Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Kiwanja kilikuwa cha akina Jane na hakikuwa na hati.Hati ingekuwepo tangu mwanzo kusingekuwa na mayele..Nyumba ilipojengwa,mume akaandika jina lake kuleee halmashauri ambapo mke hakuwepo.Alipojua hilo ndipo kazeze ikaanza.
NB;Rule number one:Usijenge ukweni.
Rule number two:Mchumba hasomeshwi.
Jina la nyumba/kiwanja halibadilishwi kienyeji hivyo
 
Sema wanawake bwana mda mwingine wanatuvuruga sana, yaani wamehamia kwenye nyumba mwaka jana tu disemba hata mwaka hawajamaliza ila tayari mwanamke anataka hati ya nyumba na kiwanja majina yabadilishwe yaandikwe yake. So sad
Kwani shida nini Buddha? Unabadirisha tu maisha mengine yanaendelea kwani shida nini mpaka muuane?
 
Tukio la kushtua limetokea Mtaa wa Senzele, Kata ya Bunju B, jijini Dar es Salaam, baada ya Laurent Kweka kudaiwa kumuua mkewe, Jeni Urassa, kwa kumpiga risasi kichwani kisha kujisalimisha Polisi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.

Kwa mujibu wa Mafwele, Laurent na marehemu walikuwa wanandoa na wote walitoka mkoani Kilimanjaro. Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.

Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.

Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.

Marehemu ameacha watoto wanne, watatu wakiwa shuleni na mmoja bado hajaanza shule.
Chanzo : Global

Vijana tuache kulazimisha mambo tufanye kazi tusing'ang'anie mali za wanawake
Uwongo mwingi muwe hata mnaona aibu, km kiwanja alinunua huyo Jeni Urassa majina ya Laurent Kweka yaliingiaje kwenye mkataba? Alinunua wakati gani kabla ya ndoa? Ndani ya ndoa? Msiifanye hiyo issue km siasa za chadema na CCM, jamaa mwenyewe ameshasema ameshamaliza kazi nyie ni kina nani mna maslahi gani kuokoteza kila uwongo huko mitaani? Ninachokiona ni upande wa mke kujenga mazingira ya kutaka kuchukua hiyo nyumba na watoto ndiyo maana wanang'ang'ania kumzika kwao. Wachaga wanaendekeza sana njaa hawaonagi hata haya!
 
Huyo mpuuzi anyongwe tu...
Mwanamke umezaa naye watoto watatu, tena bado wadogo unamuua kisa nyumba kweli? Kwanini usimuachie hio nyumba uchukulie tu ni mali ya watoto..?

Hilo jamaa ni lijinga...
Ili mchepuko wake uje kulala kwenye nyumba niliyoitolea jasho na damu,ambinue kikukundu juu mama watoto kwenye kitanda nilichonunua ndani ya nyumba niliyojenga,huyo shaba kastahiki, watoto isiwe kigezo cha kuumizana roho na msongo wa mawazo
 
icho kipengele
Scenario haiwezi kukamilika kwa sababu tyr Shahid wa kwanza keshalala katika umauti,

Lkn tunaambiwa walikuwa wana mgogoro muda mrefu, seems hata hawajahamia hapo.....

Kwamba kuhamia desemba mwakajana tyr ni muda mrefu hata mwaka hawana,

Je mgogoro wao unaosemwa wa muda mrefu chanzo chake ni nn ??

Je kuna usuluhishi ulitafutwa kuhusu mgogoro wa wanandoa hao ??

House girl anaelezea upande wa movement za muda mfupi tungepata kusikia toka alivvyoingia aliwakuta je kina babanguuuu

Jane inaonyesha alishawahi kutishiwa kuuawa je aliripoti mahala popote kwa usalama wake ?

Mwanasheria aliyetafutwa na Jane siku chache nyuma walizungumza nn hasa ?

Wengi wanamnyooshea bibiye kidole kwa kusema anataka nyumba sjui mali kwamba haiwezekani mwanamke kununua kiwanja?? Kinachowashinda ni kutokujua kutumia akili na hisia kumpenda mtu haikufanyi uandike majina yake kisa tuu kumfurahisha....

Nina mfano halisi ulitokea makongo juu hvhv kwenye mgogoro wa wanandoa kiwanja ni cha mwanamke majina ni yanasoma mwanamke, anaejenga ni wote wawili!!!

Nakulilia Jane Urassa wa lyamungo sinde cc secretarybird mwenyekiti wa kwa Urassa
icho kipengele cha nne ndo msingi haswaa
 
Maisha ya kuviziana , ndoa za sasa kia mtu ana mipango yake..Hapo , ni wanandoa ila kila mtu anaishi matumatu akijua siku moja kitanuka tu . kama mmefunga ndoa ya kuwa mwili mmoja , kuna haja gani ya mmoja kutaka kitu kijulikane ni chake pekee wakati mnaishi wote humo .

