17:29 Matokeo ya mwanzo mwanzo ya kura za urais yaliyotolewa sasa hivi kutoka kwa tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Raila Odinga ana kura 2,133,202 wakati Uhuru Kenyatta ana kura 2, 718,021
17:05 Kwa sasa Raila Odinga ana kura 2, 107, 670 wakati Uhuru Kenyatta akiwa na kura 2,697,056
17:02 Vigogo wa Muungano wa CORD wake Raila Odinga wamesema kuwa licha ya matokeo kuonyesha bado wako nyuma, wafuasi wao wasiwe na wasiwasi kwani kura nyingi zingali kuhesabiwa. Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka amewaambia wapiga kura kupitia televisheni kuwa wawe watulivu wasubiri matokeo kutoka kwa tume ya uchaguzi
15:00 Matokeo kufikia sasa ni kwamba Uhuru Kenyatta amepata kura 2,606,617 wakati Raila odinga ana kura 2,011,869
14:31 Hadi kufikia sasa kulingana na matokeo yanayotolewa na Tume huru ya uchaguzi Kenya ni kuwa Uhuru Kenyatta amepata kura 2,534 019 wakati Raila Odinga akiwa na kura 1,939,549. Haya ni matokeo ya mapema tu
13:05 Abdulkarim Taraja akiwa Mt Elgon, anasema kwenye Bofya facebook kuwa anafurahi ambavyo wanaoshindwa wanakubali matokeo ya kura katika eneo hilo
12:59 Blessed Kuriah anasema kwenye ukurasa wa Bofya facebook, Bofya bbcswahili, kuwa hali ni tulivu katika eneo bunge la Gatundu Mkoa wa Kati
12:57 Uhuru Kenyatta 2,484,760 Raila Odinga 1,884,152
12:46 Mwandishi wetu Jamuhuri Mwavyombo akiwa mjini Mombasa anasema mji umetulia, maduka mengi yangali yamefungwa watu wakiwa na wasiwasi kuangalia hali itakavyokuwa
12:37 Uhuru Kenyatta 2,459,133 Raila Odinga 1,851, 671
12:24 Idadi ya kura kwa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta 2,429,895 Raila Odinga 1,823,384
source:BBC SWAHILI WEBSITE.