Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Hakuweka jina lake wakati ananunua, hakubadili jina wakati anajenga, anaamua kubadili jina nyumba ilipokamilika. Hapo hapo mume anashikwa na uchungu sana sababu nyumba ambayo hakuhusika kununua kiwanja wala kuijenga inabadilishwa jina lake kwenda kwa mkewe mwenye watoto wake hivyo anaamua bora wakose wote yeye aende jela mke aende kaburini.

Kuna kitu hakijasemwa.
Au nwanaume ana shida ya akili.
Mali zinatafutwa mkuu. Hata kama na yeye amechangia kumuua mama wa watoto wake kisa nyumba tu ni ubinafsi. Tatizo hawa ndugu zetu wanaabudu sana mali .
 
Hakuweka jina lake wakati ananunua, hakubadili jina wakati anajenga, anaamua kubadili jina nyumba ilipokamilika. Hapo hapo mume anashikwa na uchungu sana sababu nyumba ambayo hakuhusika kununua kiwanja wala kuijenga inabadilishwa jina lake kwenda kwa mkewe mwenye watoto wake hivyo anaamua bora wakose wote yeye aende jela mke aende kaburini.

Kuna kitu hakijasemwa.
Au nwanaume ana shida ya akili.
Kiwanja kilikuwa cha akina Jane (chake)na hakikuwa na hati.Hati ingekuwepo tangu mwanzo kusingekuwa na mayele..Nyumba ilipojengwa,mume akaandika jina lake kuleee halmashauri ambapo mke hakuwepo.Alipojua hilo ndipo kazeze ikaanza.
NB;Rule number one:Usijenge ukweni/kwa mke.
Rule number two:Mchumba hasomeshwi.
 
Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.
taratibu za kumiliki silaha zipitiwe upya, huwezi mtishia mtu chuma namna hii alafu ukaachwa kuendelea kumiliki chuma


Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.
kikawaida haya ndo maisha jinsi yalivyo, au lah majirani hawajataka kuhusika kwenye maelezo
 
Mali zinatafutwa mkuu. Hata kama na yeye amechangia kumuua mama wa watoto wake kisa nyumba tu ni ubinafsi. Tatizo hawa ndugu zetu wanaabudu sana mali .
Yes mkuu, kuua ilikuwa ni ushamba but still kama jamaa hana tatizo la akili basi kuna kitu hakisemwi kuhusu sababu halisi iliyompa hasira kwa kiwango cha bora tukose wote.
 
Ameacha watoto bila msingi wa familia na kuharibu maisha yao kwa sababu ya mali.

Mwisho wa siku, mali inabaki, lakini watoto wamebaki na jeraha.

Uamuzi wa kijinga kabisa.

Ni fala, ameua kwa kukusudia. Hapo anakula kitanzi, uchunguzi ni miaka mitatu au minne. 😊

Watoto watalelewa na babu, bibi au shangazi au vyovyote. Watakosa baba na mama na mali hiyo pia wataikosa.

Hapo kuna watu wanapanga mipango namna ya kunufaika na hiyo nyumba au kuichukua kabisa.
 
Hii issue juzi nimetoka kumwambia rafiki yangu,haya majumba na mali tunazoziona wanaohangaika kuzitafuta ni wanaume lakini mwisho wa siku wanao baki nazo ni wanawake.
Mkuu, pengine ni vizuri kujua kwanza maisha yao na walikotoka kuliko kuhukumu kwa hisia. Ngoja nikupe mfano. Kuna jamaa yangu yeye ni handsome, mtu wa totoz na kujirusha kwa sana. Miaka ya nyuma raslimali aliyokuwa nayo ni bajaji yake na kila akipata fedha zilikuwa zinaisha siku hiyo hiyo. Kwa sababu ya huduma yake ya bajaji, akaja kukutana na ''dada-mama'' mmoja jembe, sura wala umbo havivutii ila linapiga kazi hakuna mfano. Yule mama akajitahidi na biashara zake, akatafuta eneo, akajenga (jamaa alikuwa anasaidia kwa kiasi kidogo tu hasa kwenye mambo ya usafiri) wakahamia, wakapata na watoto wawili. Jamaa yangu akaanza kubadilika, akaanza kutoka na watoto wakali tena kwa kumdharau yule mke wake kabisa. Matokeo yake, ukatokea ugomvi mkubwa mpaka wa ndoa ikavunjika. Hapo utasema mwanamke alikuwa na kosa gani?
 
