Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Historia ya Marekani ilianza kwa raia walioondoka Ulaya hasa Uingereza kuanzia karne ya 16 kwa sababu mbalimbali lakini kubwa zaidi zikiwa ni mbili, fursa za uchumi na mkandamizo wa dini.
Kipindi cha karne ya 15 hadi 17 kulikuwa na mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali Ulaya ikiwemo misuguano ya kidini na kimadhehebu iliyopelekea serikali za kifalme kulazimisha watu wafuate madhehebu yao, serikali ya Uingereza iliwanyanyasa Wakatoliki, serikali ya Ujerumani iliwanyanyasa ambao hawakuwa Walutherani, Spain na nchi nyingine za Wakatoliki wengi waliwanyanyasa ambao hawakuwa Wakatoliki, hawa wanyanyaswaji wenye dini, wasio na dini na raia wengine wengi ambao walikuwa kimaslahi ya uchumi tu ndio waliozamia Marekani na Canada ambayo yalikuwa makoloni ya Uingereza na Ufaransa kuwa wahamiaji masetla. Kipindi hicho Marekani ilikuwa kama shamba la wakoloni kuchuma mali, gereza la kutupia watu watukutu walioshindikana Ulaya na pia mojawapo ya eneo la makafiri/ "barbarians"/heathens.
Baada ya Historia ndefu sana hatimaye Masetla waliojipata wakachoshwa na utawala wa Ufalme wa Uingereza na kujitangazia uhuru kutoka ufalme mwaka 1776 na vita virefu vikapiganwa sana na Uingereza. Hatimaye mwaka 1787 wakijitungia katiba yao na mojawapo ya mambo makubwa waliyozingatia sana katika katiba yao kutokana na vidonda vya historia yao ikawa ni kudhibiti pakubwa mamlaka ya watawala na serikali na pia kutenganisha kabisa mambo ya kidini na serikali.
Waanzilishi wa taifa(founding fathers) walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili, Wakristo na waamini mungu tu kwa namna nyingine ambao hawakuwa Wakristo(Deists). Hawa Deists kwa kiasi kikubwa wakiwemo kina George Washington, Thomas Paine, Alexander Hamilton na wengine ndio walioukuwa vinara wa mambo na uundaji wa katiba yenyewe na waliweka hadi kipengele katika katiba kinachosema Congress haitahusika na kuheshimu, uanzishwaji wa dini yoyote au kuzuia uhuru wa dini yoyote.
Bado ya hapo japo dini ya Ukristo iliendelea kuwa ya umuhimu kwa Wamarekani wengi lakini hakukuwahi kuwa na uchanganyaji wa dini na siasa mpaka miaka ya 1980 alipoingia madarakani Ronald Reagan, katika uchaguzi wake mambo ya kidini yalijaribiwa kutumika kama ajenda na yalimuongezea nguvu zaidi za ushindi ndipo ikawa kama "jini amechoropoka kwenye chupa", tangu wakati huo mpaka leo hii mambo ya kidini yameendelea kutumika kama karata muhimu sana katika siasa za Marekani na yamezidi kuwagawanya vibaya kwa sababu mambo ya kidini siku zote yanaendeshwa kwa hisia zaidi kuliko logic na "pragmatism", hata support kubwa ya Marekani kwa Israel hisia za kidini zinahusika sana pia