March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

March 04 2013: Kenya's historic poll - Kenya decides!

nimeisoma hiyo taarifa, walilalamika sawa...
but how often? What about the Railas.
Railas si alisha gongwa na Nyoka? akiona unyasi tuu anajua kikuyu kashatia timu...!! Lakini its through those raised concerns, ndipo IEBC waliposhituka ile "times 8 factor" ya rejected votes
 
ukwelikituganikama utakumbuka kuwa hawa jamaa walijisifu sana kuwa wana tume huru na katiba mpya ambayo ni nzuri swali linakuja kwanini sasa wanaanza kupoteza imani na tume waliyoiita huru na mipaka? na mwisho ni katiba kama walitengeneza katiba wakaaita mpya na wakaamini inajitosheleza watulie wasubiri matokeo na watumie katiba katika kuamua kama uchaguzi haukua haki basi waende mahakamani au na mahakama nayo hawaiamini au nayo ni ya kabila fulani?
wakati wa kampeni najua ma suspect walijitahidi sana kupiga kampeni za kistaharabu kuliko kambi ya raila
 
Last edited by a moderator:
Tume huru kwa nchi za Kiafrika bado ni kazi ngumu kufanya kazi kwani zinakuwa influenced na viongozi pengine nahisi zinapokea maagizo fulani kuufavour upande mmoja na hili pengine linataka kujitokeza kwenye uchaguzi huo wa Kenya.Jambo jingine ni kuwa kwa nchi ambazo zina makabila machache kama wenzetu ni rahisi sana kuutumia kwenye chaguzi zao na ambalo linaleta matatizo
 
Mkuu huo mzigo ni kutoka majimbo 141 out of 291. Ngoja tuone kama gap litaendelea kupukutika ama litapanda tena ama litabaki hapohapo.
dah! uchaguzi una presha huu sijapata kuona, inawezekana kweli hao wagombea wenyewe hawajajumlisha kura zao kwa kupitia mawakala wao na kujua jumla ya kura zao?
nakumbuka kwa mnyika ubungo ndani ya masaa machache tumeshajua kura tulizokuwa nazo kibindoni..
 
Je majimbo yalobaki ni nani mwenye ushawishi mkubwa?
 
Kabla ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta, na hata kabla ya Jaramogi Oginga Odinga na Jomo Kenyatta, kabla hata wakoloni hawajaitawala, KENYA ILIKUWEPO NA ITAENDELEA KUWEPO. Wakenya pendaneni kwani sasa na baada ya uchaguzi, wote ni wakenya tu.
 
........ kitu kina gonga kyupi na kurudi.....
.

Ha ha haaaa! we jamaa Fidel80 umenifanya nicheke sana ndugu, khaaaaa!Bila shaka hapa unamaanisha 'mavi"duuuuuh!

gap kwa sasa ni kura 363,319 bila senti lol! hao ni baada ya hesabu za kaunti 132 out 0f 291 at around saa 9:30pm
 
Last edited by a moderator:
Ha ha haaaa! we jamaa Fidel80 umenifanya nicheke sana ndugu, khaaaaa!

gap kwa sasa ni kura 325,390 bila senti lol!

Toka laki 6 huku sasa zinapukutika jamaa wanawakati mgumu kuliko wale wa Raila walio kuwa wakijipa moyo
 
Last edited by a moderator:
17:29 Matokeo ya mwanzo mwanzo ya kura za urais yaliyotolewa sasa hivi kutoka kwa tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Raila Odinga ana kura 2,133,202 wakati Uhuru Kenyatta ana kura 2, 718,021
17:05 Kwa sasa Raila Odinga ana kura 2, 107, 670 wakati Uhuru Kenyatta akiwa na kura 2,697,056
17:02 Vigogo wa Muungano wa CORD wake Raila Odinga wamesema kuwa licha ya matokeo kuonyesha bado wako nyuma, wafuasi wao wasiwe na wasiwasi kwani kura nyingi zingali kuhesabiwa. Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka amewaambia wapiga kura kupitia televisheni kuwa wawe watulivu wasubiri matokeo kutoka kwa tume ya uchaguzi
15:00 Matokeo kufikia sasa ni kwamba Uhuru Kenyatta amepata kura 2,606,617 wakati Raila odinga ana kura 2,011,869

14:31 Hadi kufikia sasa kulingana na matokeo yanayotolewa na Tume huru ya uchaguzi Kenya ni kuwa Uhuru Kenyatta amepata kura 2,534 019 wakati Raila Odinga akiwa na kura 1,939,549. Haya ni matokeo ya mapema tu
13:05 Abdulkarim Taraja akiwa Mt Elgon, anasema kwenye Bofya facebook kuwa anafurahi ambavyo wanaoshindwa wanakubali matokeo ya kura katika eneo hilo
12:59 Blessed Kuriah anasema kwenye ukurasa wa Bofya facebook, Bofya bbcswahili, kuwa hali ni tulivu katika eneo bunge la Gatundu Mkoa wa Kati
12:57 Uhuru Kenyatta 2,484,760 Raila Odinga 1,884,152

12:46 Mwandishi wetu Jamuhuri Mwavyombo akiwa mjini Mombasa anasema mji umetulia, maduka mengi yangali yamefungwa watu wakiwa na wasiwasi kuangalia hali itakavyokuwa
12:37 Uhuru Kenyatta 2,459,133 Raila Odinga 1,851, 671

12:24 Idadi ya kura kwa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta 2,429,895 Raila Odinga 1,823,384

source:BBC SWAHILI WEBSITE.




mbona kura zinapungua??
 
Back
Top Bottom