Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Ukraine na Ulaya wamejifunza kwa uchungu sana, Marekani yawakataa

Baada ya NATO kushindwa mbele ya URUSI ndo wanakili hadharani kwamba walikuwa Ukraine waliingia kwa kificho wakiwa hai sasa wanaondoka hadharani wakiwa marehemu! Hiyo ndiyo urusi ninayoijua
Umesema vyema

Urusi ni lidude fulani hivi ambalo NATO wamekubali kusanda

Kama mkuu wao Marekani kakiri Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Poland n.k wao ni nani
 
Ni vile tunaishia kusimuliwa tu izi habari akuna aliyepo eneo la tukio akashuhudia mwenyewe yanayoendelea,lakini usikute hata Aya madai ya urusi kuweza kuteka asilimia 20 tu ya ardhi ya ukreni uwenda nao uwongo tu
Mambo yako wazi wakiwa Brussels ulikuwa ni mkutano ambao waandishi wa habari walikuwepo.

Unajua ni miji mingapi ya Ukraine mpaka sasa iko chini ya Urusi
?​
 
Trump Kwa hapo kaupatia sana ni ukweli usiopingika kuwa hii vita ilikokua inaelekea ni kubaya zaidi na kama wasingechukua hatua ni kuwa vita vya nyuklia vingeibuka na ingekuwa ni disaster, hakuna ya kuing'ang'ania Ukraine kuwa mwanachama wa jumuiya ya NATO ni Bora kuafiki matwaka ya namba mbili Kwa idadi kubwa ya silaha za nyuklia kuliko kuiruhusu Dunia kuingia vita vikuu vy a 3 ambayo ingekuwa more deadly than any war before, I congratulate Donald Trump
 
Natamani dunia nzima imtenge au uachane nao USA.
Tunaposema dunia inahitaji balance of power watu wawe wanatuelewa kuwa kuifanya dunia iendeshwe na taifa moja matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona tangu Trump aapishwe

Watu huwa wanakuwa wajinga kuisifu sifu Marekani sijui superpower ni kosa kubwa sana. Umeona wamesitisha misaada kama dawa za ARV waathirika ambao walikuwa wanaisifu Marekani superpower wameanza kutoa vilio

Ndio mana tunataka mataifa mengine ya kuichallenge kiuchumi, kiteknolojia, nguvu za kijeshi na misaada ili Marekani isijione bila yeye mambo hayaendi

Tayari Mrusi kashaonyesha hilo hapo Ukraine, Marekani katulizwa kakaa. Na China inafanya hivyo kiuchumi, kiteknolojia na kupitia foreign aids

Hiki ndicho tunaita balance of power tunaihitaji sana hii kitu duniani, ilipotea tangu kuanguka kwa Soviet Union miaka ya mwanzoni mwa 1990
 
Ni wakati Ulaya ikajitathimini
Ni wakati wa nchi za Ulaya kuwa na ushirikiano na China na Russia dunia ya sasa inahitaji win-win cooperation sio sera za Marekani za win-lose cooperation

Tatizo la nchi za Ulaya zimekubali kuwa U.S vassal states, wamekubali internal na foreign policies zao zitegemee sera za Marekani wanaumia sana, ndicho anachopitia Japan, South Korea, Canada, Australia na U.S vassal states nyingine.

Leo uchumi wa Ujerumani unaotegemea viwanda, uzalishaji viwandani umeporomoka kwa sababu ya kupanda kwa gharama za nishati ambazo awali walikuwa wananunua Urusi kwa bei rahisi, Marekani akalipua Nord Stream pipeline ili awauzie LNG kwa bei kubwa

Mafuta wanauziwa na India ambayo nayo inanunua Urusi na kuwauzia kama third party kwa gharama kubwa

Na bado Marekani inawatisha kwa kuwapandishia tariffs bidhaa zao.

Mchina aliona mbali kafanya juu chini kuhakikisha kuwa soko lake kubwa la bidhaa lisitegemee Marekani, kwa sasa soko kubwa la China ni Global South countries.

Ukiwa trade partner mkubwa wa Marekani lazima akutese sana kama Canada, Mexico na Japan zinavyoteswa na tariffs.

Siku hizi Mchina anafanya tit for tat Marekani akitia tariffs na yeye anampandishia tariffs kwa sababu soko la Marekani sio kipaumbele kwake.

Marekani ni kwenda naye kibabe kama Urusi na China zinavyofanya
 
Noma sana!
 
hv unajuwa hali ya Urusi sas hv ? Urusi wamefikia hatua ya kusema liwalo na liwe ika sio kwamba ukimya wao unamaanisha wapo vzr , Trump katumia busara , Hii vita imempa fursa nying China na lzn wafanye maamuz kama haya ili China asiwapige gap kubwa , kipind cha hii vita ndo China kapata ushawishi mkubwa baran kwake Asia ambako wengi walikiwa hawamtaki pia Ndo kipind China kawatoa rasmi wazungu huku Afrika , pia ndo kipind China kaanza tawala soko la Ulaya , pia ndo kipind China amepanya option ya kuiangusha USA kwa kuitumia Urusi , so ni lzm Trump arud nyuma aweke sw ila bila uwepo wa China kama superpower bas USA angemvagaa Urusi na kumdunda vzr maana hata kama angerud nyuma bas bado angekuwa kileleni maana kutoka yeye hadi mtu wa tatu anamzid krb mara 2 ila huyu wa pili yake yupo makalion , USA akidelay kdg China anakaa Mbele zaid , so uwepo wa China km mshindani wa USA ndo umefanya Trump afanye hayo maamuz
 
upo sahihi kbs lkn pia sio sahihi kuitenga USA , ni vyema Ulaya hata na Afrika pia tukawa na, urafik na kila upande bila kuchagua maana sio vyote utavipata kwa mataifa ya mashariki
 
Trump ni mwanauchumi na sio mtapanya pesa kwenye vita
 
Hivi mbona sijawahi kusikia shirika la misaada la Urusi? Lakini pia mbona sijawahi kusikia shirika la misaada la China? Walau Japan kuna JICA na Sweden kuna SIDA, ila hao giants Urusi na China wao ni maneno tu, misaada aaaah!
 
Hivi ww jamaa unajua unakiandika kwanza au unaropoka tu?
 
Kwaher crimea tutaonana Ukraine akiwa na nuclear weapons ambapo babu Putin atakuwa ardhin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…