Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #61
Guasa,Shukran maalimu kwa ufahamu unaotupatia jamvini.
Wajib...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Guasa,Shukran maalimu kwa ufahamu unaotupatia jamvini.
Guasa,Nitakuwa wakili wa chamakh kwa hili hata weye huoni kuwa uzi unanoga kwa mas ala tunayokuuliza?
Wewe mzee unapenda sana muunganiko na wafu, eti? Haya Moo kapeleka milioni 100 nenda ukasome khitma mle ubwabwa. Ujue kwa imani za watu wengine ibada za wafu ni dhambi. Mbona unakuwa ni mwenye kuchanganya kila kitu na imani yako?Kituko,
Nilichosema mimi ni kuwa wakifanya khitma na sasa hawafanyi.
Ikiwa mambo yamebadilika hapana neno mimi nimeeleza tu
historia ya Sunderland kama ilivyokuwa.
Ingekuwa Sunderland walikuwa wanasoma misa ningelisema.
Aisee kumbe ni mpenzi Wa michezo.Abunwasi,
Siku zimekwenda.
Kwenye maziko ya Abdulrahman Lukongo nilikutana na Hamisi
Kibunzi nikamweleza mazungumzo niliyokuwanayo na marehemu
Athmani Kilambo kuhusu yeye na Arthur Mambeta, Yusuf Salum
na wengineo.
Nikamwambia kuwa Yanga wakiwahusudu sana baadhi ya wachezaji
wa Sunderland na akinitajia majina.
Kilambo anasema, ''Unajua kulikuwa na watoto kule Sunderland wana
mpira mzuri sana kama Kibunzi na Arthur Mambeta na Mzee Mangara
akiwataka awalete Yanga kuongeza nguvu ulinzi na ushambuliaji...''
Kilambo anasema kuwa Mzee Mangara anatuuliza, ''Mimi nikamwabia
kuwa hawa watoto akina Kibunzi na Arthur hata tukiwaleta Yanga
hawataweza kucheza mpira huku wana mapenzi makubwa sana na
Abidjan.''
Siku zile jina lingine la Sunderland ilikuwa ''Abidjan,'' na sijui lilitokana
na nini.
Kibunzi alikuwa hana habari hizi hata chembe.
Akacheka akanambia, ''Kilambo kasema kweli sisi tusingeweza kucheza
Yanga tukipenda sana Sunderland.''
Kilambo alikuwa mzungumzaji wangu mkubwa na akijua mie siipendi
Yanga sasa yeye ikawa kila siku kuniweka roho juu.
Mechi ya Yanga na Simba Zanzibar mwanzoni 1970s, Yanga walitokea
Nigeria, basi kanifata ofisini kunitisha ananiambia, ''Tumekufanyieni
fitna kubwa Zanzibar mnachukiwa kama Hizbu.''
Kweli Zanzibar tukafungwa Yanga wakachukua kikombe.
Kilambo alikuwa muungwana akiingiliana na wachezaji wa Simba vizuri
sana na akipenda sana kumtania Emmanuel Mbele ambae akipenda
kumwita, ''Fullup.''
![]()
Waliosimama wa tatu kulia ni Athmani Kilambo, wa tano Abdulrahman Lukongo
timu ya East African Cargo Handling Services
Akijua mapenzi yangu ya mpira na alikuwa akinipa habari nyingi sana za
Yanga hadi uchawi wa kuloga mechi.
Siku za mwisho za maisha yake tukiswali pamoja msikiti wa Manyema na
akija akiniona hataingia ndani msikitini sharti kwanza aje anisalimie.
![]()
Athmani Kilambo (Yanga) kushoto na Abuu (Cosmo)
kulia kwenye khitma Saigon.
![]()
Kushoto wa kwanza mbele ni Hamisi Kibunzi, nyuma kulia wa kwanza Arthur Mambeta
anaemfuatia ni Emmanuel Mbele na wa sita ni Yusuf Salum.
Mwana,Wewe mzee unapenda sana muunganiko na wafu, eti? Haya Moo kapeleka milioni 100 nenda ukasome khitma mle ubwabwa. Ujue kwa imani za watu wengine ibada za wafu ni dhambi. Mbona unakuwa ni mwenye kuchanganya kila kitu na imani yako?
Nyiokunda,Aisee kumbe ni mpenzi Wa michezo.
Hebu siku moja tujadili UJASIRIAMALI, UCHUMI na mengineyo nje ya hitima angalau nikukumbuke kwa picha ingine. Hitmaaa hitmaaa, unakaa karibu na makaburi pengine saa zote unawaza wafu?Mwana,
Mbona umekasirika ndugu yangu?
Hili kuna mtu kalieleza na limeeleweka.
Guasa,
Juma Chogo, ''Mluya'' jitu la Kenya.
Napenda mpira tu
Tip nzuri sana hii, nina uhakika watakuwa wanapita pita hapa na watazifanyia kazi..Chamack,
Ikiwa Clouds wanataka khasa wasikie maajabu na kipindi kinoge
wamtafute Captain Malik.
Huyu mtu ana ''photographic memory,'' anaweza kukutajia hadi
list ya wachezaji wa Sunderland na Yanga na nani aliumia akatoka
nani kaingia magoli yaliyofungwa na wafungaji wake nk. nk.
Au mtu mwingine ni Juma Mnonji yeye ni shabiki mkubwa wa Simba.
Hawa mimi nikikutananao huwa napiga goti kusoma kwao.
Hawa mimi wamenishinda kwa kuwa nyakati zile hawa walingiliana na
club moja kwa moja.
MS ni mwandishi mzuri sana.. Kama kuna kitabu kuhusu historia kama hizi .. Naomba nipewe details na location hakika nitaenda kukinunua..Aisee mzee MS shukran sana. Na hii historia umeiandika mahala??
Namaanisha ujitahidi uiweke katika kumbukumbu ya maandishi. Wewe ni hazina unajua mengi sana kuhusu Jiji la mzizima. Kudos baba. Na allah akupe maisha marefu
kuna huyu mzee anaitwa Abdu Mteketa,anadai kachezea simba ilipocheza nadhani na yanga Zanzibar baadaye kachezea Pan ya dar es salaam-huyu wamjua au anafurahisha barazaNyiokunda,
Napenda mpira tu.
Jackline,kuna huyu mzee anaitwa Abdu Mteketa,anadai kachezea simba ilipocheza nadhani na yanga Zanzibar baadaye kachezea Pan ya dar es salaam-huyu wamjua au anafurahisha baraza
kuna huyu mzee anaitwa Abdu Mteketa,anadai kachezea simba ilipocheza nadhani na yanga Zanzibar baadaye kachezea Pan ya dar es salaam-huyu wamjua au anafurahisha baraza
Majibu yako yameishia njiani muungwana jaribu kutizama vizuri kama hutojali utume tena.Guasa,
Sunlight Cup kikombe hiki kikishindaniwa na majimbo tisa ya Tanganyika.
Timu kali zilikuwa
Saint,
Historia hii sijaiandika.
Imekamilika.Majibu yako yameishia njiani muungwana jaribu kutizama vizuri kama hutojali utume tena.