Marcus Rashford amefunga mabao 9 katika mashindano yote tangu ilipomalizika michuano ya kombe la dunia

Marcus Rashford amefunga mabao 9 katika mashindano yote tangu ilipomalizika michuano ya kombe la dunia

lugoda12

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
276
Reaction score
574
Marcus Rashford amefunga mabao 9 katika mashindano yote tangu ilipomalizika michuano ya kombe la dunia, ambayo ni mengi zaiidi ya mchezaji mwengine yoyote kwenye zile ligi tano bora barani ulaya.

✍️Marcus Rashford pia sasa amehusika katika mabao 9 dhidi ya Arsenal, mengi kuliko kuliko aliyohusika dhidi ya timu nyengine yoyote ya premier league katika career yake.

Rashford dhidi ya Arsenal katika premier league

michezo 15
mabao 5
pasi za mabao 4

bao alilowafunga Arsenal hapo jana, lilikuwa ni bao lake la kwanza kufunga dhidi yao katika dimba la Emirates.

✍️takwimu za Marcus Rashford msimu huu hadi sasa kwenye premier league

michezo 20
dakika 1620
mabao 9
pasi za mabao 3
amehusika katika mabao 12

√ ana wastani wa kufunga bao kila baada ya dakika 180

✍️Marcus Rashford katika mashindano yake tangu alipoanza timu ya wakubwa ya Manchester United.

michezo 301
mabao 110
pasi za mabao 51.

FB_IMG_1674459214323.jpg
 
Haaland amezungumzwa na kufunguliwa nyuzi za kutosha hapa jukwaa la michezo labda kama taarifa ziliwapita, Mleta bandiko kwasasa amevutiwa na Rashford.
 
Mkuu kwanini usifungue wewe tuje kuchangia kama hapa lakini umeishia kulalamika kama mwanamke aliyetelekezwa na mme kaachiwa watoto wa 3.

Ujazuiliwa kufungua uzi wake mkuu.
Hicho nilichokiandika ndio mchango wangu mkuu. Au unadhani mchango ni lazima uendane na mawazo yako?

Kuhusu hizo kejeli ulizoziandika hapo, mimi pia naziweza. Ila nimechagua ustaarabu!
 
Back
Top Bottom