Upepo wa Pesa
JF-Expert Member
- Aug 8, 2015
- 21,600
- 35,158
Biden wakati wa kampeni USA alimdhihaki mfalme wa Saudia, sasa naona ana mlipizia kisasi!Nchi za Opec Plus zimekubaliana kupunguza uzalishaji wa mafuta kwa sababu za kiuchumi. Lakini marekani yakurupuka na kusema Saudia amefanya njama na Urusi ili kupitisha azimio hilo.
Matokeo yake bunge lao wameanza kusema wataanza kupitia upya sera ya mahusiano na kati yake na Saudia.
Naona sasa wameona hakuna namna maana kwenye OPEC + Russia yuko ndani ya nyumba.
Nchi za OPEC + ni Azerbaijan, Bahrain, Brunei, Kazakhstan, Malaysia, Mexico, Oman, Russia, South Sudan and Sudan.
Chanzo: DW mchana.
Hao hawaivi chungu kimoja!Sasa Saudia bila US itakuwaje
Labda kama unaiongelea saudia ya chato.Hiyo serikali ya kifalme ya Saudi Arabia iliwekwa madarakani na Marekani na Uingereza mwanzoni mwa miaka ya thelathini.
Hii serikali ya kifalme haina mustakbali wowote huko mbele na huyu mfalme wa sasa ndio atakuwa wa mwisho baadaye Saudi Arabia itakuwa na utawala wa kidemokrasia ambao utatenganisha siasa na mambo ya dini hali ambayo itapelekea Saudi Arabia kuwa na maendeleo makubwa.
Mkuu watu wanafanya business wewe unaleta mihemko yako.Sijui OPEC walikuwa kweli wameungana na Russia kupigana na Marekani are they serious???? Let us see what will happen yetu macho
Kuna mhemko gani hapo, je wewe unachakufanya hapo au ni taarifa tu kwetu can we infuence anything there? Sinamhemko apo acha hizo habari.Mkuu watu wanafanya business wewe unaleta mihemko yako.
Kwa kifupi kwenye siasa za kimataifa hakuna rafiki wa kweli, usione USA anataka production iongezeke ukadhani anakupenda, anaangalia faida yake kama OPEC wanavyo angalia faida yao.
Kwahiyo OPEC wanafanya vyema kupunguza uzalishaji ili mafuta yapande bei? Wabongo kama siyo ukichaa tuna utindio wa ubongo
Ushakuwa sheikh yahya unatoa utabiri Hila kutabiri vya nchini kwako huweziHiyo serikali ya kifalme ya Saudi Arabia iliwekwa madarakani na Marekani na Uingereza mwanzoni mwa miaka ya thelathini.
Hii serikali ya kifalme haina mustakbali wowote huko mbele na huyu mfalme wa sasa ndio atakuwa wa mwisho baadaye Saudi Arabia itakuwa na utawala wa kidemokrasia ambao utatenganisha siasa na mambo ya dini hali ambayo itapelekea Saudi Arabia kuwa na maendeleo makubwa.
Mafuta USA anayo Kwa ajili ya matumizi yake tu na vile vile hayatoshi ndio maana Huwa anatafuta ya kujaziaUzuri US ana kete zake haendi kinyonge, kingine mafuta anayo, na ndiyo maana ana ubavu wa kuamua kufanya hayo anayoyafanya sasa hivi na siku zijazo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]kama maendeleo ya libya , au sio mkuu ?
Sasa anacholalamikia ni nini?,si angepiga kimya?,usilolijua ni sawa na usiku wa giza tororo,hujui kitu wewe,ni shabiki maandazi wa USAUzuri US ana kete zake haendi kinyonge, kingine mafuta anayo, na ndiyo maana ana ubavu wa kuamua kufanya hayo anayoyafanya sasa hivi na siku zijazo
Na bado tena nchi zinazoongozwa na mandezi kama hapa ,we subiri tutataftana humuNilikuwa natazama aljazeera nikaona anaichimba mkwara Saudi Arabia kuwa kuna consequences za kuungana na mrusi.
Sasa jambo la kuchekesha ni kwamba wao marekani hawaongezi uzalishaji wa mafuta eti kwakuwa wawekezaji ya makampuni hao ya mafuta hawana uhakika kama wakiongeza uzalishaji bei haitoporomoka.
Pia IMF wanasema 2023 utakuwa mwaka ambapo hali ya uchumi itatikisika kinoma dunia itapitia magumu sana na chumi za nchi zitaanguka.
Wabongo ni misukule , ukiyaona yanavyo jjiliza na inflation as if hayajui sababu mojawapo ya inflation ni kupanda Kwa BEI ya nishati ya mafuta na gesiKwahiyo OPEC wanafanya vyema kupunguza uzalishaji ili mafuta yapande bei? Wabongo kama siyo ukichaa tuna utindio wa ubongo
Kuna wale Wahouth WA Yemen na Iran , wanasema don't bite the hand that feeds you ,naona wamevimbiwa hawa wa Saudia ngoja balaa lianze hizo kobazi ,madela na vilemba vyao wataviona vizitoMalekani amewekeza akili yake nyingi pale Saudi Arabia bila yao kuelewa ivyo. Wao wanakaaa wanawaza kuzaa na kuenda msikitini, subiri kinuke waanze kukimbizana na kumfata USA awasaidie. Dunia uwanja wa fujo, na asiyekuwa na nguvu kafa
Kinachofata ni njaa huku Africa, vitu vitapanda bei maradufuSijui OPEC walikuwa kweli wameungana na Russia kupigana na Marekani are they serious???? Let us see what will happen yetu macho
Wewe mwenyewe ukijiangalia na ukiwaangalia wenzako hapo nchini kwenu mnajiona ni watu wa kawaida ?Unajua marekani sijui wanatuchukuliaje watu ambao si wamarekani.
Umemjibu vzr sana [emoji3][emoji3]kama maendeleo ya libya , au sio mkuu ?
Vita vya nishati ya mafuta vitatuumiza sana.