Basi Nenda
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 20,774
- 47,866
Muda mfupi uliopita nilikuwa nasoma habari kwenye tovuti ya The citizen kuhusu huyu mzee Njonjo ambaye aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa Kenya kwa takriban miaka 17. Kilichonivutia hasa kuhusu habari hii ni uhusiano kati ya Mwai Kibaki na marehemu mzee Njonjo. Mwandishi anadai wazee hawa waliishi mtaa mmoja lakini hawakuwahi kutembeleana wala kutazamana usoni isipokuwa wakati wa msiba wa mke wa Mzee Moi mwaka 2004.
Wazee hawa licha ya kuishi mtaa wa Muthaiga ila hata Kibaki alipofiwa mke, mzee Njonjo hakwenda kabisa. Chanzo cha ugomvi wao inadaiwa ni kwamba Mzee Njonjo alimpropose Kibaki kwa Moi alambe kiti cha Ikulu huku Njonjo akitumai kwamba Kibaki akimaliza muda wake atamuachia kiti mzee Njonjo, alipofail kufanya hivo ndipo mzee Njonjo akachukia mpaka siku anafariki.
Mwandishi anaendelea kusema wawili hawa walitofautiana hata mtindo wa kimaisha, wakati Njonjo alipenda kuogelea, Kibaki hajawahi kuvaa nguo za kuogelea maisha yake yote na anaamini kuogelea ni kwa ajili ya samaki na viumbe wa aina hiyo huku pia Kibaki akipenda kucheza golf Njonjo yeye haelewi kwanini wanaume wazima wapoteze muda wao kutazama ka mpira kadogo siku nzima😂
Mwandishi anadai marehemu mzee Njonjo alikuwa ni mnonko yani alikuwa anachomea wenzie kwa Rais Kenyatta na pia mzee Njonjo alikuwa anawadharau watu weusi sana.
W