Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
Mwaka 1968 aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje ya Marekani Henry Kissinger alisema:
"Inaweza kuwa hatari kuwa adui wa Marekani, lakini kuwa rafiki wa Marekani ni majanga."
– Henry Kissinger
– Henry Kissinger
Na Marekani imethibitisha kuwa Kissinger alikuwa sahihi. Mara kwa mara, Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Zamu hii Ukraine na Ulaya wamejifunza.
Akizungumza na washirika wa NATO mjini Brussels, Belgium, Waziri wa Ulinzi wa Marekani alitoa matamshi ambayo naamini mpaka sasa Zelensky na viongozi wa Ulaya hawaamini macho yao.

"Hakuna uanachama wa NATO kwa Ukraine"
"Hakuna vikosi vya Marekani kwenda nchini Ukraine"
"Hakuna askari wa NATO kwenda nchini Ukraine. Lakini nchi za Ulaya zinaweza kutuma wanajeshi wao wenyewe.”
"Lazima tuanze kwa kutambua kwamba kurudishwa kwa mipaka ya Ukraine ya kabla ya 2014 ni lengo lisilowezekana, kufuatia lengo hili lisilowezekana kutaongeza muda wa vita na kusababisha mateso zaidi."
"Wanajeshi wowote wa Uingereza au Ulaya ambao walitumwa nchini Ukraine hawatakuwa chini ya misheni ya NATO au na dhamana ya kifungu cha 5 cha muungano huo, watategemea usaidizi kutoka kwa mataifa yanayoshiriki."
– Pete Hegseth (Waziri wa ulinzi wa Marekani)

Na kama haitoshi naye Trump alifanya mazungumzo na Putin kwa saa 1:30 wakaafikiana kuwa mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa watakutana Saudi Arabia mada kuu itakuwa suala la vita ya Ukraine.
Lakini wakati huohuo Trump alitumia dakika 10 tu kuongea kwenye simu na Zelensky.
Ukraine imeambulia kupoteza mamia ya maelfu ya askari, mamilioni ya Waukraine wamekimbia nchi yao, wamepoteza karibu 20% ya ardhi yao na uchumi na miundombinu mingi kuharibiwa na Urusi.