Guasa Ambonii
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 8,545
- 10,283
Shukran mzee wanguGuasa,
Tusahau haya yeshapita tuangalie mbele.
Mnaharibu uzi hii ni sport na ameshawajibu wengine vizuri tu,heshima kwa watu wazima hasa wanaojibu kiungwana namna hii hauhitaji wazaz wakuambieWewe mzee unapenda sana muunganiko na wafu, eti? Haya Moo kapeleka milioni 100 nenda ukasome khitma mle ubwabwa. Ujue kwa imani za watu wengine ibada za wafu ni dhambi. Mbona unakuwa ni mwenye kuchanganya kila kitu na imani yako?
Sura nzuri kama kuna la kuongezea watakuja wengine.Sura jamil..nifahamishe jamil maana yake nn
Maalim Mohamed Said kwanza natoa salamu kwako pili uniwie radhi kwa kurudisha nyuma uzi wako kwani nimechelewa kuuona,tatu usiwe mnyonge hata siku moja kwa kusema Maktaba yako imechoka ukweli ni kuwa Maktaba iliyochoka ndiyo iliyosheheni hazina ya kumbukumbuSergio,
Maktaba imechoka kwa ajili ya kuhamahama.
Maalim wanguGuasa,
Hii ya Kitwana Popat sijui lilikujaje.
Mwinda Ramadhani ''Maajabu,'' ni ile ''good football,'' yake.
Chogo alikuwa akifahamika kwa Chogo Chemba au Chogo Mluya,Guasa,
Juma Chogo, ''Mluya'' jitu la Kenya.
Maalim Wangu Abdulrahaman Juma ni kweli hakuwa Center half au Mkoba, aliyekuwa akicheza Mkoba ni *Mwamba Kapera,* sikuwahi kumuona hata siku moja Mwamba kapera akicheka hovyo uwanjani!Ndinani,
Abdulrahmani Juma hakuwa ''centre half,'' watoto wa mjiini wakiita
''mkoba.
''Yeye alikuwa akicheza mbele na Yanga wakimuita ''Bwana Fedha.''
Abdulrahmani alikuwa na ''gentleman player,'' ''excellent ball control.''
Sasa pale katika alikuwa akigawa mipira kila mahali kama vile ''cashier,''
anavyolipa fedha ndiyo wakampa jina hilo.
Mbetini,Maalim Wangu Abdulrahaman Juma ni kweli hakuwa Center half au Mkoba, aliyekuwa akicheza Mkoba ni *Mwamba Kapera,* sikuwahi kumuona hata siku moja Mwamba kapera akicheka hovyo uwanjani!
kitu kimoja naomba nikukumbushe kuhusu Captain Abdulrahrahman Juma mbali na kuitwa cashier alijulikana zaidi kwa jina la LINK MAN ilikuwa kila mpira kona anaenda kupiga yeye na hapo sisi mashabiki wa Yanga tulikuwa tunashangilia kwa sababu alikuwa anapiga kona mpira unakuwa hatari ya kufugwa wapizani wetu.
Sikuwahi kumuona Link man apige kona itoke nje au iwe fyogo wala short corner.
Mbetini,Maalim Mohamed Said kwanza natoa salamu kwako pili uniwie radhi kwa kurudisha nyuma uzi wako kwani nimechelewa kuuona,tatu usiwe mnyonge hata siku moja kwa kusema Maktaba yako imechoka ukweli ni kuwa Maktaba iliyochoka ndiyo iliyosheheni hazina ya kumbukumbu
Maalim wangu
Kitwanna Popat na kitwana Douglas ni wachezaji wawili tofauti.
Kitwana Popat ni kitwana Manara na ndiye aliyekuwa Golikipa na akaja kuwa center forward akicheze timu ya Yanga.
Kitwana ni kaka yake Sunday Manara (computer) na Kassim Manara wote walichezea Yanga. Nyogeza ya habari ni Baba yake Mkubwa Hajji Manara Msemaji wa simba kwa sasa!!
Kitwana Douglas huyu ni mchezaji mwingine na alikuwa anachezea Cosmo.
Chogo alikuwa akifahamika kwa Chogo Chemba au Chogo Mluya,
Hii Chemba ilikuwa ni aina yake ya kupiga mpira, kwanza mpira anauputa unapaa juu kisha anabutua kwa kuruka juu sasa huo urukaji ndiyo ukitwa Chemba. Huu urukaji wake wakati anafanya hivyo vituko mashabiki wa Simba hulipuka kwa kushangilia sana.
Hivyo ukaigwa na kujulikana kama kupiga Chemba.
