma Kapuya, John Komba, Anna Makinda na Abas Mtemvu, walitekeleza ahadi gani mpaka wakachaguliwa tena kama si ushabiki wa CCM? Hata jukumu la uwakilishi wa watu wao unaweza kujivunia nini.

ZeMarcopolo, ukipenda chongo utaita kengeza.
Naona hujaelewa huyu ndugu alichokiandika, alichomanisha ni kwamba asilimia kubwa ya wapiga kura hawasikilizi tena sera na ahadi nzuri za mgombea kama kigezo cha kumpigia kwa sababu sera na ahadi ni kama ngazi inayowasaidia kupata kura lakini wakishapata uongozi sera na ahadi hazikelezwi hivyo wapiga kwa sasa hawaoni sababu ya kutumia ilani(sera) kama kigezo cha kuchagua zaidi ya kuangalia vigezo vingine kama kabila, jirani, ndugu au dini au hata jinsia; na amemtaja Mnyika kama mfano angeweza kutaja mbuge yeyote.
 
Hapa ni wazi kazi hipo na hapo ndipo utata unapo anza!

...Haa ha ha, Kalonzo Musyoka akizungumza na Wanahabari, akisema mpaka sasa ni 30% tu ya kura zimehesabiwa na kuwalaumu Jubilee kwa kuanza kusherehekea ushindi wakati eti hakuna anayejua ni nani kashinda mpaka kura zitakapokamilika, ukiisoma body language yake na ya James Orengo aliyekuwepo nyuma yake hautahitaji ushahidi wa IEBC kuwa tayari CORD wameshachinjiwa baharini...
 
Hivi inakuwaje nchi ndogo kama Kenya mpaka sasa wamehesabu asimilia 30% tuu ya kura? Kweli East Africa, we have long way to go.
 
...Haa ha ha, Kalonzo Musyoka akizungumza na Wanahabari, akisema mpaka sasa ni 30% tu ya kura zimehesabiwa na kuwalaumu Jubilee kwa kuanza kusherehekea ushindi wakati eti hakuna anayejua ni nani kashinda mpaka kura zitakapokamilika, ukiisoma body language yake na ya James Orengo aliyekuwepo nyuma yake hautahitaji ushahidi wa IEBC kuwa tayari CORD wameshachinjiwa baharini...
Sijui kwa nini anawalumu Jubilee kuanza kusherehekea, hata kama ningekuwa mimi bila kujali matokeo ya mwisho Kalonzo anafikiri kuongoza toka jana ni mchezo.
 
Tunaiomea Kenya mchakato wa uchaguzi uishe vizuri. Atakayeshinda ndiye chaguo la watu na la Mungu pia.
Mkuu ni sawa lakini usimchanganye Mungu kwenye mambo ya uchaguzi, kwanza utawala wa Mungu hauna cha kupiga kura, ni dictatorship kama jeshi!!

Naona hujaelewa huyu ndugu alichokiandika, alichomanisha ni kwamba asilimia kubwa ya wapiga kura hawasikilizi tena sera na ahadi nzuri za mgombea kama kigezo cha kumpigia kwa sababu sera na ahadi ni kama ngazi inayowasaidia kupata kura lakini wakishapata uongozi sera na ahadi hazikelezwi hivyo wapiga kwa sasa hawaoni sababu ya kutumia ilani(sera) kama kigezo cha kuchagua zaidi ya kuangalia vigezo vingine kama kabila, jirani, ndugu au dini au hata jinsia; na amemtaja Mnyika kama mfano angeweza kutaja mbuge yeyote.
Nimemwelewa sana.

Huyo mkuu ni anti-Mnyika, ndio maana nimemjibu hivyo. Kwa maoni yake, Mnyika hapaswi kuongea bungeni mf. tatizo la maji, bali kuwaletea watu wa ubungo maji. Anakerwa mawaziri wanapoulizwa maswali magumu na Mnyika. Kwa nini mfano alioutoa ni mfano wa Mnyika tu.

Humu JF tunafahamiana.
 
Mwanaume kutegemea umbeya kuishi mjini mbaya sana.

Daah! Lameck Madelu aka Mwigulu bhana!!! Ama kweli wewe ni Mchizi wa Ukweli. Vipi wale wanaotegemea kuendelea kubaki madarakani kwa kubaka demokrasia na kufanya mauaji? Hiyo iko poa siyo. Acha unazi dogo....

CC. Ben Saanane
 
Mpaka sasa Uhuru 54%.
Raila 41%
Kura bado znaendelea kuhesabiwa mpambano ni mkali
 
If we factor in spoilt votes, runoff becomes a reality. What! has it been raining somewhere? Impetous child! Yes so many tears.
 
mpaka sasa uhuru 54%.
Raila 50%
kura bado znaendelea kuhesabiwa mpambano ni mkali
kweli huuu ujinga mpaka % hatuzijui hv hii nchi tunaipeleka wapi!? Hebu jumlisha % zako zimezidi 100 kwanini!?
 
