Yanga ya AHSANTE KOTOKO: baba watoto Kilambo Athumani akiwa na beki Kapera na Boi Wickens wanapaki bus nyuma; GOALKEEPER Elias Michael na Centre half wao Abdulhaman Juma. Hiyo ndio Yanga ya Mangara Tabu!!!
Ndinani,
Abdulrahmani Juma hakuwa ''centre half,'' watoto wa mjiini wakiita
''mkoba.
''Yeye alikuwa akicheza mbele na Yanga wakimuita ''Bwana Fedha.''
Abdulrahmani alikuwa na ''gentleman player,'' ''excellent ball control.''
Sasa pale katika alikuwa akigawa mipira kila mahali kama vile ''cashier,''
anavyolipa fedha ndiyo wakampa jina hilo.
Yanga hawakuwa na staili ya kuzuia lango yaani, ''kuegesha basi.''
Yanga walikuwa na wachezaji hodari wa kufunga kama
Maulid Dilunga.
Kilambo kwa kuwa alikuwa more ''flamboyant,'' na mpira akiweza kuuchezea
yeye alikuwa ''stopper,'' akicheza mbele ya
Kapera kwa kuwa Kapera
alikuwa ''stiff player.''
Kwa ajili hii
Kapera akawa, ''swipper,'' yaani akipitwa Kilambo ''striker,''
atakutana na
Kapera.
Hii staili wakiita ''double centre half'' yaani ''stopper na sweeper.''
Ndiyo maana Yanga walikuja kupata tabu sana kuwasinda Simba enzi za
Abbas Dilunga na
Willy Mwaijibe kwa kuwa walikuwa wanashambuliwa
kutoka pembeni na ma ''winger,'' wenye mbio na wepesi.
Nitakuambia kitu ujue vipi Allah anawapa watu nema zake.
Huwezi amini lakini juu ya kuwa Kilambo alikuwa hana elimu ya sekula
lakini alikuwa hodari wa kujifunza maneno ya Kiingereza khasa yanayohusu
mpira.
Nimejifunza mengi kutoka kwake.
Yeye ndiye akinieleza tofauti ya ''placing,'' na ''shooting.''
Alikuwa akinambia, ''Mwambieni
Sabu si kila mahali ni ''shooting,''
mmetukosa kutufunga kwa ajili mipira mingi ambayo angefanya placing
yeye ana shoot inakweda juu. Ile mipira ange-place yote yale magoli.''
''Hapakuwa na haja ya ''lobbying,'' pale. Yeye angepiga kweye ''box.''
Kilambo alikuwa ''sportsman,'' wakati mwingine baada ya Simba na Yanga
bila kujali matokeo yeye atafanya uchambuzi wake wa mechi.
Utamsikia anawalaumu Simba anasema, ''Nyinyi Simba mechi ya jana ndiyo
mmeiharibu.
Hivi yule Bobeya mnampangia nini?''
Bobea alianza kama mlinda malango Zanzibar kisha akaja Simba kama
''centre half,'' lakini yeye akitumia nguvu sana uchezaji wake.
Kilambo atasema, ''Pale nyuma wangekuwa
Arthur na
Kibunzi mpira
ungekuwa mzuri sana jana.''
Kilambo hata alipokuja kuwa mwalimu wa mpira baada ya kustaafu soka
timu yake akiifunza kucheza staili ya
Kibrazil.
Ulikuwa ukiongea na
Kilambo unastarehe.
Utoto wake alikuwa Bagamoyo akivua samaki.
Akikupa strori za uvuvi utashika mbavu.