Sema wanawake bwana mda mwingine wanatuvuruga sana, yaani wamehamia kwenye nyumba mwaka jana tu disemba hata mwaka hawajamaliza ila tayari mwanamke anataka hati ya nyumba na kiwanja majina yabadilishwe yaandikwe yake. So sad
Maisha ya kuviziana , ndoa za sasa kia mtu ana mipango yake..Hapo , ni wanandoa ila kila mtu anaishi matumatu akijua siku moja kitanuka tu . kama mmefunga ndoa ya kuwa mwili mmoja , kuna haja gani ya mmoja kutaka kitu kijulikane ni chake pekee wakati mnaishi wote humo .

Hao wanajuana, ukisoma mchezo hapo jamaa angeonekana bwege huko migombani kama angeachia hiyo nyumba kizembe ..kaona bora wakose wote .
 
Hii issue juzi nimetoka kumwambia rafiki yangu,haya majumba na mali tunazoziona wanaohangaika kuzitafuta ni wanaume lakini mwisho wa siku wanao baki nazo ni wanawake.
Sahihi kabisa, mtu tuna watoto zaidi ya wanne napata wapi muda wa kuwaza kuanza kugombea Mali nilizotafuta mwenyewe na mwanamke wangu. Ni zake na watoto, Mimi mwanaume ni title tu ila wao ndio watumiaji Tena halali.
 
Uwenda mwanamke alisha hisi taraka, akaona apambanie mali mapema kabla hilo halijatokea.
Na pia huenda mwanamke alikuwa na genuine reason ya kutaka kuandikisha kwa jina lake. N vizuri sana kujua walivyokutana, walikuwa na nini, walichangia namna gani kwenye maendeleo yao na kilichowagombanisha ni nini.
 
Wapuuzi kibao wana silaha. Wewe huijui hii nchi?
labda za magendo na jamaa kama ilikuwa ni ya magendo angesha kamatwa kwa kuwa alishawai kushtakiwa kwa tishio la kumdhuru mwanzo na iyo silaha. na vigezo vya kumiliki silaha vipo wazi hasa kwenye umiliki wa mali kuanzia kiasi fulani. pia huangalia utimamu wa akili kabla ya kukabidhiwa. Kiufupi kinasababu ya jamaa kufanya hayo ambayo mimi na wewe hatujui zaidi ya kuishia kiskia stories za hapa na pale.

unless sijaelewa ilitaka kusema nini au unajaribu kutetea nini hasa karibu
 
Wewe unadhani mwanamke anaweza kukurupuka tu kudai jina leke linandikwe kwenye hati ? Hilo ni jambo lisilowesekana asilani ,, mwanaume jipange jenga kisha oa uone kama mwanmke atataka jina lake liwekwe kwenye hati ya nyumba uliyojenga wewe ,, labda ingekuwa mwanamke jambazi amuue jamaa ili abaki na mali. Lakini kwa huyo dada mpaka kufikiria kutafuta mwana sheria na kutaka jina lake liwekwe kwenye hati 70% huenda hiyo ni mali yake kweli na jamaa akaona hataki kupoteza.
Binamu yangu alikua akifanya kazi relwe/TRC,mkewe mama wa nyumbani,aliponunua kiwanja na kujenga,mke mara atake nyumba iandikwe jina lake mara watoto
 
Back
Top Bottom