Marekani achanganyikiwa baada ya nchi za OPEC Plus kutangaza kupunguza uzalishaji wa mafuta

eliakeem

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Posts
17,214
Reaction score
15,853
Nchi za Opec Plus zimekubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa sababu za kiuchumi. Lakini marekani yakurupuka na kusema Saudia amefanya njama na Urusi ili kupitisha azimio hilo.

Matokeo yake bunge lao wameanza kusema wataanza kupitia upya sera ya mahusiano na kati yake na Saudia.

Naona sasa wameona hakuna namna maana kwenye OPEC + Russia yuko ndani ya nyumba.

Nchi za OPEC + ni Azerbaijan, Bahrain, Brunei, Kazakhstan, Malaysia, Mexico, Oman, Russia, South Sudan and Sudan.

Chanzo: DW mchana.
 
Yaani ni hivi 👇👇😆😆

20221011_175026.jpg
 
Hiyo serikali ya kifalme ya Saudi Arabia iliwekwa madarakani na Marekani na Uingereza mwanzoni mwa miaka ya thelathini.

Hii serikali ya kifalme haina mustakbali wowote huko mbele na huyu mfalme wa sasa ndio atakuwa wa mwisho baadaye Saudi Arabia itakuwa na utawala wa kidemokrasia ambao utatenganisha siasa na mambo ya dini hali ambayo itapelekea Saudi Arabia kuwa na maendeleo makubwa.
 
kama maendeleo ya libya , au sio mkuu ?
 
Nchi za Opec Plus zimekubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa sababu za kiuchumi. Lakini marekani yakurupuka na kusema Saudia amefanya njama na Urusi ili kupitisha azimio hilo. Matokeo yake bunge lao wameanza kusema wataanza kupitia upya sera ya mahusiano na kati yake na Saudia.

Naona sasa wameona hakuna namna maana kwenye OPEC + Russia yuko ndani ya nyumba.

Chanzo: DW mchana.
Uzuri US ana kete zake haendi kinyonge, kingine mafuta anayo, na ndiyo maana ana ubavu wa kuamua kufanya hayo anayoyafanya sasa hivi na siku zijazo
 
Nchi za Opec Plus zimekubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa sababu za kiuchumi. Lakini marekani yakurupuka na kusema Saudia amefanya njama na Urusi ili kupitisha azimio hilo. Matokeo yake bunge lao wameanza kusema wataanza kupitia upya sera ya mahusiano na kati yake na Saudia.

Naona sasa wameona hakuna namna maana kwenye OPEC + Russia yuko ndani ya nyumba.

Chanzo: DW mchana.
Nilikuwa natazama aljazeera nikaona anaichimba mkwara Saudi Arabia kuwa kuna consequences za kuungana na mrusi.

Sasa jambo la kuchekesha ni kwamba wao marekani hawaongezi uzalishaji wa mafuta eti kwakuwa wawekezaji ya makampuni hao ya mafuta hawana uhakika kama wakiongeza uzalishaji bei haitoporomoka.

Pia IMF wanasema 2023 utakuwa mwaka ambapo hali ya uchumi itatikisika kinoma dunia itapitia magumu sana na chumi za nchi zitaanguka.
 
Unajua marekani sijui wanatuchukuliaje watu ambao si wamarekani.
Yaani wanachekesha sana.

Leo nilikuwa natazama aljazeera walikuwa wanazungumzia masuala ya energy mtangazaji akawa anasema ni kama vike ulaya wanapokuwa hawana shida wanasisitiza afrika isitumie fossil fuel ila sasa wao wanahamia huko kwa kasi wamesahau kuhusu mazingira kwakuwa shida imewakumba.

Ila wakati mambo mazuri na wakijua afrika 75% ya araia hawana umeme wanasisitiza tusitumie fossil fuel
 
Hiyo serikali ya kifalme ya Saudi Arabia iliwekwa madarakani na Marekani na Uingereza mwanzoni mwa miaka ya thelathini.

Hii serikali ya kifalme haina mustakbali wowote huko mbele na huyu mfalme wa sasa ndio atakuwa wa mwisho baadaye Saudi Arabia itakuwa na utawala wa kidemokrasia ambao utatenganisha siasa na mambo ya dini hali ambayo itapelekea Saudi Arabia kuwa na maendeleo makubwa.
Kwani Saudia haina maendeleo? Au sijakuelewa. Isije ikawa umemaanisha maendeleo ni uhuru wa watu kuoana jinsia moja.
 
Hiyo serikali ya kifalme ya Saudi Arabia iliwekwa madarakani na Marekani na Uingereza mwanzoni mwa miaka ya thelathini.

Hii serikali ya kifalme haina mustakbali wowote huko mbele na huyu mfalme wa sasa ndio atakuwa wa mwisho baadaye Saudi Arabia itakuwa na utawala wa kidemokrasia ambao utatenganisha siasa na mambo ya dini hali ambayo itapelekea Saudi Arabia kuwa na maendeleo makubwa.
Malekani amewekeza akili yake nyingi pale Saudi Arabia bila yao kuelewa ivyo. Wao wanakaaa wanawaza kuzaa na kuenda msikitini, subiri kinuke waanze kukimbizana na kumfata USA awasaidie. Dunia uwanja wa fujo, na asiyekuwa na nguvu kafa
 
Back
Top Bottom