Marejesho ya VAT kwa watalii wa kigeni yaongezeka kwa kiasi kikubwa nchini China

Marejesho ya VAT kwa watalii wa kigeni yaongezeka kwa kiasi kikubwa nchini China

Yoyo Zhou

Senior Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
199
Reaction score
322
VCG111602860585.jpg
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Idara Kuu ya Kodi ya China zinaonesha kwamba, mwaka 2025, idadi ya watalii wa kigeni walioomba marejesho ya kodi ya nyongeza ya thamani (VAT) iliongezeka kwa asilimia 305, huku marejesho ya VAT yakiongezeka kwa takriban asilimia 96. Siku hizi watalii kutoka nchi mbalimbali duniani si kama tu wanatembelea sehemu maarufu kama vile Forbidden City na Ukuta Mkuu, bali pia wananunua bidhaa mbalimbali wanazopenda kwa kiasi kikubwa nchini China.

China inajulikana kama kiwanda cha dunia, bidhaa zake za ngazi mbalimbali zinawavutia watalii wa kimataifa. Licha ya hariri, chai, na sanaa za mikono, ambazo ni zawadi zinazopendwa sana watalii kutoka nje, sasa wanapenda zaidi kununua bidhaa za teknolojia za juu ikiwemo simu za mkononi, kompyuta na hata roboti, pia wananunua sana vinyago vya IP vyenye umaarufu mkubwa duniani katika maduka ya Pop Mart, nguo za mtindo wa Kichina na vipodozi vinavyochanganya ubunifu wa kitamaduni.

Ongezeko la manunuzi kwa watalii wa kigeni nchini China linatokana na ustawi wa soko la China na kupanuliwa zaidi kwa sera ya kufungua mlango. Mwaka jana, China ilishuhudia idadi ya watalii wa ndani kufikia bilioni 6.522, ambalo ni ongezeko la asilimia 16.2 kuliko mwaka 2024, na jumla ya mauzo ya rejareja ya bidhaa yalizidi yuan trilioni 50 sawa na dola trilioni 7.14 za kimarekani. Ustawi wa soko na ongezeko la kiwango cha huduma vimehimiza manunuzi kwa watalii wa kigeni nchini China. Zaidi ya hayo, sababu nyingine zikiwemo ongezeko la nchi zinazosamehewa visa ya kuingia China, kuboreshwa kwa mazingira ya malipo ya kimataifa, na ongezeko la safari za ndege za kimataifa, vyote vimerahisisha watalii wa kigeni kutembelea na kufanya manunuzi nchini China.

Ongezeo la manunuzi kwa watalii wa kigeni nchini China pia linatokana na uboreshaji wa sera ya kurejeshewa VAT na urahisi wa malipo. Shanghai imeanzisha mfumo wa kurejeshewa VAT kwa APP ya simu ya mkononi. Kwa kupitia APP hiyo, watalii wanaweza kurejeshwa VAT kwa simu yao ndani ya dakika chache tu. Mjini Beijing, takriban maduka makuu 18,000 yanakubali kadi za kigeni, na ATM 11,400 zinaunga mkono kadi za kigeni.

Ongezeko la haraka la manunuzi kwa watalii wa kigeni nchini China ni kama dirisha la kutazama maendeleo ya China. Linaonesha wazi njia ya kimkakati ya China ya “kuvutia rasilimali za kimataifa kuingia katika soko la ndani, na kukuza mzunguko mzuri kupitia mazingira wazi ya kibiashara.” Wakati “utalii nchini China” na “ununuzi nchini China” vinapoungana zaidi, matokeo yake si tu ni ongezeko la mapato ya utalii, bali pia ni ongezeko la vivutio vya China duniani.
 
Back
Top Bottom