Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Hivi karibuni, Marekani imefanya kila iwezalo kwa kisingizio cha “usalama wa taifa” kuidhoofisha kampuni ya teknolojia ya Huawei, hata kuikashifu kuwa “mkiukaji wa haki za binadamu” na kutangaza kuweka vikwazo vya visa dhidi ya wafanyakazi wa Huawei. Lakini je, nani anayetishia zaidi usalama wa dunia na ni “mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu”? Jibu ni wazi.
Ni tishio dhidi ya maendeleo ya dunia
Jumanne iliyopita serikali ya Uingereza ilibadilisha uamuzi wake wa mapema mwaka huu, na kuizuia kampuni ya Huawei kushiriki kwenye ujenzi wa mtandao wa 5G wa nchi hiyo. Juu ya hilo, gazeti la The Guardian limefichua kuwa kabla ya tangazo hilo kutolewa, maofisa wa serikali ya Uingereza walikutana na wasimamizi waandamizi wa kampuni ya Huawei, na kuwaambia kuwa uamuzi huo umefanywa kutokana na “siasa za kijiografia”, yaani shinikizo la Marekani.
Kabla ya hapo, rais Donald Trump wa Marekani alisema hadharani kuwa yeye binafsi amezitaka nchi nyingine nyingi ziizuie kampuni ya Huawei kushiriki kwenye ujenzi wa mtandao wa 5G, la sivyo zitapoteza fursa ya ushirikiano wa kibiashara na Marekani, nchi mbili alizotaja ni Uingereza na Italia.
Kauli hiyo imefichua kuwa kuikataza kampuni ya Huawei hakuhusiani kabisa na usalama wa taifa, na pia watu wanafahamu kuwa Marekani ndio nchi inayofanya uchochezi hapa na pale na kukwamisha na kuyumbisha maendeleo ya nchi nyingine duniani. Gazeti la The Star la Kenya limeripoti kuwa huenda teknolojia ya 5G ya China imekuwa bora zaidi kuliko ya nchi za magharibi, na serikali ya Kenya haitakiwi kufuata nyanyo za Marekani na Uingereza na badala yake kuhakikisha kuwa kampuni za simu za Kenya zina haki ya kuchagua kwa uhuru wenzi wa ushirikiano wanaoweza kuleta maendeleo kwa mtandao wa 5G nchini Kenya.
Ni tishio dhidi ya afya ya binadamu
Hadi kufikia saa 7 alfajiri ya leo tarehe 21 kwa saa za Afrika Mashariki, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imezidi milioni 3.81, na watu laki 1.4 wamefariki dunia, idadi ambazo zote ni robo moja ya idadi za jumla duniani. Lakini baada ya rais Donald Trump wa Marekani kutangaza nchi yake kujitoa Shirika la Afya Duniani WHO, waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo, naye alisema China inatakiwa kulipia hasara zinazotokana na maambukizi makubwa ya virusi vya Corona duniani.
Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Kituo cha Kudhibiti Magonjwa cha Marekani CDC wikiendi iliyopita, virusi vilivyowaambukiza watu wa New York mapema mwezi Machi mwaka huu havikutokea China, kwani Marekani ilikuwa imewapiga marufuku watu kutoka China kuingia nchini humo mwezi Februari.
Ni kweli kuwa msimamo wa serikali ya Marekani wa “kuhusisha siasa kwenye sayansi” hauwezi kuisaidia kutokomeza virusi vya Corona nchini humo. Jambo la hatari zaidi ni kuwa kama bado kuna nchi duniani ina virusi vya Corona, nchi nyingine zote duniani hazitakuwa salama.
Marekani ni nchi yenye nguvu kubwa zaidi duniani, lakini ili kutimiza malengo yake ya kisiasa ya ndani na nje, imepoteza “mantiki, maadili, na uaminifu” kabisa, na hata imechoka kuwa kama ni nchi inayowajibika na maendeleo ya dunia na maisha ya binadamu. Marekani haijajiandaa vya kutosha na hata haipendi kupatana kwa usawa na nchi yoyote duniani, sio na China pekee. Katika mvutano wake na Marekani, China sio tu inajitetea kwa ajili ya maslahi yake binafsi, bali ni kwa ajili ya kupanua uwezekano wa kujiendeleza kwa nchi nyingine duniani.