Marehemu kutokwa na jasho !

Marehemu kutokwa na jasho !

Kama mlimuweka mochwali basi baridi inayeyuka kama vile unavyotoa soda kwenye friji ikikaa baada ya muda inatoa jasho

hili ndo jibu. wakati mwingine lazima kuwepo na leso kufuta jasho hilo ili waagaji wamuage vizuri
 
huyo alichomwa sindano ya sumu angalia sana hospital hizo maana mimi mwenyewe yalishanikuta kuna madaktari wengine wakiona mgonjwa hawezi kupona wanamuondoa kiaina au kuna kamchezo ka mali
 
Sasa ndugu, na wewe uliondolewa kwa sindano ya sumu?
huyo alichomwa sindano ya sumu angalia sana hospital hizo maana mimi mwenyewe yalishanikuta kuna madaktari wengine wakiona mgonjwa hawezi kupona wanamuondoa kiaina au kuna kamchezo ka mali
 
  • Thanks
Reactions: Paw
Ndugu, yaani kila nikiona comment zako, wewe ni;
Interesting........,
Anzisha uzi kisha uwe na maudhui ya neno moja tu, 'interesting' watu watiririke na mawazo! Just kiddin!!
Lol!

bosi kichefuchefu uyo usimgasi
kidding me too mweh!
 
Ni hali ya kawaida sana maiti kutoa jasho kwani mimi nimeshuhudia mara nyingi sani hiyo inatokana na kuwekwa kwenye frige mda mrefu au kuchomwa madawa ya kuzuia mwili kuhalibika kwa wingi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Ndugu yangu alifariki baada ya kusumbuliwa na malaria na shinikizo la damu kwa muda mfupi. Daktari alithibitisha kuwa amefariki dunia na akaandika death certificate. Lakini cha kushangaza, wakati wa kuagwa na ndugu na marafiki nyumbani kwake, marehemu alikuwa anatokwa jasho usoni. Hii maana yake nini wajuzi??

Mkuu hii mada uliyoleta ni very interesting!

Swali la kwanza la kujiuliza je kifo ni nini?

Bado hakuna definition iliyonyooka na kuridhisha kwa makundi yote ya kijamii.

Kifo ni nini basi....
Ni kuondokewa kwa uhai wa kile kilichokuwa kinaishi.

Kisayansi kifo sio tukio la ghafla bali ni safari ya kuondokewa kwa uhai.seli na tishu mbalimbali za mwili hupoteza uwezo wake wa kufanya kazi au kuishi katika spidi mbalimbali.

Hapa kuna utata unaotokea kuhusu ni wakati gani hasa kifo hutokea?

Na kupelekea kuwe na aina mbili za kifo

1-Kifo cha selihai(cellular level)
Hapa seli na tishu zinapoteza uwezo wa kufanya kazi ama kuishi na hivyo kushindwa kutumia oksijeni na hatimaye zinaanza kujivunjavunja na kuoza.ikiwa jambo hili litahusisha seli za mwili mzima basi hiki ni kifo.

selihai hufanya kazi tofauti na spidi ya kufa huwa tofauti labda kwenye tukio ambalo litaharibu seli zote kwa wakati mmoja kwa mfano mlipuko wa nyuklia.

selihai za ngozi au mifupa huweza kuishi masaa mengi kulinganisha na selihai za ubongo zinazochukua madakika tu baada ya mtu kuonekana "amekufa"

2-Kifo cha kimwili(somatic death)
Hapa mwili unapoteza uweza wa kuwasiliana na mazingira na pia unakuwa haujitambui na kupoteza sifa za uhai.

Hivyo kwa ufupi kumjibu mleta mada ni kuwa ni kweli inawezekana kuwa ndugu yako alikuwa yuko kwenye process ya kifo na hivyo kumuona akiendelea kutoka jasho(sisemi mlimzika akiwa hai)

Cha msingi ninachokiona ni kwamba daktari,ndugu,jamaa na marafiki wakikubali kuwa mtu huyu amefariki basi hakuna wa kupinga.

Nadhani nitakuwa nimekufungua kidogo kuhusu possibility ya kuona jasho au hata movement kwa mtu aliyehesabika 'amekufa'

Kwa hisani ya vitabu mbalimbali.
 
Huyo walimpeleka mochware chukulia mfano Maji nyama ukiiweka kwenye friji ukiitoa hutoa majimaji inayoonesha ya kuanza kuyeyuka hyo wala sio jasho
 
naona wengi mmejibu kisomi na kutaka kujifanya eti hamjui mambo ya kiswahili (ushirikina) kwa mimi naelewa si wote wanaokufa hufa kweli kwa swala la jasho unaweza pata mifano na maelezo mengi ila kuna marehem mpaka anaenda kuzikwa bado mwili unavuja dam hii ipo na mara nyingi hutokea mtu alokufa hawez toka jasho wala kutoka dam na wengi wa namna hiyo huwa hawajafa
 
Huyo walimpeleka mochware chukulia mfano Maji nyama ukiiweka kwenye friji ukiitoa hutoa majimaji inayoonesha ya kuanza kuyeyuka hyo wala sio jasho

hujawah kuona na siku ukiona utasema maajabu uliwahi kuona au kusikia maiti kuvuja dam siku nzima
 
naona wengi mmejibu kisomi na kutaka kujifanya eti hamjui mambo ya kiswahili (ushirikina) kwa mimi naelewa si wote wanaokufa hufa kweli kwa swala la jasho unaweza pata mifano na maelezo mengi ila kuna marehem mpaka anaenda kuzikwa bado mwili unavuja dam hii ipo na mara nyingi hutokea mtu alokufa hawez toka jasho wala kutoka dam na wengi wa namna hiyo huwa hawajafa

Elezea kishirikina basi!
 
Back
Top Bottom