Marehemu Jane ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga, alitaka jina lake liwe kwenye hati

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.
Huyo ni mfanyakazi wa ndani au msemaji wa familia? Huyo alipaswa kuongelea mauaji yalivyofanyika kwa kadili ya alivyoyashuhydia. Hayo ya mgogoro wa muda mrefu, na nani alinunua Kiwanja yeye yanamhusu vipi? Anafahsmu nani alitoa hizo hela za kununuliwa Kiwanja? Mbona amejipa mamlaka ambayo hana?
 
Pamoja na kwamba sitaki kuhukumu, Maisha ya ndoa yana changamoto sana
Mnaweza kuingia kwenye Ndoa mtu anakulazimisha mjenge kwenye kiwanja chake, kumbe yeye ana agenda ya siri...
Nafikiri wala siyo kulazimisha, katika hali ya kawaida kabisa kwa kuwa tayari ni wana ndoa na mmoja anamiliki kiwanja ni kawaida kabisa na ni rahisi kuanza ujenzi kwenye hicho kiwanja.

Sema nini, wanawake mara nyingi wanaendeshwa na hisia/hasira ina sababisha watoe maneno ambayo mtu ukikaa ukatafakari unaona hapa hakuna future.
 
Inabidi akutane na matokeo ya kosa lake la kukusudia.

Kama ni kweli aliwahi kusema "ipo siku ntakupiga risasi" basi ni mauaji ambayo aliyapanga.

Sioni ubaya wa jamaa kunyongwa au kifungo cha maisha.

Mkuu sheria upo wazi, huyo mkali hapo lazima atalipa maisha ya mtu kayakatisha. Hapo tayari mambo yashaharibika. Sema siku hizi kesi kama hizi hazikawii sana, zamani hapo angekaa hata miaka 10, anasubiri hukumu. 😁
 
Tukio la kushtua limetokea Mtaa wa Senzele, Kata ya Bunju B, jijini Dar es Salaam, baada ya Laurent Kweka kudaiwa kumuua mkewe, Jeni Urassa, kwa kumpiga risasi kichwani kisha kujisalimisha Polisi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.

Kwa mujibu wa Mafwele, Laurent na marehemu walikuwa wanandoa na wote walitoka mkoani Kilimanjaro. Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.

Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.

Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.

Marehemu ameacha watoto wanne, watatu wakiwa shuleni na mmoja bado hajaanza shule.
Chanzo : Global

Vijana tuache kulazimisha mambo tufanye kazi tusing'ang'anie mali za wanawake
Kwani Ile Sheria ya wanandoa Mali walizichuma wakiwa pamoja ni za wote ilishafutwa?
 
Hapa watu wana commit logical fallacies mbili kwa wakati mmoja.

1. Hasty generalization - kuhitimisha na kuhukumu mambo kwa kutumia mfano mmoja au michache sana.

2. Ad Populum (Bandwagon) - kuamini kuwa mnachokisema ni kweli kwakuwa kundi kubwa la watu linaamini kuwa ndio ukweli.

Ukweli ni kuwa haya mambo hutokea sana kila mahali hata nje ya Tanzania lakini imekuwa kasumba ya kuwa exaggerated pale tu panapoonekana jina la kichagga.

Badilikeni bwashee.
Tumebadilika mmeku!Na,tunataka twende nanyi pamoja.Ni kuwa-challenge tu.Hamna baya!
 
Kwa ndoa hizi za sshv???
U must be kidding
Huko ndoani kila 1 kakaa kimtego tu, aba plan b...
Hata ndoa za miaka ya nyuma yalikuwepo ni vile wanawake walifanywa kuwa watumwa na kutokuruhusiwa kusema yanayowakumba

Kwahiyo hakuna ndoa ya sasa wala zamani ishu ni wakati tuu mkuu...

Kweka kazingua ngoja tuende kwanza machame
 
Mali nn kuna miamba washaacha wake zao na wamewaachia majumba magari maana si mmezaa
Bwana mna watoto

Ova
Tumeumbwa tofauti. Kuna baadhi ya wanaume hawakubali , wanaweka ushindani na wanawake as if ni jinsia moja, hawataki kukubali yaishe, hawawezi kuvumilia maneno machafu na ya kuudhi toka kwa wake zao.

Dunia tunapita
 
Wala sijasema anamoliki kiholela. Nakwambia hivi watu wengi wa hovyo wanamiliki silaha kihalali tu labda huijui Tz.
Kama yule jamaa yangu wa sinza yule mkurya 😄
Sema walikuja mnyanganya mpk leo hawamrudishia,maana ilikuwa bar mara kaitoa kaiweka mezani
Mara kamtishia muosha magari
Waendawazim wengi watu ambao hawajui kumiliki na kukaa na silaha ni wengi sana

Ova
 
Tukio la kushtua limetokea Mtaa wa Senzele, Kata ya Bunju B, jijini Dar es Salaam, baada ya Laurent Kweka kudaiwa kumuua mkewe, Jeni Urassa, kwa kumpiga risasi kichwani kisha kujisalimisha Polisi.

Tukio hilo linadaiwa kutokea Alhamisi, Oktoba 1, 2026, majira ya saa 11:30 alfajiri ndani ya nyumba ya wanandoa hao. Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Faustine Mafwele, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa anashikiliwa kwa ajili ya upelelezi.

Kwa mujibu wa Mafwele, Laurent na marehemu walikuwa wanandoa na wote walitoka mkoani Kilimanjaro. Ameongeza kuwa baada ya uchunguzi na taratibu za kisheria kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Mfanyakazi wa ndani wa familia hiyo, Rebecca Mbasha, ambaye amefanya kazi nyumbani hapo kwa miaka minane, amesema mauaji hayo yanadaiwa kufuatia mgogoro wa muda mrefu wa kifamilia kuhusu umiliki wa nyumba.

Rebecca amedai Jeni alikuwa akitaka kubadili majina yaliyokuwa kwenye hati ya nyumba ili kubakiza jina lake na la watoto wao, akieleza kuwa yeye ndiye aliyenunua kiwanja na kujenga nyumba hiyo.

Amesema siku ya tukio Laurent aliingia nyumbani na baada ya muda mfupi alimsikia Jeni na baadaye akasikia kishindo. Aliporejea ndani, alimkuta Laurent akitoka chumbani akiwa ameshika bastola na kumwambia, “nimeshamaliza kazi.” Rebecca alipokwenda chumbani alimkuta Jeni akiwa ameanguka chini akiwa na jeraha kichwani.

Kwa upande wake, Jacqueline Nkaya, ambaye ni mama mdogo wa marehemu, amesema wanandoa hao walikuwa na mgogoro wa muda mrefu na wakati mmoja Jeni aliwahi kutishiwa kuuawa kwa bastola na mumewe, jambo aliloliripoti Polisi.

Amesema Laurent aliondoka na kwenda Kilimanjaro ambako alikaa takribani miezi miwili kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya tukio.

Majirani wamesema hawakuwa na taarifa za migogoro hiyo, wakieleza kuwa familia hiyo ilikuwa ikionekana kuishi kwa amani tangu ilipohamia katika nyumba hiyo Desemba 2025.

Marehemu ameacha watoto wanne, watatu wakiwa shuleni na mmoja bado hajaanza shule.
Chanzo : Global

Vijana tuache kulazimisha mambo tufanye kazi tusing'ang'anie mali za wanawake
Ukinunua kiwanja jina linaandikwa lako kwenye hati ya manunuzi,Why hakuandika jina lake? Mwanamke muongo huyu
 
Back
Top Bottom