Marehemu Ayubu Kiguru: Shabiki mkubwa wa Sunderland football club miaka ya 1960

Marehemu Ayubu Kiguru: Shabiki mkubwa wa Sunderland football club miaka ya 1960

Ahasante Mohamed kwa kutukumbusha mambo ya zamani. Katika picha hiyo waliosimama nyuma wa kwanza kulia ni marehemu Maulid Dilunga; Akifuatiwa na Hassan Gobos; wa nne ni Kitwana Manara. Waliochuchumaa kulia kabisa ni CHUMA na kushoto kabisa ni MSOMALI!!!
Nidhani,
Dilunga
tukifahamiana vyema na alikuwa mzugumzaji wangu
ingawa hakuwa na ''eloquence,'' ya Kilambo.

Dilunga aka DDT.
Dilunga Dangerous Ten!
 
Dilunga aka DDT.
Dilunga Dangerous Ten

Yanga ya AHSANTE KOTOKO: baba watoto Kilambo Athumani akiwa na beki Kapera na Boi Wickens wanapaki bus nyuma; GOALKEEPER Elias Michael na Centre half wao Abdulhaman Juma. Hiyo ndio Yanga ya Mangara Tabu!!!
 
Guasa,
Kisa hiki sikijui lakini Haji Lesso nikimfahamu hakutokea Zanzibar.
Lesso alikuwa striker hatari sana na akiutumia urefu wake vizuri sana.

Huyo wa tatu kulia ndiye Haji Lesso nadhai kwao ni Kondoa au Singida.

6Gdrm2VchKJ1uLXl3psqWm2p0KYv9SroHy-S7mzLDVIsz-C3u5IYsOR4mNFnbvJyXz9XWQK9Mkz3rBE9w_OkZK5leGYck7jGYwoGBCvis7g8lZkjlKw4GHmwMcxrmNnHZtqOxdE5c-hso8LMQINH96LDBWVGVcv6PfLdYOilwBvShpRwTCUKzK_QSwxa8BgK9CDT3stzMSx_SlLKMAE4Eu7T81HQ0WHL7HHkA6zcVTN87ZDj2Ehx4oQV5asFEk4HNwFQmb1XbQ9owaF4kYKQvimxmOnWByyxbmFdWpcBasGf0H3ijZckwEi0b3Quaxo2YIpnhLr6AFOIet6CCgMceIFCvXA5xzxqmtxlrbdJeI3WHaJ8Wl8msN4jhkdRU319rV5zxxk71K7w5R9-Vu2DqC2NDXKqaoxDbIO4KGeiYQ81nZ3avQUjOVzM67Vk4720rsbYUio0Ze7-LH9WOtEwlJ1uvbbjSSQww8cNgGowz8DBRv75a8u1LynG3IZGZjXktHEBK_e3FSAGb6_U-6OrgzjMKuk12e_1CpfM4U4g90rxg47ubzIQ75YNO1HMJ1ie6OC_dFIWRZ35PX70bf2Re4doW7toONs=w986-h657-no
Shukran na kisa hiki kuna mtu alinielezea kuwa baada ya kuonyeshwa aende msimbazi baada kama ya wiki kukawa na mechi na Haji leso akawa ndio muuwaji wa Yanga sasa wale wazee waliompeleka huko wakaanza kulaumiana kuwa weye ndio ulimpeleka huko.
 
Yanga ya AHSANTE KOTOKO: baba watoto Kilambo Athumani akiwa na beki Kapera na Boi Wickens wanapaki bus nyuma; GOALKEEPER Elias Michael na Centre half wao Abdulhaman Juma. Hiyo ndio Yanga ya Mangara Tabu!!!
Boi ndio kifupi cha boimanda?
 
Ok ndio maana nimeweka alama ya kuuliza ahsante sana maalimu wangu.
Guasa,
Mimi a Boi tumepata kazi East Africa Cargo Handling siku moja.
Check No. ya Boi Iddi ni 41 - 6241 yangu 41- 6242.

Sijui kama ile Boi ni Boimanda.
Hii Wickens ni ''nickname,'' yake.

hGe9HtLNYarjGzopFnmuyEuG-P3rXOQJPrrbsSFy_sNCvZgNttqWeFBcjIRYR1AN1xG3g8r3-6I=w891-h600-no

Kushoto: Boi Wickens, Capt. Maliki, Emmanuel Mbele na Khalid Abeid

Wakati ule kila kijana wa Kidaresalaam alikuwa na nickname.

Kitwana aliyekuwa akicheza Cosmo yeye alikuwa ''Douglas,''
kachukua jina la actor Kirk Douglas.

Kulikuwa hapo hapo Cosmo na Hamisi ''Brando,'' kutokana na
actor Marlon Brando.

Jamil Hizam (Cosmo) yeye alikuwa Denis Law kutokana na
mchezaji wa Uingereza.
 
Guasa,
Mimi a Boi tumepata kazi East Africa Cargo Handling siku moja.
Check No. ya Boi Iddi ni 41 - 6241 yangu 41- 6242.

Sijui kama ile Boi ni Boimanda.
Hii Wickens ni ''nickname,'' yake.

