Marehemu Roy alikuwa anajua sana

Marehemu Roy alikuwa anajua sana

Hivi Complex mpenziwe si alikuwa ni Vivian ama! au Tilya ni jina lake pia?

Roy RIP alitisha sana na G2 yake enzi hizo...yaani kina Tonya Mbili kipindi hiko walibamba sana kupitia mkono wa huyu jamaa. Kila nikisikiliza "Siamini" ya Matonya lazima inijie taswira ya huyu jamaa aise.
Imenibidi ni u download huu wimbo jana, yani bado mkali kama umetengeneza jana na ile style yake ya rthym za bass jamaa alikuwa mkali sana.
 
roy mshkaji sana wakati anafanya kazi G record pale chang'ombe alikuwa anatupigisha sana story akipita.. wakati huo sisi wadogo...

nakumbuka mpenzi wake alikuwa jirani yetu chang''ombe walifariki mfululizo hawa watu waswahili wakawa wanasema ukimwi
 
Yah watu uwa wanadai ngoma.
Sema kuna siku 20% alikuwa anahojiwa anasema kipindi hicho anaenda kwa roy kurekodi, roy anawakalisha nje kila siku anawapiga karenda ila blu akija anapitiliza mpaka ndani hata hi hawapi.
Eti 20% alikuwa anamaindi sana ila siku moja akaja mzee nature ndiye akakaa nao akapiga nao story akawa anawapa moyo kuwa watatoka
 
G - 2 ilikuwa ya kwake roy...mwanzo aliajiriwa G record ya G lover.. pale chang'ombe.. na hit song zote karibu na jina alilipatia G record.. enzi za mr blue anatoka, aby skills, alikiba, bjb, snoop lee, Enika.. wengi nilikuwa nawajua sababu nyumba yetu ilikuwa jirani na G record

G2 walitisha saaaaaaaaaaana
 
Cinderela,Nakshi Mrembo,Siamini,Mapozi,Blu blu zilikuwa nyimbo za taifa kutoka kwenye mikono salama ya Roy.
Dah nikiukumbuka huu wa Siamini wa Matonya pamoja na ule wa Mb Dogy, Mapenzi kitu gani nakumbuka mbali sana.
Ndio nyimbo zilizonifanya nikatiwa mimba miaka ile ya 2005.
Dah!
Kila nikizisikiliza nyimbo hizi, nakumbuka bikra yangu niliyopoteza kwa kwenda Club miaka hiyo kusikiliza hizi nyimbo.
R.I.P Roy ndani ya G2
 
Hahaha uliitoa au ulizaa?
 
Back
Top Bottom