Marejeo ya Historia: Mahatma Ghandi, Abraham Lincoln, Nelson Mandela na Mama Tereza waenziwe kwa utume kama Muhammad?

Hivi unafikir kuna mtu ambaye ajawai kupingwa ? Musa alikwenda kwa FARAO na miujiza lakini bado alipingwa sasa ajabu hiko wapi Mohamadi kupingwa? hizi elimu mnasoma wapi?
 
Kwa hiyo unataka kutuambia Mungu hawezi mtokea au mtuma malaika wake kama uko pangoni? au hoja yako iko wapi usaidiwe maana inaonekana pango kwako ni kitu cha ajabu kweli kweli
 
Unafahamu kama Mungu wako alikabwa mpaka akamchezea rafu mja wake? au unatoka povu tu kwa Mohammad kukabwa , badala ya kustaajabu Mungu kukabwa wewe unastaajabu mtu kukabwa, kalagha bao
 
Haya maswali uliyouliza hapa ni sawa na kuuliza kwanini wewe Mungu ajakuumba mwanamke? Jibu ni rahisi Mungu anafanya anachoona yeye kinafaa sio unachoona wewe kinafaa , ndio maana Mungu alimuacha Yohana akatwe kichwa kwa sababu aliona inafaa , au nikuulize swali kwani Mungu alishindwa kumuokoa yohana asiuliwe?
 
Hili dai ni uongo mtupu kijana , waraqah hakuwai kumpa utume nabii Mohamadi popote pale kama yupo anaeweza kuthibitisha kuwa waraqah kampa utume nabii Mohamadi karibu sana
 
"Sasa wapi amedhalilishwa ?"

Wewe huoni kwamba Muhammad alidhalilishwa? Mtu mzima na watoto waliokuwa wanamtegemea baba yao kama mlinzi Wa familia walijisikiaje kumuona Baba yao amerudi huku amelowa jasho chapachapwa?
Jasho ni maumbile , hata siku moja jasho halijawai kuwa ni udhalilishi, unajenga hoja kwa vitu vya kitoto kabisa
 
Naunga mkono hoja maana hawana tofauti kubwa na Mtume.
 
Sijawahi kujua maisha ya Mt Mohamed. Ahsante kwa hilo!
Maswali yangu yanaweza kuwa nje ya ulichokusudia.
1 Kabla ya kutokewa na maono, alikuwa dini gani?
2 Kama hata kabla ya Uislam, watu Walienda kuhiji Makka kwa kuabudu miungu mbalimbali, je hili jambo limechipukia kutoka upagani?
3 Kuna uwezekano hizi dini mbili kubwa na chimbuko moja, na kadiri muda ulivyosogea ndivyo watu wakazidi kutengana?
Ni hayo tu.
 
Kwa kuwapitia wote, naona hao wote isipokuwa Mt Mohamed, hawastahili kuwa manabii. Kwamba alikuwa akitokewa na mjumbe anayeaminika anatumwa na Mungu, ni sababu pekee ya yeye kuwa tofauti. Kuhubiri na kufundisha maelezo kutoka kwa Mungu ni tofauti na uanaharakati. Yeye Sawa yake ni Yesu.
Mahatma, Lincoln na Teresa, wanaweza kuwa pamoja kwa utu wao, ila bado sio manabii au mitume.
Mandela amefungwa kipindi kirefu, ila sioni kama kuwa kwake ndani kulikuwa kunamsaidia yeyote, zaidi ya yeye kunyimwa uhuru wake. Nina imani wako waliopoteza maisha, kupata vilema na hasara kubwa kwa kumpigania Mandela ila sio kinyume chake. Nyerere angeweza kuwa juu kabisa Kati ya waliojitolea kwa wengine ila si Mandela.
 
Sasa mkuu mbona hautaki kumjadili Paulo ambaye nae anadai alitokewa na Yesu?

Hivi unafahamu kutokewa kwa Paulo kuliacha au kuliambatana na mambo gani ambayo yalipita nguvu za kiasili? Kwa Muhammad kulitokea hivyo?
 

1. Kabla ya "kupewa" utume alikuwa ni mpagani na yeye alikuwa ni muabudu miungu Wa kabila lake la Kikureshi.


2. Kile unachokiona leo kuwa ni Hija ni transformation ya hija ya miungu midogo midogo na kubakiza mungu mmoja aliyeitwa "Allah" aliyekuwa hapo Kaba. Kulikuwa na jiwe moja kubwa jeusi lililoitwa "Allah" ambaye ndiye alikuwa mungu mkubwa miongoni mwa miungu wenu.
 
Ujumbe alopewa muhamad ausome ni mfupi sana kushindwa kuukariri ni ushahidi wa ukilaza wake
 
MAJIBU
1. hakuwa na dini wala hakuwa mshirikina , bali alikuwa mkweli na mwaminifu
2.Asili ya hiyo nyumba ya kuhiji sio wapagani, Quran imeweka wazi mjenzi wa nyumba hiyo ni Ibrahim na mwanae Ishmael, wapagani walivamia tu nakujimilikisha tu ,
3.Uislamu umeanza muda mrefu alichofanya mtume ni kuhuisha, kuhusu ukristo wenyewe wapo watakujibu alianzisha nani?
 
Ujumbe alopewa muhamad ausome ni mfupi sana kushindwa kuukariri ni ushahidi wa ukilaza wake
Hapa ndio napata wasiwasi na akili yako, kwa mara ya kwanza Mohammed anatokewa na malaika kibinadamu lazima awe na hofu , kwa hiyo ujumbe kutoukariri ni hofu za kibinadamu
 
Na kingine kukabwa na kuona vitu kama nyota ni matokeo ya oxygen deprevation iliyopelekea akapata visible hallucination probably ni kutokana na meditation yake kwenda wrong,baada ya kwenda kumsimulia mwenzake na kudanganyana plus influence ya mke wake ndo akaanza kujiita mtume kama musa na ibrahimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…