Wakati ule kila kijana wa Kidaresalaam alikuwa na nickname.

Kitwana aliyekuwa akicheza Cosmo yeye alikuwa ''Douglas,''
kachukua jina la actor Kirk Douglas.

Kulikuwa hapo hapo Cosmo na Hamisi ''Brando,'' kutokana na
actor Marlon Brando.

Jamil Hizam (Cosmo) yeye alikuwa Denis Law kutokana na
mchezaji wa Uingereza.
Guasa,
Mimi a Boi tumepata kazi East Africa Cargo Handling siku moja.
Check No. ya Boi Iddi ni 41 - 6241 yangu 41- 6242.

Sijui kama ile Boi ni Boimanda.
Hii Wickens ni ''nickname,'' yake.

Wakati ule kila kijana wa Kidaresalaam alikuwa na nickname.

Kitwana aliyekuwa akicheza Cosmo yeye alikuwa ''Douglas,''
kachukua jina la actor Kirk Douglas.

Kulikuwa hapo hapo Cosmo na Hamisi ''Brando,'' kutokana na
actor Marlon Brando.

Jamil Hizam (Cosmo) yeye alikuwa Denis Law kutokana na
mchezaji wa Uingereza.
Tuambie mzee wetu nickname yako wewe ilikuwaje?
 
Shukran maalimu kwa ufahamu unaotupatia jamvini.
 
Yanga ya AHSANTE KOTOKO: baba watoto Kilambo Athumani akiwa na beki Kapera na Boi Wickens wanapaki bus nyuma; GOALKEEPER Elias Michael na Centre half wao Abdulhaman Juma. Hiyo ndio Yanga ya Mangara Tabu!!!
Ndinani,
Abdulrahmani Juma
hakuwa ''centre half,'' watoto wa mjiini wakiita
''mkoba.

''Yeye alikuwa akicheza mbele na Yanga wakimuita ''Bwana Fedha.''

Abdulrahmani alikuwa na ''gentleman player,'' ''excellent ball control.''

Sasa pale katika alikuwa akigawa mipira kila mahali kama vile ''cashier,''
anavyolipa fedha ndiyo wakampa jina hilo.

Yanga hawakuwa na staili ya kuzuia lango yaani, ''kuegesha basi.''
Yanga walikuwa na wachezaji hodari wa kufunga kama Maulid Dilunga.

Kilambo kwa kuwa alikuwa more ''flamboyant,'' na mpira akiweza kuuchezea
yeye alikuwa ''stopper,'' akicheza mbele ya Kapera kwa kuwa Kapera
alikuwa ''stiff player.''

Kwa ajili hii Kapera akawa, ''swipper,'' yaani akipitwa Kilambo ''striker,''
atakutana na Kapera.

Hii staili wakiita ''double centre half'' yaani ''stopper na sweeper.''

Ndiyo maana Yanga walikuja kupata tabu sana kuwasinda Simba enzi za
Abbas Dilunga na Willy Mwaijibe kwa kuwa walikuwa wanashambuliwa
kutoka pembeni na ma ''winger,'' wenye mbio na wepesi.

Nitakuambia kitu ujue vipi Allah anawapa watu nema zake.

Huwezi amini lakini juu ya kuwa Kilambo alikuwa hana elimu ya sekula
lakini alikuwa hodari wa kujifunza maneno ya Kiingereza khasa yanayohusu
mpira.

Nimejifunza mengi kutoka kwake.
Yeye ndiye akinieleza tofauti ya ''placing,'' na ''shooting.''

Alikuwa akinambia, ''Mwambieni Sabu si kila mahali ni ''shooting,''
mmetukosa kutufunga kwa ajili mipira mingi ambayo angefanya placing
yeye ana shoot inakweda juu. Ile mipira ange-place yote yale magoli.''

''Hapakuwa na haja ya ''lobbying,'' pale. Yeye angepiga kweye ''box.''

Kilambo alikuwa ''sportsman,'' wakati mwingine baada ya Simba na Yanga
bila kujali matokeo yeye atafanya uchambuzi wake wa mechi.

Utamsikia anawalaumu Simba anasema, ''Nyinyi Simba mechi ya jana ndiyo
mmeiharibu.

Hivi yule Bobeya mnampangia nini?''

Bobea alianza kama mlinda malango Zanzibar kisha akaja Simba kama
''centre half,'' lakini yeye akitumia nguvu sana uchezaji wake.

Kilambo atasema, ''Pale nyuma wangekuwa Arthur na Kibunzi mpira
ungekuwa mzuri sana jana.''

Kilambo hata alipokuja kuwa mwalimu wa mpira baada ya kustaafu soka
timu yake akiifunza kucheza staili ya Kibrazil.

Ulikuwa ukiongea na Kilambo unastarehe.

Utoto wake alikuwa Bagamoyo akivua samaki.
Akikupa strori za uvuvi utashika mbavu.
 
Kama alijulikana kama Douglas sasa la popat lilikujaje? na mwinda ramadhani akijulikana kama "maajabu "nae ilikuwaje?
 
Bila kusahau nickname ya mzee omar chogo ndio alikuwa mtaalamu wa hiyo chogo chemba?
 
Back
Top Bottom