Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Kamuua alafu kajisalimisha? Basi mwamba hakua mtu mbaya, ila Kuna muda ukiona kelele ndani Bora acha mali jiondokee
Wewe unadhani mwanamke anaweza kukurupuka tu kudai jina leke linandikwe kwenye hati ? Hilo ni jambo lisilowesekana asilani ,, mwanaume jipange jenga kisha oa uone kama mwanmke atataka jina lake liwekwe kwenye hati ya nyumba uliyojenga wewe ,, labda ingekuwa mwanamke jambazi amuue jamaa ili abaki na mali. Lakini kwa huyo dada mpaka kufikiria kutafuta mwana sheria na kutaka jina lake liwekwe kwenye hati 70% huenda hiyo ni mali yake kweli na jamaa akaona hataki kupoteza.
 
Sema wanawake bwana mda mwingine wanatuvuruga sana, yaani wamehamia kwenye nyumba mwaka jana tu disemba hata mwaka hawajamaliza ila tayari mwanamke anataka hati ya nyumba na kiwanja majina yabadilishwe yaandikwe yake. So sad
Ukioa mwanamke maana yake umejisalimisha wewe kama mwili na nafsi yako na chochote unachomiliki na utakachomiliki.Sasa,nini shida uanze kung'ang'ania vitu?
 
Mwanamke akiwa amenunua uwanja na amejenga nyumba kwa pesa yake, ni ya kwake. Huyo jamaa hata kama alichangia lakini nyumba ni ya Mwanamke. Huyo Mangi wa wapi, alitakiwa astuke mapema sana awe na ya kwake pembeni. Haya sasa anaishia jela na nyumba watakaa watu wengine.
 
Alinunua kiwanja halafu kikawa na majina gani kabla ya hapo mbona haisemwi? Kila sehemu unakuta ooh alitaka kubadili majina yasome lake na watoto, je kabla ya hapo majina gani yalikua kwenye hati? Nani alipendekeza majina ya awali na kwanini leo ndio akumbuke kubadili majina? Msukumo wa kubadili majina ulitokana na nini? Kwanini wkati ananunua hakuwa na msukumo huo? Andikeni uchambuzi kamili sio hizi kanjanja na takataka mnatuletea.
 
Ulivyomaliza utafikiri ulikuwepo, una uhakika mzee Laurent hakuhusika kwenye ujenzi? Kiwanja kama alinunua yeye jina la mmewe lilifikaje kwenye hati? Usihukumu kabla hujasikiliza na upande wa pili.
 
Ukitumia akili utajua wanawake niwatu wakubadilika. Anaweza kuwa mwanzo alikubali lakini sasa anaona kuna viashiria havielewi anadai chake mapema. Au wamekwanzana na migogoro mwanamke ni mapema sana kubadili maamuzi tofauti na sisi wanaume
 

Kakosa vyote sasa kwa hasira zake bila kutumia akili. Kakosa mke, kakosa kulea watoto wake, kakosa nyumba. Anaishia nyuma ya nondo maisha yake yote.

Bora hata angefanya umafia mwingine, ila kuua namna hiyo. Stori yake imesishia hapo. Hapo kesi itamalizika miaka miwili au mitatu, na jamaa atakula kitanzi au maisha jela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…