The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Huawei ilikua inakuja vizuri sana kwa miaka 3 iliyopita. Ghafla bin vuu mwaka jana ikawekwa kwenye black list ya serikali ya Marekani ikaanza kupambana na vikwazo.
Sasa Huawei imeanza kupoteza hata ile miradi na mikataba iliyokua imepata ya kufunga mitambo ya 5G. Uingereza iliipa Huawei ila sasa imebadilisha msimamo, inategemewa hivyo hivyo kwa Hispania, na nchi kadhaa kubwa Ulaya kujiondoa kwenye mikataba na Huawei.
Uingereza inasema ni kwa sababu ya vikwazo vipya vinavyotegemewa kutangazwa September, Huawei haitakua na uwezo wowote wa hata kuzalisha vifaa vinavyohitajika sio kwa 5G wala kwa simu zake zote kwa sababu haitakua na uwezo wa kutengeneza chip yake ya Krin.
Sababu ni moja kubwa, teknolojia ya kisasa zaidi inayotumika kuzalisha vifaa vya 5G au chip za simu 90% ina mkono wa Marekani. Kwa sasa Huawei hupata baadhi ya teknolojia kwa kibali maalumu cha serikali ya Marekani. Inategemewa kuanzia September hali inaweza kua mbaya zaidi kwa Huawei.
Marekani imebadilisha tuhuma kwa Huawei kua ni tawi la jeshi la China hivyo itakabiliwa na vikwazo vyote vinavyohusu jeshi la China.
Why Huawei's days in the UK could be numbered