Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Amejisalimisha! Ila madhara ya kesi ya mauji hayajui!
Hapo hana tena nyumba,ni maskini kuliko wasio na nyumba,watoto ni yatima sasa! Akirudi kutoka magereza ni mwaka 2050 hana meno wala haoni
Kujisalimisha Polisi ni aina ya kuchanganyikiwa.

Kwani alisikia kutafutwa na Polisi ni kosa kisheria?

Kujisalimisha lazima afike pale na kuanza kuropoka 'nimeua', kuchukuliwa maelezo na kusainishwa!

Na hakuna ushahidi wenye thamani kama hayo maelezo ya awali ambayo mtu unayatoa huku umepaniki.

Unapofanya tukio, kimbia ili Polisi wafanye kazi yao.

Kujisalimisha au kukiri kosa haraka haraka hakukupunguzii adhabu.
 
fwatilia vigezo vya kumiliki silaha na wala siyo mpaka uwe na billions of money.ila elewa jamaa alikuwa anamiliki kihalali na alikuwa na mzigowa kiasi aliobarikiwa na Mungu. Ndo mana mpaka sasa hujaskia kuwa alikuwa akimiliki silaha kiholela.
Wala sijasema anamoliki kiholela. Nakwambia hivi watu wengi wa hovyo wanamiliki silaha kihalali tu labda huijui Tz.
 
Manamake ya kichaga huyajui,huko machame nyumba nyingi zinamilikiwa na wajane,wazee waliuawa kwa mashoka,visu mitaani,au kisukari
na ninashangaa kwamba Kweka ambaye ni mmachame alishindwaje kujua namna ya kudeal na hii issue ya kugombania mali za ndoa na hasa ukizingatia mkewe naye ni mchagga kwa hiyo alijua kabisa kabla hata hawajaoana juu ya msimamo wa mali kwa kuzingatia historia ya kabila lao ambayo ipo mamia ya miaka.
 
Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.
Huyu anatoa wapi moral authority ya kuongelea haya mambo. Tanzania mnapenda sana masikhara yanayoiingiza nchi kwenye laana
 
Watoto hapo kwa usimamizi wa watu wazima,ndipo familia ya mke inaposhika bango, maana wakipewa wao dhamana ya kusimamia watoto basi ghorofa litakua chini yao, watoto wataishi nao kwenye vibanda vyao, ghorofa watapangisha au hata kukopea
Ndiyo mpaka ndugu wawe na roho hiyo sasa

Ova
 
Alinunua alitoa wapi fedha ndani ya ndoa na kuweza kununua yeye mwenyewe bila mume wake? Au alikuwa Anadanga?
May be alikuwa nacho kabla ya kuolewa

All in all,kwann hakikuwa na jina lake tangu mwanzo ?na kilijuwa na jina la nani?
Au labda kilikuwa na majina yao wote akataka kuondoa jina ka mume na kuweka ya watt?
Aisee maswali ni mengi
 
Ukitumia akili utajua wanawake niwatu wakubadilika. Anaweza kuwa mwanzo alikubali lakini sasa anaona kuna viashiria havielewi anadai chake mapema. Au wamekwanzana na migogoro mwanamke ni mapema sana kubadili maamuzi tofauti na sisi wanaume
Exactly ukute aliona mume kabadirika
Na yeye hayuko tayari kuacha watt wahangaike
 
Ni ninyi tu.Uliwahi kusikia wapi mke wa mtu aitwaye "Mkegani" ,mzaramo anagombea mali?Au akina Chiza wa Kigoma,Kumshindwi wanagombea nyumba? Most cases ni ninyi akina arawa.Hebu badilikeni aisee!
Hapa watu wana commit logical fallacies mbili kwa wakati mmoja.

1. Hasty generalization - kuhitimisha na kuhukumu mambo kwa kutumia mfano mmoja au michache sana.

2. Ad Populum (Bandwagon) - kuamini kuwa mnachokisema ni kweli kwakuwa kundi kubwa la watu linaamini kuwa ndio ukweli.

Ukweli ni kuwa haya mambo hutokea sana kila mahali hata nje ya Tanzania lakini imekuwa kasumba ya kuwa exaggerated pale tu panapoonekana jina la kichagga.

Badilikeni bwashee.
 
Back
Top Bottom