March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

Yeah.utaanzaje kutangaza matokeo kisha uyasitishe ghafla? Kwangu mimi saa takribani kumi kusitisha matokeo mpaka kesho asubuhi ni nyingi sana kwa chochote kuweza kufanyika.
 
Yawezekana anacholisema Tiba ni sahihi lakini ukweli ni kwamba kura hazijaisha kuhesabiwa kwa hiyo sio rahisi kujua idadi ya watu waliopiga na kama wameshajua idadi ya waliopiga toka jana kazi ingekuwa imeshaisha maana hizo percentage toka jana zinatolewa kwa maana hiyo kama unakubali maelezo ya Tiba kwamba idadi ya waliopiga inajulikana obvious kwa muda wote huo hata kura za mmoja mmoja zingekuwa zishajulikana na kazi ingekuwa imeshaisha.

Ndugu yangu una rahisisha mambo sana. Kuhesabu kura zote zilizopigwa kwenye kituo ni rahisi sana. Kimbembe ni pale ambako kila kura inafunguliwa na kuangaliwa ni ya nani na wawakilishi wa vyama kuhakikisha kwamba ni kweli kura hiyo ni ya huyo mgombea. Hili zoezi ni gumu kidogo na ndilo hasa linalosababisha matokeo kuchelewa. Nisingependa kuendeleza hii ligi, kama ni mtu wa kuelewa, natumaini umeelewa.

Tiba
 
Naona Tume ya Uchaguzi makao makuu BOMAS Nairobi, imeshaanza kujivua lawama kama za Marehemu Kivuitu na kuwataka "The Returning Officers will start bringing the official results any time now. We will announce the official results beginning tomorrow. Each commissioner will read out results for each of the region that they supervise," he said IEBC Chairman Isaack Hassan .

Tuesday March 5, 2013
Nairobi, Kenya

IEBC to start releasing official results on Wednesday

The Independent Electoral and Boundaries Commission (IEBC) has said it will start announcing official election results from Wednesday after its electronic transmitters experienced delays.


IEBC Chairman Isaack Hassan explained that the delays experienced in the electronic transmission of election results from polling stations had prompted them to decide to release official results being submitted by Returning Officers.


The Returning Officers are currently on their way back to the national tallying centre in Nairobi from their respective postings in the 290 constituencies.


IEBC has been releasing provisional results that were transmitted from polling stations using the electronic transmission system. The system has however developed serious delays.


"There is a growing concern at the slow pace that results are being relayed. This has given rise to speculation and rumours that our servers have crashed.. We are working to sort out the delay," said IEBC chairman Isaack Hassan.


"The Returning Officers will start bringing the official results any time now. We will announce the official results beginning tomorrow. Each commissioner will read out results for each of the region that they supervise," he said.


Source: IEBC to start releasing official results on Wednesday - CAMPAIGN NEWS - elections.nation.co.ke
 
Ndio tatizo la kutaka kukimbia kabla ya kutambaa. Wanata hi tech system wakati hata "low tech" hawajawahi kuona!!!


Si walisema Kenya inaongoza kwa IT Afrika Mashariki na ya Kati na mitandao (network interconnection) ya IT ipo bomba sana kusafirisha 'data' kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki, bora wangeomba kupitishia 'data' katika mkongo wa mawasiliano wa taifa NATIONAL FIBER OPTIC CABLE NETWORK (MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO)Kilimanjaro - TEHAMA wa Tanzania mambo haya yasingewakuta.
 
Si walisema Kenya inaongoza kwa IT Afrika Mashariki na ya Kati na mitandao (network interconnection) ya IT ipo bomba sana kusafirisha 'data' kuliko nchi yoyote Afrika Mashariki, bora wangeomba kupitishia 'data' katika mkongo wa mawasiliano wa taifa NATIONAL FIBER OPTIC CABLE NETWORK (MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO)Kilimanjaro - TEHAMA wa Tanzania mambo haya yasingewakuta.

Si unajua mkuu, kwenye vipofu akitokea mmoja akaweza kuona angalau ukungu kwa mbali basi huwa ndio mwenye kuelekeza wenzake njia.
 
Naona Kenyatta anazidi kumpeperushia manyoa Raila... Gap la 500,000, labda awasiliane na ccm wamfundishe au kumsaidia namna ya kukimbia na masanduku au kuchakachu matokeo....

awasiliane na makongoro mahanga..
 
Aliye kenya pse tujulishe huyo mwanamke aliyetanzazwa na citizen kuwa amefariki huko kislii sababu ni nini?
 
ha ha haaa, Africa bado sana na mambo ya technology! Mnakumbuka kipindi kile kwa Bush, USA ilibidi jimbo moja, nafikiri California ilibidi kura zihesabiwe kwa mkono?
 
awasiliane na makongoro mahanga..

Yap mkuu, mzee wa masanduku huyo, pia ni Thatha wangu, ila kwa sasa mild strock plus ule ugonjwa wetu wa mujini unamsumbua sana, inawezekana ni laana ya kudhurumu kura...
 
That was yesterday if am not mistaken!

Kikundi cha watu wenye silaha kimeteka nyara vituo viwili vya kupigia kura huko Garissa Kaskazini mwa Kenya karibu mwa mpaka wake na Somalia.

Vilevile imeelezwa kuwa watu wapatao 19 wameuawa katika matukio mbalimbali yanayohusiana na uchaguzi.

Chanzo: Gazeti la Metro 5.3.13

View attachment 85678
 
nilikuwa naongea na rafiki yangu ambae nae yupo kwenye usimamizi wa uchaguzi anasema kuna baadhi ya matukio mengi tu yametokea huko ila uchaguzi wa mwaka huu media zote walikubaliana kuwa wasireport habari hizo kwa sana maana kipindi kilichopita media zilichangia sana kuhamasisha machafuzi na inavyoonekana uhuru atashinda ilingali wengi hawakubaliani nalo wanasubiria kesho kuona watu watapokeaje hayo matokeo. kweli africa sijui tukoje tuwaombee hili jambo lipite salama lisipopita ni balaa, maana kenya mambo yakiharibika ni matatizo hata kwetu
 
sasa hii habari haina ladha hata kidogo, tushasikia uwepo mkubwa wa uchakachuaji wa kura kwa kuwatumia IT gurus wa safaricom hadi tume imesitisha kuendelea kutangaza matokeo. Aibu sana hii
 
Back
Top Bottom