Boxboy,SIMBA ni ile ya kina Juma Mzee
Kilomoni
Msomali
Kulikuwa Na Dreva Taxi alikuwa anapark club ya SIMBA pembeni alikuwa anaitwa Mzee Mwinyigumba aka Under line
Hiyo SIMBA Mbwiga hawezi kuijua
Mbetini,Maalim Mohamed Said kwanza natoa salamu kwako pili uniwie radhi kwa kurudisha nyuma uzi wako kwani nimechelewa kuuona,tatu usiwe mnyonge hata siku moja kwa kusema Maktaba yako imechoka ukweli ni kuwa Maktaba iliyochoka ndiyo iliyosheheni hazina ya kumbukumbu
Maalim wangu
Kitwanna Popat na kitwana Douglas ni wachezaji wawili tofauti.
Kitwana Popat ni kitwana Manara na ndiye aliyekuwa Golikipa na akaja kuwa center forward akicheze timu ya Yanga.
Kitwana ni kaka yake Sunday Manara (computer) na Kassim Manara wote walichezea Yanga. Nyogeza ya habari ni Baba yake Mkubwa Hajji Manara Msemaji wa simba kwa sasa!!
Kitwana Douglas huyu ni mchezaji mwingine na alikuwa anachezea Cosmo.
Chogo alikuwa akifahamika kwa Chogo Chemba au Chogo Mluya,
Hii Chemba ilikuwa ni aina yake ya kupiga mpira, kwanza mpira anauputa unapaa juu kisha anabutua kwa kuruka juu sasa huo urukaji ndiyo ukitwa Chemba. Huu urukaji wake wakati anafanya hivyo vituko mashabiki wa Simba hulipuka kwa kushangilia sana.
Hivyo ukaigwa na kujulikana kama kupiga Chemba.
Muungwana ni vitendo na huyo ndio Alhaji sheikh Muungwana mzee wngu Mohamed Said ninaye mjua mie safi sna mzee wngu ila naomba nikupe kisa ambacho umewahi kukiandika na kunieleza mara nyingi japo sikumbuki vzuri nafikiri ilikuwa kwenye kikao cha TANU kupitasha wagombewa wao kuna mtu alimuuliza Sir George Kahama swali naweza kusema la kizushi juu Mali zake na kumfananisha na bepari lkn kwa hekima za mwalim nyerere alimkataza Sir George Kahama kujibu swali ilo kutoka na yy mwenyewe mwalim kumjua vzuri Kahama na historia yao nami pia na kuomba sna usiwe unawajibu watu wajinga wajinga na malofa km hao mzee wngu maana kwanza anaonekana ni mgeni mpili uzi unazungumzia mambo mengine na yy analeta mambo mengine unajua dunia yetu ya leo hii chizi au mwenda wa zimu sio mpk avue nguo mzee wngu nina hakika huyo kijana wenzangu Akili zake hazipo sawaAbunuwasi,
Iko siku niko Marekani nafanyiwa utambulisho kabla sijapanda jukwaani
kuzungumza.
Mzungumzaji kanipamba mwisho wa kunipamba.
Ghafla inanijia picha ya marehemu mama yangu nina miaka mitano tuko
sokoni kwa muuza vitabu ananinunulia kitabu cha ''Jifunze Kusoma.''
Anamlipa muuzaji ananikabidhi kitabu na tulipofika nyumbani yeye ndiye
mwalimu ananianzisha alif kwa kijiti.
Kuna kitu kilipanda hadi kooni kikanikwama machozi yanataka kunitoka.
Najiambia, ''Ingekuwaje mama yangu, mwalimu wangu Bi. Mwanaidi biti
Sheikh leo ungelikuwa hapa ukaniona mie mwanao nahadhiri chuo kikuu
Marekani na hawa Wazungu wameitana kuja kunisikiliza...''
Laiti mzungumzaji angeliendelea zaidi ningelihadhirika.
Ningeliwamwagia chozi...
Abunwasi,
Hayo mimi ninakutananayo kila siku wala yasikupe tabu.
Huyo anaugua maradhi ya nafsi na ni mabaya sana kwani tiba yake ni ghali
mno.
Ngoja nihitimishe.
Alikuja Mhariri wa Oxford Univeristy Press kutoka Nairobi kuja turekebishe vitu
fulani katika kitabu nilichoandika ili wakichape.
Tumeifanya kazi tushamaliza.
Kumbe huyu bwana ana kitu kinamchonyota.
Muda wote tukisema Kiswahili.
Sasa anafunga lap top yake ananiuliza, ''Mr. Said hiki kitabu uliandika kwa Kiswahili
halafu ukampa mtu akuwekee kwa Kiingereza?''
Jibu langu lilikuwa hapana.
Nikataka tufahamiane ili siku nyingine anipe kazi.
Nikamwambia nina First Class Merit Pass English Oral Cambridge Examination 1970.
