Marekani hakuna Rais daktari, CPT, Engineer wala Advocate? Kwanini hawapendi kusoma?

Hii imekaa vizuri. Siyo huku kwetu mpaka Msukuma na mwenzake Babu Tale eti nao wanajiita Dokta Msukuma! Dokta Babu Tale!! Halafu elimu yenyewe unakuta darasa la 7 au form four failure!!
 
Huku kwetu kila kiongozi anaona ni ufahari kuitwa Dr. Hata kama kichwani ni empty head. Badala ya kuumiza vichwa kuzifanyia nchi zao mambo makubwa; wao wako busy kupeana, na hata kununua kabisa vyuoni hayo majina ya Udokta!!
Tunapenda title. Mtu anajiita wakili msomi na uwakili wake ni wa cheti tu hautatui matatizo ya jamii kesi za serikali tunashindwa huko nje.
 
Sijawahi kujua kumbe paroko wetu ni Dr. Jamaa yangu ndio alikuja kuniambia Kuwa alisoma na paroko ni Phd holder.
Baadhi ya Watawa, Mapadre na Maaskofu wa Katoliki wana sifa ya kuitwa Madokta na pia Maprofesa! Ila huwezi kuwakuta wanajikweza kiasi hicho.

Maana wanatambua fika vyeo vyao vya Kanisa ni Utawa/Upadre/Uaskofu! Ila wangekuwa ndiyo hawa ndugu zangu; pangechimbika.
 
Hakika!
 
Acha direct translation from English to Kiswahili.
He was admitted to law bar (alilazwa kwenye baa ya sheria)
 
Sisi tunae Dr. SSH. Hutaki acha.
 
Sijasoma hadi mwisho
Nimekisoma kichwa cha habari tu na kugundua kina kasoro au kimeandikwa ili kuvutia wasomaji.

Si kweli kwamba Marekani haijawahi kuwa na Rais msomi.
Wapo. Wapo hadi level ya Professor.
Nchi yao hairuhusu kutumia utambuzi wa taaluma yao. Ni marufuku kabisa.
 
Viongozi wenyewe tulio nao ndio hawa ambao anasimama hadharani na kusema kama sio Samia mzazi wake angekufa kabla ya siku
 
Hapana. Obama, Clinton, na Biden hawana PhD.

Wana JD, ambayo ni Juris Doctor.

Juris Doctor si sawa na PhD.

Juris Doctor ni shahada ya sheria Marekani. Kila mwanafunzi anayehitimu shule ya sheria Marekani hutunukiwa JD.

PhD ni research doctorate.

Nadhani kinachowafanya mdhani kuwa Obama ana PhD ya sheria ni hilo jina la Juris Doctor.

Kwa taarifa yako, kila wakili Marekani ana JD. Hata wale DUI lawyers nao wana JDs. Divorce lawyers nao wana JD.

JD si sawa na PhD.
 
Je mkuu wa mkoa kujiita CPA makala Je hii 👆 ni sawa
 
Naona maneno yanawachanganya.

Kwanza kabisa, Marekani mwalimu wa chuo huitwa profesa.

Pili, Obama ana shahada ya sheria. Shahada ya sheria Marekani huitwa JD au Juris Doctor.

Kila mwanafunzi anayehitimu shule ya sheria huko Marekani, hutunukiwa JD.

Kwa msingi huo, kila wakili Marekani aliyesoma na kuhitimu kwenye chuo kilichopo nchini humo, hutunukiwa Juris Doctor degree.

Juris Doctor degree si sawa na PhD na ndo maana watu walio na shahada za sheria Marekani huwa hawatumii huo utambulisho wa Doctor.

Marekani hata cheti cha sekondari huitwa diploma. Lakini huwezi kulinganisha high school diploma ya North Forsyth High school na Diploma itolewayo Mzumbe.

Maneno na matumizi yake naona yanawachanganya.
 
Familia pekee mbili za Marekani zilizaowahi kushika Urais wa Marekani mara mbili

2. John Adams (1797-1801)
6. Andrew Jackson (1829-1837)

41. George H. W. Bush (1989-1993)
43. George W. Bush (2001-2009)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…