Sijui kwa nini anawalumu Jubilee kuanza kusherehekea, hata kama ningekuwa mimi bila kujali matokeo ya mwisho Kalonzo anafikiri kuongoza toka jana ni mchezo.

Suala sio kuongoza tokea jana bali ni kura za wapi zimeshahesabiwa. Kwa jinsi ninavyoona hii ngoma itaenda second round kwani aslimia za Uhuru zinazidi kupungua and we are talking about aproximately 5 millions votes out fourteen millions that were supposed to be casted. This game is too far from over; my advice, get your popcorns ready and enjoy the rollercoaster.
 
mkuu Consigliere ukabila pembeni kwanza tuangalie sera za candidate mhusika,most voters in East Africa ukiwauliza kwanini unampenda mgombea fulani? atakujibu
1.ni mkristo/muislamu mwezangu
2.ni kabila la kwetu
3.nimetokea tu kumpenda
tunapiga kura kwa mazoea tu,hakika hata mm ningesimama nafasi ya Uhuru Kenyatta ningekuwa rais wa kenya jpokuwa sina sifa yoyote zaidi ya kabila

uongeacho ni sahihi kabisa, lakini ili uwe safe side, side ya kuumia kuona unachokipenda hakipewi kibali machoni pa watu, inakubidi ukumbuke kuwa only minority ndiyo hutumia akili katika ku reason but majority wanahitaji kutekwa, kushawishiwa nk...just to win them.
Wengine hutafuta personal or group interest to satisfy their desire, hapo ndipo suala la udini, ukabila na asili huibuka.
 
Tanzania kuna hivi vitu 3 uwe navyo ili uwe kiongozi wa nchi
1.Uwe unajua kutoa na kuithamini RUSHWA ili kuwashawishi wapiga kura wakuchague
2.uwe na ushawishi mkubwa wa KIDINI
3.Jifunze kuwa MUONGO kwa hali ya juu sana,bila kudanganya hupati kura hata moja
 
kweli huuu ujinga mpaka %
hatuzijui hv hii nchi tunaipeleka wapi!? Hebu jumlisha % zako zimezidi
100 kwanini!?

WANAJANVI hum ndani tunaviplate kinoma kashindwa kujua ata Odinga anaasilimia ngapi? shem on u. Odinga mida hiyo alikuwa na 40.7%.
 
nimejaribu kutafuta wastani wa matokeo hayo kwa kujumlisha asilimia za kila jimbo kwa kila mgombea na kutafuta wastani. Nimepata kuwa kama yanaakisi matokeo ya mwisho basi uhuru anaweza akashinda kwa asilimia 50.6 na Odinga anaweza kupata asilimia 45.2. hata hivyo, kwa kuwa matokeo yaliyotolewa kwenye link hiyo kwa kila jimbo yametolewa kwa asilimia lolote laweza kutokea kwa sababu matokeo ya asilimia sio lazima yaakisi matokeo ya kura mojamoja zikijumlishwa kwaa nchi nzima na kutafutiwa asilimia kwa pamoja. kwa mfano fikiria mgombea wx katika jimbo A amepata kura 80 kati ya 100 zilizopigwa sawa na 8o% na katika jimbo B amepata kura 0 kati ya kura 10 zilizopigwa sawa na 0%. Mgombea yz amepata kura 20 kati ya 100 zilizopigwa katika jimbo A sawa na 20% na katika jimbo B akapata kura zote kumi kati ya kumi zilizopigwa sawa na asilimia 100%. ukitumia kutafuta wastani kwa kutumia asilimi yz ndo mshindi. lakini ukijumlisha kura moja moja na kuatafuta asilimia wx ndio mshindi. kwa hiyo mgawanyo wa kura kama unavoonekana kwenye link hiyo inawza kuakisi matokeo ya mwisho au isiakisi. tungoje na kusubiri tume itoe matokeo.

muda mfupi kama saa moja ilopita Uhuru alikuwa na silimia 55 na Odinga 40. sasa hivi 17:34 Uhuru ni 53.6 na Odinga ni 42. hii ni kwa mujibu wa Kenya Elections 2013 - Daily Nation
 
Nimemwelewa sana.

Huyo mkuu ni anti-Mnyika, ndio maana nimemjibu hivyo. Kwa maoni yake, Mnyika hapaswi kuongea bungeni mf. tatizo la maji, bali kuwaletea watu wa ubungo maji. Anakerwa mawaziri wanapoulizwa maswali magumu na Mnyika. Kwa nini mfano alioutoa ni mfano wa Mnyika tu.

Humu JF tunafahamiana.
Kama ni mpinzani wa Mnyika na unamjua siku zote hapo sawa.
 
Back
Top Bottom