Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Ukraine na Ulaya wamejifunza kwa uchungu sana, Marekani yawakataa

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
3,651
Reaction score
11,548
Mwaka 1968 aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje ya Marekani Henry Kissinger alisema:

"Inaweza kuwa hatari kuwa adui wa Marekani, lakini kuwa rafiki wa Marekani ni majanga."
– Henry Kissinger

Na Marekani imethibitisha kuwa Kissinger alikuwa sahihi. Mara kwa mara, Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Zamu hii Ukraine na Ulaya wamejifunza.

Akizungumza na washirika wa NATO mjini Brussels, Belgium, Waziri wa Ulinzi wa Marekani alitoa matamshi ambayo naamini mpaka sasa Zelensky na viongozi wa Ulaya hawaamini macho yao.

"Hakuna uanachama wa NATO kwa Ukraine"

"Hakuna vikosi vya Marekani kwenda nchini Ukraine"

"Hakuna askari wa NATO kwenda nchini Ukraine. Lakini nchi za Ulaya zinaweza kutuma wanajeshi wao wenyewe.”

"Lazima tuanze kwa kutambua kwamba kurudishwa kwa mipaka ya Ukraine ya kabla ya 2014 ni lengo lisilowezekana, kufuatia lengo hili lisilowezekana kutaongeza muda wa vita na kusababisha mateso zaidi."

"Wanajeshi wowote wa Uingereza au Ulaya ambao walitumwa nchini Ukraine hawatakuwa chini ya misheni ya NATO au na dhamana ya kifungu cha 5 cha muungano huo, watategemea usaidizi kutoka kwa mataifa yanayoshiriki."

– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)

Na kama haitoshi naye Trump alifanya mazungumzo na Putin kwa saa 1:30 wakaafikiana kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa watakutana Saudi Arabia mada kuu itakuwa suala la vita ya Ukraine.

Lakini wakati huohuo Trump alitumia dakika 10 tu kuongea kwenye simu na Zelensky.

Ukraine imeambulia kupoteza mamia ya maelfu ya askari, mamilioni ya Waukraine wamekimbia nchi yao, wamepoteza karibu 20% ya ardhi yao na uchumi na miundombinu mingi kuharibiwa na Urusi.
 
Kwa sasa taifa pekee ambalo Marekani analihofia duniani ni China.
"Pia tunakabiliwa na mshindani China anayeweza kutishia Marekani na maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacific. Marekani imekuwa ikibadilisha vipaumbele vyake vya kijeshi kwa kulinda nchi yake na kuizuia China."

– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)​


Hapo kwa China wasipoteze muda na pesa Trump mwenyewe anajua hilo alijaribu 2018-2021 akafeli vibaya mno.
 
Trump ni pandikizi la Putin
Sidhanii hivyo,ninachofikiri ni kua Trump kaona ukweli kua NATO wameishindwa Urusi na ukweli ni kua, Ukraine imepoteza watu wengi mno pamoja na sehemu ya ardhi,kuendelea kupigana na Urusi ni kuendelea kuua watu na kupoteza ardhi zaidi,na uzembe ukifanyika TU, vita vya nyukilia vinaweza kuibuka.

Hapa ni akili ya kiutu uzima TU imetumika, sio kama akina Biden wapenda damu.
 
We are strong together than alone.

Ukraine inahitaji support ya kila aina kutoka Nchi wananchama wa NATO, kama Marekani imekataa kwa sababu zake za siasa za ndani, basi wanachama waliobaki wajipange au waunde ummoja mpya na wamkaribishe mwenzao wakimuacha wanamkaanga.

Acha ajitoe akili lakini iko siku atatamani kushirikiana na yeyote hata Somalia na hatopata. Inaweza kuwa dua la kuku.
 
Wamempiga nyuki busu wakajua maumivu yake alafu wewe unashauri waendelee na huu mchezo?

Tangu 2014 nawaambia wajinga kama wewe kuingia vitani na Urusi ni sawa na kudumbukia kwenye tanuru la kuyeyusha vyuma.
Falme nyingi zimeijaribu urusi zikapotea usije kufikiri marekani ni mjinga
 
NATO ni Marekani! Akishasema huyo, hao wengine ni bendera tu fuata upepo. Kwa hiyo usitegemee maamuzi au kauli nyingine tofauti na hiyo.
 
Zelensky tulimshauri mapema akagoma, wacha tu apewe za uso
 
Maskini, pole sana mkuu, inauma sana ila ukweli ni kwamba Ukraine keshatumika na wakati wake wa kutupwa umefika rasmi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…