Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Ukraine na Ulaya wamejifunza kwa uchungu sana, Marekani yawakataa

Marekani imeonyesha kuwa si mshirika wa kutegemewa katika masuala ya kimataifa. Ukraine na Ulaya wamejifunza kwa uchungu sana, Marekani yawakataa

Urusi inayotumia hadi wanajeshi wa Korea Kaskazini ya Kim Kiduku na kuchukua silaha kutoka China??
Hakuna ushahidi kuwa Urusi inatumia wanajeshi wa Korea Kaskazini

Ila kinachojulikana ni kuwa Ukraine inatumia mercenaries kutoka nchi za Ulaya

Na mengi tumeyasikia katika ripoti ya waziri wa ulinzi wa Marekani ambayo tulikuwa hatujui
 
Dunia ya balance of power ya USSR babu zako walikuwa wanavaa suruali zenye matobo na viraka kwenye makalio, ilikuwa dunia ya hovyo sana ndio maana USSR ilianguka na Western order ikachukua ushawishi wa dunia.
Dunia yenye ushawishi mkubwa wa China itakuwa mbaya sana pia.
Wakati wa USSR wasomi wengi kutoka nchi za 3rd world countries walipata scholarship ya kwenda kusoma katika mataifa ya Soviet

USSR ilisupport kuondoa ukoloni kwa mataifa mengi ya Afrika na maeneo mengine duniani kwa moral, material na diplomatic support

USSR ilitoa msaada wa kiuchumi na financial aid, ikawa alternative kwa matifa mengine ambayo hayakuunga mkono sera za capitalism za nchi za Magharibi

Moral support gani kutoka kwa USSR iliyokuwa inazishikilia nchi nyingi mateka katika umoja huo?
Watu gani wa maana waliosoma USSR unaowajua?
 
Dunia yenye ushawishi mkubwa wa China itakuwa mbaya sana pia.
Tofauti ya China na Marekani ni kubwa sana inapohusu ushawishi.

Mchina yeye haingilii internal affairs anapokuwa na bilateral au multilateral cooperation na mataifa mengine.

Kupitia BRI Mchina anajenga miundombinu ili kulisaidia taifa analoshirikiana nalo Marekani anajenga miltary base.

Inapohusu misaada katika mfumo wa capital kwa sasa China ndio inaongoza kuizidi Marekani na nchi zingine kwa pamoja.

China imefanya leo watu wengi waweze kuafford kununua bidhaa kwa gharama nafuu hasa kwa nchi masikini. Leo ni wachache sana wangeweza kuafford kununua bidhaa za Magharibi.

China builds U.S bombs. Marekani ndiyo taifa linaongoza duniani kwa kuuza silaha, China inaongoza kwa kuuza bidhaa za viwandani kwa matumizi ya amani.

Nikupe mfano mmoja wa jinsi ushawishi wa China ni wenye matokeo chanya. China iliwapatanisha viongozi wa Iran na Saudi Arabia pale ilipowaita Beijing. Tukio ambalo Marekani alichukua sana Marekani anataka kuwe na uadui kati ya mataifa hayo yeye anawaza vita tu vipiganwe.

Ushawishi wa Marekani umeleta matokeo yasiyo mazuri duniani mfano umechangia mapinduzi ya kijeshi yakiongozwa na CIA viongozi wengi wamepinduliwa na kuuwa kwa sababu tu hawakuunga mkono sera za Marekani. Marekani imechangia sana kwenye unnecessary wars and conflicts worldwide.

Kwa kumalizia Marekani ni warmonger, nitajie taifa ambao China imewahi kulivamia kijeshi na kivita. Marekani imeua mamilioni ya watu wasio na hatia na bado wanaendelea kuua.

20250214_085058.jpg

20250214_085240.jpg
 
Moral support gani kutoka kwa USSR iliyokuwa inazishikilia nchi nyingi mateka katika umoja huo?
Watu gani wa maana waliosoma USSR unaowajua?
Waliwapa morale ya kuwaondoa wakoloni

Miaka ya 1970s na 1980s Watanzania wengi walipata scholarship ya kwenda kusoma USSR
 
Tofauti ya China na Marekani ni kubwa sana inapohusu ushawishi.

China imefanya leo watu wengi waweze kuafford kununua bidhaa kwa gharama nafuu hasa kwa nchi masikini. Leo ni wachache sana wangeweza kuafford kununua bidhaa za Magharibi.
China imesababisha sekta ya viwanda nchi za Africa kufa kabisa, leo hii hadi makabati, viti na meza vinatoka China!
Hatuna viwanda vya nguo, nguo karibia zote zinatoka China.
 
Tofauti ya China na Marekani ni kubwa sana inapohusu ushawishi.

Inapohusu misaada katika mfumo wa capital kwa sasa China ndio inaongoza kuizidi Marekani na nchi zingine kwa pamoja.
Acha projo zako, China haina utaratibu wa kutoa misaada, inatoa mikopo tu na usipolipa inakukamua mpaka utapike pesa yao.
 
Tofauti ya China na Marekani ni kubwa sana inapohusu ushawishi.

Kwa kumalizia Marekani ni warmonger, nitajie taifa ambao China imewahi kulivamia kijeshi na kivita. Marekani imeua mamilioni ya watu wasio na hatia na bado wanaendelea kuua.
Mao Zedong mwanzilishi wa Jamuhuri ya China aliua raia wake wachina zaidi ya milioni 40.
 
China imesababisha sekta ya viwanda nchi za Africa kufa kabisa, leo hii hadi makabati, viti na meza vinatoka China!
Hatuna viwanda vya nguo, nguo karibia zote zinatoka China.
Tutajie viwanda vilivyokufa Tanzania kwa sababu ya bidhaa kutoka China

Hapo mkoa wa Pwani viwanda vinajengwa kila siku na wawekezaji wakubwa ni Wachina
 
We are strong together than alone.

Ukraine inahitaji support ya kila aina kutoka Nchi wananchama wa NATO, kama Marekani imekataa kwa sababu zake za siasa za ndani, basi wanachama waliobaki wajipange au waunde ummoja mpya na wamkaribishe mwenzao wakimuacha wanamkaanga.

Acha ajitoe akili lakini iko siku atatamani kushirikiana na yeyote hata Somalia na hatopata. Inaweza kuwa dua la kuku.
Bila US hakuna NATO!
 
Mao Zedong mwanzilishi wa Jamuhuri ya China aliua raia wake wachina zaidi ya milioni 40.
Hizo ni propaganda za nchi za Magharibi

"When I say the United States is evil, I mean its ruling class. The American people are pretty good. Many of them haven't awakened yet, but they will."
–Mao Zedong
 
Mao Zedong aliua raia wake wachina wangapi kulingana na taarifa za China??
 
Back
Top Bottom