Mimi nilimwia radhi kwa kuwa alikuwa akisikia Kiswahili changu kina ''heavy accent,''
ya usemaji wa Kidaresalama ikamjia fikra nyingine.
Maalim wanguMbetini,
Nashukuru sana kwa kunikumbusha hili jina la Link Man mimi nililisahau.
Hakika Abdulrahman Juma ndiye alikuwa ''corner taker,'' wa Yanga na
kitu kimoja ni kuwa ile mipira yake ilikuwa inaangukia kwenye kichwa
cha Kitwana Manara.
Kumbe wewe Yanga!
Aha!
Hakuna neno bila nyinyi sisi hatuwezi kuwepo na mpira utakuwa hauna
ladha yoyote.
Mara ya mwisho nimekutana na Abdulrahman Juma ilikuwa Mtaa wa
Congo na Uhuru baada ya hapo sikumuona hadi alipofariki.
Allah amrehemu.
Mbeteni,Maalim wangu
Allah awa rehemu waasisi wa hizi klabu na wachezaji waliotangulia mbele ya Haki.
Maalim la Uyanga naam mi Yanga damu tena Kwala!,kwenye ukoo wetu wote sisi Yanga kasoro ndugu yangu mmoja ndiyo Abijo.
Maalim katika kuzurura kwangu nimeokota picha ya watani zangu naiweka hapa ili kama kuna mtu anawatambua atujuze,mi nimemtambua mchezaji mmoja tuu ni khamisi Kisiwa.View attachment 380787
Rubawa,Muungwana ni vitendo na huyo ndio Alhaji sheikh Muungwana mzee wngu Mohamed Said ninaye mjua mie safi sna mzee wngu ila naomba nikupe kisa ambacho umewahi kukiandika na kunieleza mara nyingi japo sikumbuki vzuri nafikiri ilikuwa kwenye kikao cha TANU kupitasha wagombewa wao kuna mtu alimuuliza Sir George Kahama swali naweza kusema la kizushi juu Mali zake na kumfananisha na bepari lkn kwa hekima za mwalim nyerere alimkataza Sir George Kahama kujibu swali ilo kutoka na yy mwenyewe mwalim kumjua vzuri Kahama na historia yao nami pia na kuomba sna usiwe unawajibu watu wajinga wajinga na malofa km hao mzee wngu maana kwanza anaonekana ni mgeni mpili uzi unazungumzia mambo mengine na yy analeta mambo mengine unajua dunia yetu ya leo hii chizi au mwenda wa zimu sio mpk avue nguo mzee wngu nina hakika huyo kijana wenzangu Akili zake hazipo sawa
Maalim wangu jana kwenye baraza yetu nilikuwa nasimulia habari hizi za Marehemu Ayoub Kiguru jinsi ulivyomuelezea humu JF kuna mmoja wa jamaa zangu pale Barazani akaniambia hebu muulize Maalim kuwa unakikumbuka kisa cha marehemu alifungiwa kuingia uwanja wa mpira Ilala Stadium kwa sababu ya maneno lilimtoka kombora kumbe mgeni wa heshima kwenye huo mchezo alikuwa Marehemu mzee karume! Maalim wangu hebu tujuze kidogo hiki kisa.Mzimu...
Amin kwa sote.
Bahati niliyokuwanayo mimi ni kuwa nilizaliwa hapa Dar es Salaam
kwa hiyo haya yote nimeyaona kwa macho yangu mwenyewe.
Na mimi napenda kuieleza Dar es Salaam kama ninavyoijua.
Mbetini,Maalim wangu jana kwenye baraza yetu nilikuwa nasimulia habari hizi za Marehemu Ayoub Kiguru jinsi ulivyomuelezea humu JF kuna mmoja wa jamaa zangu pale Barazani akaniambia hebu muulize Maalim kuwa unakikumbuka kisa cha marehemu alifungiwa kuingia uwanja wa mpira Ilala Stadium kwa sababu ya maneno lilimtoka kombora kumbe mgeni wa heshima kwenye huo mchezo alikuwa Marehemu mzee karume! Maalim wangu hebu tujuze kidogo hiki kisa.
Maalim wangu usemacho hakina ubishi hakika Yanga na Simba ni watani wa jadi ila wapenzi wa kila timu tulikuwa na mapenzi ya dhati kwa timu zetu,bahati nzuri Barza yetu ni mseto lakini ukikuta tunavyo interact kwenye Ukwala na Uabijo ni raha tupu.Mbetini,
Nacheka peke yangu nakuomba ruksa niwageukie wanabarza niwaulize swali.
Wanabarza mmeamini kuwa Ayubu Kiguru alikuwa kibiko ya Yanga?
Mnaona huyu Yanga anavyomkumbuka katika barza yake na bila sha hiyo barza
ya watani wangu.
Kisa hiki maarufu.
In Sha Allah nitarejea.