Hao wanajuana, ukisoma mchezo hapo jamaa angeonekana bwege huko migombani kama angeachia hiyo nyumba kizembe ..kaona bora wakose wote .
Ndoa bila kuaminiana ni mzigo wa gunia la misumari. Ndoa ikashakuwa na mipango ya siri, malengo ya siri, mapato ya siri, maneno ya siri (mume vs mke) ni kama mtu na koboko kuishi chumba kimoja. Hili la tatizo la kutojua next move ya mwenza wako ndiyo huleta mapambano kama haya.
 
Tukio la kushtua limetokea Mtaa wa Senzele, Kata ya Bunju B, jijini Dar es Salaam, baada ya Laurent Kweka kudaiwa kumuua mkewe, Jeni Urassa, kwa kumpiga risasi kichwani kisha kujisalimisha Polisi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.

Kwa mujibu wa Mafwele, Laurent na marehemu walikuwa wanandoa na wote walitoka mkoani Kilimanjaro. Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.

Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.

Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.

Marehemu ameacha watoto wanne, watatu wakiwa shuleni na mmoja bado hajaanza shule.
Chanzo : Global

Vijana tuache kulazimisha mambo tufanye kazi tusing'ang'anie mali za wanawake
Nimeona comment nyingi humu wengi wakifika kwenye conclusion na kumuhukumu mwanaume,sisi wanaume tunaficha mengi sana tunayotendewa na hawa wanawake.
Mnapambana mda mrefu kutafuta Mali,Pamoja siku mnazipata mwanamke ndo analeta mizinguo,unaweza kuta huyo mwanamke kapata serengeti boy wake kamshauri akamfosi mume wake wabadilishe umiliki wa Mali,au hata ndugu wa mwanamke wanachangia hapo.
Mwanaume akishakuwa na watoto zaidi ya 2 huwa anatulizaga wenge na kufocus na maisha,siku zote mwanaume akipata pesa anawaza kuboresha maisha yake na familia yake,lakini kwa mwanamke ni tofauti yeye anawaza haishi mwenyewe ndo maana mtaani single mama wengi sana.
Wanaume wenzangu ukiona ndani ya nyumba kuna migogoro mingi ni Bora kujiondokea kivyako,kuna msemo huwa wazee usema watoto ni wa mwanamke,ata upambane vipi mwanaume mwisho wa siku watoto watasema nani kama mama .
 
Uwongo mwingi muwe hata mnaona aibu, km kiwanja alinunua huyo Jeni Urassa majina ya Laurent Kweka yaliingiaje kwenye mkataba? Alinunua wakati gani kabla ya ndoa? Ndani ya ndoa? Msiifanye hiyo issue km siasa za chadema na CCM, jamaa mwenyewe ameshasema ameshamaliza kazi nyie ni kina nani mna maslahi gani kuokoteza kila uwongo huko mitaani? Ninachokiona ni upande wa mke kujenga mazingira ya kutaka kuchukua hiyo nyumba na watoto ndiyo maana wanang'ang'ania kumzika kwao. Wachaga wanaendekeza sana njaa hawaonagi hata haya!
umeanza vizuri ila mwishoni umeharibu kuingiza ukabila🤣

umesahau wote hao ni wachaga na vijiji vyao ni pua na mdomo sawa na posta na magimeni. ivyo epuka prejudice na kuwa biased ili sote tujifunze.
 
icho kipengele
icho kipengele cha nne ndo msingi haswaa
Hii ishu ya nyumba inawekwa tuu kuna kitu kilikuwa nyuma ya pazia ila hakiwekwi wazi hapa.....

Kwenye ndoa mnang'ang'ania vipi Mali ikiwa mna watoto tyr ?? kama sio upungufu wa akili

Kwa upumbavuu wao wahanga ni madogo janja aseeh....
 
Ndoa bila kuaminiana ni mzigo wa gunia la misumari. Ndoa ikashakuwa na mipango ya siri, malengo ya siri, mapato ya siri, maneno ya siri (mume vs mke) ni kama mtu na koboko kuishi chumba kimoja. Hili la tatizo la kutojua next move ya mwenza wako ndiyo huleta mapambano kama haya.
Ndoa za siku hizi ndivyo zilivyo hasa upande wa mwanamke,ni escape route tu moyoni ana lake,huu ugonjwa hadi wanawake watu wazima
 
Hii ishu ya nyumba inawekwa tuu kuna kitu kilikuwa nyuma ya pazia ila hakiwekwi wazi hapa.....

Kwenye ndoa mnang'ang'ania vipi Mali ikiwa mna watoto tyr ?? kama sio upungufu wa akili

Kwa upumbavuu wao wahanga ni madogo janja aseeh....
Kung'ang'ania mali ipo mkuu,tena nimeona kwa mwanamke 60yrs,kapata kiinua mgongo karudi kwao na hati ya nyumba aliyojenga mumewe,yeye akaenda Jenga nyingine huko kwao
 
Back
Top Bottom