Watu wasiompenda Messi wametafuta vichaka vingi sana vya kujificha, kote hapawasaidii. Walijaribu kwa mshkaji wao Ronaldo, wakagundua kichaka ni kifupi. Wakajaribu kwa Mbappe, wakakuta kichaka ni kidogo mno. Wamerudi kwenye kichaka cha pele, na chenyewe hakitawasaidia!
Kwanza kabisa, kuwalinganisha wachezaji kwa kuangalia wameshinda world cup ngapi, ni kuonyesha kiwango kidogo cha uelewa. World cup sio individual trophy, ni kitu kinapatikana kwa efforts za team nzima. Ndio maana Olivier Giroud anayo, ila Cristiano Ronaldo hana!
Lakini pia kuanzia mechi za makundi, mpaka fainali ya world cup, ni mechi saba pekee. Ni uongo kupima ubora wa mchezaji kwa mechi saba pekee. Ndio maana kuna wachezaji wengi huwa wanaonekana kung'ara kipindi cha world cup, na kisha wanapotea. Unamkumbuka Diego Forlan? Unamfahamu golikipa wa kuitwa Ochoa? Hao ni baadhi ya waliong'ara kwenye kombe la dunia pekee, na sababu ni uchache wa mechi. Only seven matches from group stage, to the final!
Ubora wa mchezaji, tutaupima kwa kuangalia performance yake ya kila siku. Pale England, majitu yanacheza mechi kama 30 kwa msimu za EPL pekee. Yanakutana kwenye Carrabao cup, FA cup, Champions League na wengine Europa League. Hiyo ni zaidi ya mechi 40 kwa msimu. Na hiyo ni kwa ligi zote kubwa ulaya, England, Spain, France, Germany na kwingineko. Hapo tunapata kweli kuuona ubora wa mchezaji, sababu sio rahisi kua na consistency kwenye mechi zaidi ya 30 ndani ya msimu mmoja.
Leonel Messi na Cristiano Ronaldo wamethibitisha ubora wao kwa kufanya mambo makubwa kwa miaka zaidi ya kumi sasa kwenye hizi ligi. Wamefunga kila aina ya magoli, wamevunja na kuweka kila aina ya rekodi. Hakuna unachoweza kuwadai wao kama individual players. Kutuambia eti hawamfikii Pele kwakua Pele ameshinda world cups nyingi, ni kutuongopea. Pele hakushinda world cup peke yake, zilikua juhudi za team nzima ya Brazil aliyokuwemo!
Hata juzi, Emiliano Martinez alifanya save dakika ya mwisho kabisa ambayo ndiyo iliyowanyima France ubingwa. Sio sahihi kumpa sifa Messi pekee, zilikua juhudi za team nzima. Ndio maana hata Pele hatakiwi kubeba sifa za kushinda world cup peke yake, zilikua juhudi za wengi.
Mwisho wa siku, mchezaji bora anaamuliwa na individual performance. Umefunga magoli mangapi, umetoa assists ngapi, umechangia nini kwenye performance ya team? Hapo ndipo tunaporudi kuangalia takwimu za mchezaji kwa nafasi anayocheza. Na hapo ndipo Messi na Ronaldo wanasimama juu ya hao giants, Pele na Maradona.
Mimi binafsi, Ronaldinho Gaucho ndio mchezaji ninaemkubali kuliko wote. Namuona kama the most complete football player ever. Lakini tukiweka individual records zake mezani, hatoboi kwa Ronaldo na Messi.
Tutaenda mbele, tutarudi nyuma. Tuliweka kipimo cha mchezaji bora duniani kikaitwa Balon d'Or. Siku akitokea mchezaji akawa nazo nyingi kumzidi Messi, basi yeye ndie atakua bora. Ila kwa sasa, hicho ni cheo cha Leonel Andres Messi Cuccittini pekee!
Kama unapinga, leta individual records za mchezaji wako tulinganishe. Usiniambie kuhusu makombe, hayo ni matokeo ya juhudi za team nzima. Tuletee individual records!
NB: Dani Alves ndie the most decorated football player of all time. Ameshinda makombe mengi kuliko mchezaji yeyote aliepata kutokea. But we don't consider him as the G.O.A.T.